Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 - Nov 22, 2024

Niaje wazee!
Huu uzi hauna mambo mengi ila ningependa tu kujuwa
Hivi kile kifusi walichokuwa wanakiondoa pale wameenda
Kukimwaga wapi!!!

Ova
 
Duh poleni...
Hili jengo lumeondoka na wengi
Nimeambiwa hata wale jamaa
Waliyokuwa na biashara ya mpesa tigo pesa kwenye jengo hilo wamengoka dah na walikuwa na mzigo kweri kweri

Ova
 
Poleni jamani.
 
Kwenye ajali ya Kariakoo iliyohusisha kuporomoka kwa jengo la biashara la ghorofa nne kisha kifusi kufunika mamia ya watu, huyu mama amepoteza wanae wawili. Mabinti warembo kutoka katika ardhi ya Mkoa wa Songwe huko Tunduma, ambao waliamua kuchagua njia sahihi ya upambanaji na si njia nyingine za mkato zinazifanywa na mabinti wengi.

Embu rejea kutazama sura yake💔 inaongea mengi, hapo alikuwa akimuaga mtoto wake aliyepatikana awamu ya kwanza asijue kama huyo mwingine yuko hai au amekufa. Na leo hii kama sio jana jioni amepokea taarifa kuwa hata yule binti yake mwingine amefariki huku mwili wake ukiwa umeharibika.

Wengi hatujui alikuwa na watoto wangapi, ukimtazama ni kama halii yuko kawaida, hicho ni kiwango cha maumivu cha levo ya juu, ukifikia kiwango hicho machozi huyaoni, na wakati mwingine unaweza ukaanza kucheka na wengine huishia kurukwa na akili. Naomba kwenye maombi yako ya kila siku usisahau kumjumuisha na huyu mama yetu mzuri, Mungu afanye wepesi juu yake jaribu hili liishe na limuache akiwa salama, Amin🙏🏽
 
Pole sana Kwa msiba huo mzito.yote haya kasababisa awamu ya sita kuruhusu ujenzi usiozingatia kanuni za ujenzi.Mama samie muuaji kabisa na anastahili kushitakiwa ICC
 
Mwili wa Brigita ambaye ni mdogo wa Marehemu Neema ambaye alikuwa miongoni mwa waliokuwa hawajulikani walipo baada ya ajali ya jengo kuporomoka Kariakoo umepatikana leo wakati zoezi la uondoaji vifusi likifanyika.

Kwa mujibu wa Izrael Mahenge, ambaye ni msemaji wa familia amesema maandalizi kwa ajili ya mazishi yanaendelea kwenye familia bado hakijajulikana kama atazikwa Dar es Salaam au watasafirisha.
 
Pumzika kwa amani dada,, inauma sana hasa unapoona kabisa haya yote yanatokea sababu ya baadhi tu wenye mamlaka kushindwa kusimamia majukumu yao,, ipo siku watalipa,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…