Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 - Nov 22, 2024

Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 - Nov 22, 2024

Muda huu mtaa wa Congo Kariakoo l uokoaji unawndelea.

Tuwaombee wnzetu wapone
===

Ghorofa moja katika Mtaa wa Congo na Mchikichi limeporomoka , hadi sasa hali ya majeruhi au vifo haifahamika lakini kwa mujibu wa mashuhuda kulikuwa na watu katika ghorofa hilo

View attachment 3153537

View attachment 3153536
View attachment 3153546
Inakera, ila hatujifunzi. Kuanzia viwango vya material, nondo, cement, ufundi na usimamizi. Baada ya tukio, je vifaa vya uokoaji vipo ? Kama havipo kwa nini?
 
kitaalamu hii ni sahihi kabisa katika response ya Majanga...huwezi kimbiza rasilimali zote at per kwenye eneo active la ajali ...unajuaje ajali nyingine inaweza kuendelea??Umejiridhisha vipi kama sio tukio "chambo" ili muingie kichwa kichwa ??
Tupunguze lawama pasipohitaji lawama.
Unaikumbuka Septemba 11 ??Jengo la kwanza limepigwa wote wakakimbilia pale halafu likapigwa na jengo la pili ...sasa baada ya hapo wahanga na waokoaji wote wakawa wahanga.

Kwa hiyo ndiyo maana wakaenda bila vifaa? Wewe vipi!
 
Kila siku maghorofa yanaota kama uyoga na hayazingatii ubora wa ujenzi.Huyu mama Abdul karuhusu uholela kufanyika nchini.Ajiuzulu Nchi imemshinda.
Ccm walitakiwa waweke PINGAMIZI JAMBO HILI au hawakujua lingetokea????
 
Inakera, ila hatujifunzi. Kuanzia viwango vya material, nondo, cement, ufundi na usimamizi. Baada ya tukio, je vifaa vya uokoaji vipo ? Kama havipo kwa nini?
Sio kuanzia viwango vya material bali hata Utaalam wa wale wanaojenga i.e kiwango cha Ufundi na Uzoefu. Mtu hajawahi kujenga ghorofa ila anauzoefu wa kujenga hizi nyumba za kawaida au mtu amehitimu Chuo kikuu ( Engineering..) lakini hana uzoefu wowote wa Field hata kidogo bali anauzoefu wa kujenga kwenye Kompyuta. :AYOOO: au kutumia AI programmes.
Wakati wa ujenzi mafundi,saidia fundi n.k. huvaa helmet.
 
Yeah. Hapo uliposema "weledi wa uokozi" ndiyo jambo la msingi sana.
Mtu hajakatazwa au kuzuiliwa kusaidia kutoa msaada wa kuokoa. Lakini huyo mtu anayetoa msaada wa uokozi kwamba yeye kwanza kama Mwokozi atakuwa Salama na yule Anayeokolewa pia atakuwa salama. Lengo litafanikiwa. Isiwe tu ni kazi ya kupangua matofali na kukata nondo kumbe kwa kufanya hivyo unasababisha mzigo mkubwa ushuke juu ya waathirika na kuwaponda, unaziba matundu yanayopitisha hewa kwa waathirika ndani ya kifusi au unagusa vitu vinavyoweza kusababisha moto kutokea n.k.
Ndio nilichomaanisha, huwezi kulazimisha polisi kuingia kwenye kazi isiyo taaluma yao na wakaharibu halafu mtawalaumu
 
Kuchelewa kutoa "Tamko la kufunga mtaa" kunaweza kweli ikawa ni Uzembe lakini pia Tamko lazima lipate idhini na Uwezeshaji. Mtaa haufungwi kama tunavyofunga gheto,nyumba, Bar au Kilabu ya taptap. Inatakiwa Polisi/walinzi wawepo hapo Kuhakikisha Utekelezaji sawasawa. Vinginevyo utakuwa umeukabidhi mtaa kwa vibaka.
Greda kuchukua muda kufika ni sahihi kabisa kwani huwezi kujua kama bado jengo linaendelea kuporomoka. Greda likiwepo hapo watu fyatu au hata walio timamu wanaweza kushinikiza greda lianze kazi halafu Mjengo ukashuka juu yake na wote greda +waathirika wakawa ni wahanga.
Inaonekana watu wengi hamzifahamu hizi machine na kazi zake. Grader inaenda kufanya kazi gani hapo?
 
Sio kuanzia viwango vya material bali hata Utaalam wa wale wanaojenga i.e kiwango cha Ufundi na Uzoefu. Mtu hajawahi kujenga ghorofa ila anauzoefu wa kujenga hizi nyumba za kawaida au mtu amehitimu Chuo kikuu ( Engineering..) lakini hana uzoefu wowote wa Field hata kidogo bali anauzoefu wa kujenga kwenye Kompyuta. :AYOOO: au kutumia AI programmes.
Wakati wa ujenzi mafundi,saidia fundi n.k. huvaa helmet.
Kinachotokea miaka hii wale wahandisi wanaoorodheshwa kwenye mabango ya site hawasimamii ubora, wengi wao wakilipwa wanawaachia mafundi Wenye uzoefu tu basi
 
Back
Top Bottom