Kuporomoka kwa Bei ya Brevis

BREVIS na PASSO bei zake huwa sielewi why zinakuwaa chini hata kama gari unaonaa ni mpyaa na kali sanaa.
Nadhani maintainance, Brevis kwa mwezi inakula kodi ya nyumba, kama unaiweza haina shida. Passo nadhani iko weak sana (body na engine), hivyo maintainance mara kwa mara ila mafuta kiduchu.
 
Wese, raia wengi maisha ya kubangaiza...

Pia mafundi wengi wanaigwaya engine yake, shida kidogo ya engine wanahenya kweli kweli...

Ila ni gari moja matata sana kwenye kukata upepo..
Kuchomoka inachomoka 🔥
 
Crown ziko standard sana kilomita 12 unatoboa freshi tu ..watu wengi wanoengelea kula mafuta sana hawajazitumia wanasikia tu stori baada ya kusikia engine capacity ..crown zile gari zimeboreshwa sana wamezibalance na umeme ulaji wake wa mafuta sio mkubwa kama watu wanvyotishana...
 
mh!mkuu hii ya kwako nayo mpya,ukileta kaimahesabu haiji kabisa,labda pikipiki,,full tank ya allex ni 50 litres,robo tank ni 12.5 litres,
485km/12.5litres=38.8km kwa litre 1?mh hii ngumu,labda kama mimi sijaelewa.
 
Mazda ile tech yao ya Skyactiv ni bonge moja la tech, hata ukute engine kubwa ya petrol bado ina consumption nzuri tu.
 
Premio la,ima iwe kimbilio zaid kwa sababu yenyewe inatembea km nyingi kuliko crown, ns ndio maana premio zilizojazana hapa bong ni za cc 1496 na kidogo zinafata 1790 zile zenye cc 2000 ni za kutafuta kwa tochi na hazina soko kabisa.
Premio za Cc2000 watu hawazinunui sana siyo kwa sababu ya Consumption. Ila kwa sababu ya aina ya engine.

Premio ya Cc1990 haitofautiani kabisa consumption na premio ya Cc1790
 
Premio za Cc2000 watu hawazinunui sana siyo kwa sababu ya Consumption. Ila kwa sababu ya aina ya engine.

Premio ya Cc1990 haitofautiani kabisa consumption na premio ya Cc1790

Skyactive inafanya mazda kuwa bora sana kwene engine hizi mpya….

Najiuliza kwanini wasi innovate hii technology zaidi dunia iachane na hybrid [emoji28]
 
mh!mkuu hii ya kwako nayo mpya,ukileta kaimahesabu haiji kabisa,labda pikipiki,,full tank ya allex ni 50 litres,robo tank ni 12.5 litres,
485km/12.5litres=38.8km kwa litre 1?mh hii ngumu,labda kama mimi sijaelewa.
Najua huwezi amini ila ndio ipo hvyo, nilifikka Morogoro mshale bado upo kwenye F, tatizo ni uendeshaji mkuu, speed kumbwa ambayo nilitembea siku ile ni 120km/h na ni kule dumila kuna sehemu hakuna 50 kipande kirefu sana.
 
Premio za Cc2000 watu hawazinunui sana siyo kwa sababu ya Consumption. Ila kwa sababu ya aina ya engine.

Premio ya Cc1990 haitofautiani kabisa consumption na premio ya Cc1790
Na yote hii ni kwa sababu ya kukaririshwa kuwa injini yoyote kubwa inatumia mafuta mengi zaidi kumbe sio zote.

Premio ya 2000cc hadi imekosa soko kisa eti ina injini kubwa na watu wanaambiana kabisa usinunue premio yenye injini kubwa.
 
Wabongo ni watu wakukariri sana pia wanatishana sana..wanataka utumie IST tu ndio kitu walichoambiana
 
Wabongo ni watu wakukariri sana pia wanatishana sana..wanataka utumie IST tu ndio kitu walichoambiana
Ni kweli kabisa, niliwahi kuona be forward wakielezea kuwa Ist old ya cc 1290 inatembea km14 had 18 wakati Ist ya 2009 inatembea km 18 hadi 23 kwa lita, hapo ndio utashangaa hadi leo watu wanakimbilia Ist old na ni kwa sababu ya kufata mkumbo tu.
 
Hizo gari ni nyonya damu kama una kipato Cha ching....
 
Na yote hii ni kwa sababu ya kukaririshwa kuwa injini yoyote kubwa inatumia mafuta mengi zaidi kumbe sio zote.

Premio ya 2000cc hadi imekosa soko kisa eti ina injini kubwa na watu wanaambiana kabisa usinunue premio yenye injini kubwa.
Premio ya Cc2000 inakupa performance karibu sawa na engine ya Cc2400 with consumption ya engine ya Cc1800.

Utunzaji tu...
 
Abs Master ya Brevis huwa inakufa mara kwa mara kwa sababu zipi?
 
Crown au brevis
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…