Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 - Nov 22, 2024

Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 - Nov 22, 2024

Ajali bana!!

Hii mitaa kuanzia mida ya saa tatu usiku inakuwa Haina watu wachache sana,ila ghorofa limesubiri mida ya asubuhi alafu weekend ndiyo limeporomoka.

Unakuta wengine tulipanda nao magari asubuhi kuelekea mjini alafu wamefikiwa na umauti kwa kuangukiwa na ghrofa.

Kifo ni fumbo!!
Ghorofa litaanguka likipewa hekaheka na uzito. Watu kama hamna si linakuwa limetulia hakuna hata mtikisiko wa chini kabisa.
 
Tutarajie mengi zaid kuporomoka maana sio kwa kasi hii ya majengo yanayojengwa hapo kariakoo. Na kuna mdau humu alishaonya kuwa jamani haya majengo yanayojengwa kwa kasi hapa kariakoo je taratibu za kitaalam za ujenzi zinafuatwa?????
Nchi yetu inaharibiwa vibaya na rushwa,na uzembe,inaumiza sana !
 
Kamuone daktari kuna shida kichwani
Unakatwa na ngedere wanaokata umeme wa SGR.
Nafikiri mnamtafsiri vibaya huyu mtu, ukitafakari kwa kina Sana kuhusu hoja zake nafikiri unaweza ukamwelewa vizuri.
Kiini cha majanga haya ukichunguza kwa umakini Sana utagundua kwamba ni RUSHWA iliyotamalaki huko Serikalini. Hakuna mamlaka za Serikali ambazo ni competent kwa kushughulika au kusimamia kikamilifu suala la ubora na viwango vya majengo. Ajali kama hizi kwa hapa Tanzania mara nyingi Sana huwa zinasababishwa na uzembe wa makusudi wa watu, ajali hizi huwa hazitokani na 'kudra za Mungu.'
Tatizo ni RUSHWA na UZEMBE WA WATU.
 
Back
Top Bottom