Kuporomoka kwa Bei ya Brevis

RPM max ngapi kupata 13km/l kwenye 4GR? Combined fuel rate ngapi?
Isizidi 2000 (2), crown ina nguvu rpm ikivuka moja tu chuma inasepa, usiilazimishe acha gari iende yenyewe utakuja kunishukuru baadae. Zingatia usipende kupata speed kubwa kwa muda mfupi itakughanimu kwenye mafuta maana rpm lazima iende juu sana. Kama ulishafatilia waendeshaji weng wa crown ni wastaarabu sana huwezi sikia muungurumo wa crown labda iwe mbovu, huwa zipo kimya kimyaaaa.
 
Hahahahah crown huwa kama inateleza tu ukiegesha mguu 🤣
 
RPM max ngapi kupata 13km/l kwenye 4GR? Combined fuel rate ngapi?
Gari yoyote ya Toyota ukiwa na soft foot haili wese. Hasa hizi zenye VVT-i tech.

We egesha mguu kidogo tu, itabadili gear haraka na utashangaa inapandisha speed tu yenyewe hadi kufikia optimum speed ya 80km/h bila kuvuka RPM ya 2.

Ila ukiwa mtu wa masifa unataka gari kuilazimisha kupandisha speed haraka itang'ang'ania gia namba 2 mda mrefu na rpm zitafika hadi 3 au zaidi. Wese linalika gari haiendi sana.
 
Mkuu,,, hizo gari ni hatar,,, mi nilishawah kuwa nayo naweka mafuta elfu 30 lkn dashboard inasoma red,,, zinakula sana mafuta hizo,,,
 
Kwa highway ni sawa jombaa, mimi Mark X nilishatembea kwa 17km/L speed 80kmph.
Mkuu highway unamaanisha ukitoka Dar-Moro au Kimara-Posta? Stop and Go traffic sidhani kama kuna V6 itakuacha salama. Kama kuna mwenye crown naomba picha ya 13km/l ikiwa kwenye foleni au hata 9km/l
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…