Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 - Nov 22, 2024

Your browser is not able to display this video.

Habari wanajamvi.
Kuna clip ina trend mitandaoni, kuna Jengo limeporomoka Kariakoo na kuna watu wamefukiwa na kifusi.

Haya ndiyo yale majengo yaliyojengwa fasta usiku na mchana bila viwango

Mliopo Kariakoo tupeni habari.
 
Kwani ukiambiwa waokoaji kinachokujia akilini ni gari la zimamoto!!?
KUtokana na aina ya ajali iliotokea waokoaji waje na vifaa vya kufukulia kifusi kama backhoe, excuvator nk.
Sijaongelea uokoaji hapo nimesema gari ya zimamoto soma vizuri uelewe tulichokuwa tunakiongelea
 
Wabongo sasaaaa
Kilamtu na kisimu chake anachukua video yan dah tumekuwa wajinga wa kupitiliza mahala pa msaada vieo tuu.
Aibu sana
Acha bangi... kijana.
Jeshi la uokoaji na zima moto lipo hapa.
Umeambiwa watu wamekaa na kushangaa....habari ni lazima ili tufahamu nini kinaendelea kwa wenzetu waliokwama.
 
Nmeona maaskari wenye mafunzo ya uokoaji wanajiham na kuogopa kutoa msaada, raia wasiokuwa na mafunzo ndiyo wanapambana, inasikitisha 😔
 
Ni hatari sana.

Tatizo kubwa zaidi lililopo Tanzania ni kwamba Hakuna mamlaka madhubuti za kudhibiti viwango na ubora wa Majengo pamoja na bidhaa zingine mbalimbali.
Watanzania tunaishi kwa nguvu ya Mungu tu peke yake.
Contractor's Registration Board (CRB) iwajibike. Siku ni kijiwe Cha wajanja tu! Majengo yatakuwa na ubora gani wakati Wale mameneja waadilifu walishaondokana Sasa wamebaki wapigaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…