Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 - Nov 22, 2024

Ndio nilichomaanisha, huwezi kulazimisha polisi kuingia kwenye kazi isiyo taaluma yao na wakaharibu halafu mtawalaumu
Uokoaji sasa hivi ni jeshi kabisa sio kikosi kama zamani. Linaitwa jeshi la zimamoto na uokoaji, je wana vifaa vya kufaa na kutosha kwa maafa ? Kama vifaa vipo je wana mafunzo ? Aliwahi kuzama mtu mmoja katika dimbwi la mvua, zimamoto walishindwa kumuopoa Hadi akatafutwa raia mtaalam wa kuopoa maiti waliozama tena bila vifaa.
 
Mnaweza kulaumu mafundi wa jengo kumbe tatizo wala halijatokana na ubora wa jengo bali taweza kuwa mzigo ulio wekwa juu ni mkubwa kulingana na uwezo wa jengo ,sasa hapo fundi anahusiaje
 
Absolutely.

Kiutaratibu site zenye shughuli za ujenzi ( aidha kujenga au kubomoa) huwa zinatakiwa kuwekewa uzio ( fence) ya 'hoarding,' sijui ni kwa nini kwenye hilo jengo hapakuwekwa huo utepe mwekundu au hoarding fence??
Tatizo watanzania tunapenda kufanya vitu kwa mazoweya japokua utaratibu unajulikana sema watu wengi hwapendi kuufuata,na rushwa ndiyo chanzo cha yote hayo!!
 
Hilo ni jingine kama la shule za kisasa bila ya walimu Wenye ujuzi stahiki
 
Mnaweza kulaumu mafundi wa jengo kumbe tatizo wala halijatokana na ubora wa jengo bali taweza kuwa mzigo ulio wekwa juu ni mkubwa kulingana na uwezo wa jengo ,sasa hapo fundi anahusiaje
Kama ni mzigo lazima fundi sana sana mtaalam, ahusike. Uimara na ukubwa wa vifaa lazima uzingatie idadi ya watumiaji. Mfano. huwezi kujenga chumba cha kuhudumia watu 50 ukajengea nondo mm ndogo kuokoa gharama za ujenzi. Au ratio ya mfuko mmoja mchanga 4 wewe unaweka 7 kuokoa gharama pia,, hapo unajenga kaburi sio jengo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…