Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 - Nov 22, 2024

Inakera, ila hatujifunzi. Kuanzia viwango vya material, nondo, cement, ufundi na usimamizi. Baada ya tukio, je vifaa vya uokoaji vipo ? Kama havipo kwa nini?
 

Kwa hiyo ndiyo maana wakaenda bila vifaa? Wewe vipi!
 
Kila siku maghorofa yanaota kama uyoga na hayazingatii ubora wa ujenzi.Huyu mama Abdul karuhusu uholela kufanyika nchini.Ajiuzulu Nchi imemshinda.
Ccm walitakiwa waweke PINGAMIZI JAMBO HILI au hawakujua lingetokea????
 
Inakera, ila hatujifunzi. Kuanzia viwango vya material, nondo, cement, ufundi na usimamizi. Baada ya tukio, je vifaa vya uokoaji vipo ? Kama havipo kwa nini?
Sio kuanzia viwango vya material bali hata Utaalam wa wale wanaojenga i.e kiwango cha Ufundi na Uzoefu. Mtu hajawahi kujenga ghorofa ila anauzoefu wa kujenga hizi nyumba za kawaida au mtu amehitimu Chuo kikuu ( Engineering..) lakini hana uzoefu wowote wa Field hata kidogo bali anauzoefu wa kujenga kwenye Kompyuta. au kutumia AI programmes.
Wakati wa ujenzi mafundi,saidia fundi n.k. huvaa helmet.
 
Ndio nilichomaanisha, huwezi kulazimisha polisi kuingia kwenye kazi isiyo taaluma yao na wakaharibu halafu mtawalaumu
 
Inaonekana watu wengi hamzifahamu hizi machine na kazi zake. Grader inaenda kufanya kazi gani hapo?
 
Kinachotokea miaka hii wale wahandisi wanaoorodheshwa kwenye mabango ya site hawasimamii ubora, wengi wao wakilipwa wanawaachia mafundi Wenye uzoefu tu basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…