Mwalimu wa tuisheni
JF-Expert Member
- Oct 19, 2019
- 6,602
- 10,801
😂😂😂 Kweli sijaona kila kitu kwenye hii duniaHuwa wengine wanapandishia juu ya nyumba ya kawaida, nyumba ya kawaida inabadilishwa kuwa ghorofa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😂😂😂 Kweli sijaona kila kitu kwenye hii duniaHuwa wengine wanapandishia juu ya nyumba ya kawaida, nyumba ya kawaida inabadilishwa kuwa ghorofa
Naona ilikua ya kipindi kile itakua mod wameuzima ila jana ulikua ni news kwa redSijauona huo uzi, mbona majanga kila kona
Majanga na kula bata kimeanza kipi mkuu ...Majanga yanatokea halafu kiongozi wa nchi anaenda kula bata. Shame
Akizungumza akiwa katika eneo la tukio lilipo anguka ghorofa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesemaJumapili Novemba 17, 2024, Saa 7:00 asubuhi: RC Chalamila - Hakuna aliyefariki kwa kukosa hewa, zoezi la uokoaji halikusimama
Akizungumza akiwa katika eneo la tukio lilipo anguka ghorofa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema "Kwa wale wachache waliopata madhara ya Kifo hadi sasa inavyoonekana walifariki kwenye tukio lenyewe, yaani wakati wa kudondoka [jengo] wamedondokewa na jiwe, au wamechomwa na nondo au namna nyingine. Lakini mpaka muda huu, waliokufa kwa suffocation bado hatujaipata taarifa hiyo, kwa hiyo ile ni taarifa [ya vifo] ya papo kwa hapo wakati tukio llinatokea. Niwaombe sana, tuendelee kushirikiana na hasa kurejesha confidence kwa watu ili madhara yake yasiweze kuwa makubwa zaidi."
Pia, ameongeza kuwa "Jana nilipita kwenye mitandao nikaona kwamba opereshi ya uokoaji imesitishwa. Ukweli ni kuwa operesheni ya uokoaji haijasitishwa. Jengo hili sasa hivi tunavyoongea karibu saa moja au saa moja kasoro, kuna watu tunaowasiliana nao na wapo chini kwa upande wa basement na tumeshawafikia kwa kuwapatia oxygen, maji na glucose. Tumewasihi waendelee kuwa wastahimilivu tunapoendelea kutumia akilli kubwa ili tusidhuru jengo zima na kuweza kuwadhuru wenzetu waliopo pale chini. Kwa tunaamini tumeshawapata wenzetu wachache na wanaendelea kuzungumza tunaamini pengine Mungu aatendelea kutuzaidia ili wenzetu waweze kutoka na wao wakiwa hai. Baadhi ya Wananchi wanasema mbona mnaenda taratibu sana, labda chini haina vifaa vya kusaidia, angalia kuna wheeloader, excavator lakini vifaa hivi hatujavitumia kwani jengo hili tunaogopa kulitikisa tunatumia njia nzuri tuweze kuwafikia wenzetu vizuri zaidi."
Saa 2:55 Usiku: Majeruhi 63 kati ya 70 waruhusiwa, 7 wanaendelea kupokea matibabu, uokozi bado unaendelea, zoezi halijasitishwa
Mpaka muda huu wamekwisha okolewa watu 70, ambapo wamepata matibabu katika hospitali ya Amana, Muhimbili na Mnazi mmoja, muhimbili walikuwa watu 40 ambapo 35 wameruhusiwa na 5 bado wanaendelea kupata matubabu, na katika hospitali hizo mbili wameruhusiwa wote na kubali watu 2, hivyo waliobaki wakiwa wanaendelea kupokea matibabu mpaka sasa, na waliofariki mpaka kufikia saa kumi na moja jioni kwa taarifa zilizothibitishwa na madaktari waliofariki ni 4.
=====
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amefika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuongea na majeruhi wa ajali ya ghorofa Kariakoo iliyotokea leo November 16,2024.
Saa 1:47 Jioni: Waziri Mkuu afika Hospitali ya Muhimbili kuwaona Majeruhi wa ajali, 33 waruhusiwa 7 bado wanatibiwa
View attachment 3153916
PM Majaliwa amesema taarifa iliyopo ni kwamba walikuwepo Wagonjwa 40 ambapo 33 wameruhusiwa na saba bado wanaendelea kupatiwa matibabu.
======
Saa 11:19 Jioni: ZIMAMOTO wasema atano wamefariki watu 42 tumewaokoaKamanda wa Mkoa wa Kizimamoto Kinondoni ambaye ndio Kamanda oparesheni wa tukio la kuanguka kwa ghorofa Kariakoo leo November 16,2024, Mrakibu Peter Mtui, amesema hadi kufikia sasa Watu watano wamefariki na wengine 42 wameokolewa kutokana na tukio hilo.
Akiongea akiwa eneo la tukio leo amesema "Zoezi la maokozi linaendelea tangu tupate taarifa saa tatu asubuhi, mpaka sasa hivi Watu 42 wameokolewa na walipoteza maisha ni watano"
====
Saa 9: 05 Mchana: Waziri Mkuu afika eneo la Tukio Kariakoo, aagiza Oksijeni kupelekwa chiniWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewasili Kariakoo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujionea hali ya uokoaji inavyoendelea katika jengo la ghorofa liliporomoka leo Jumamosi Novemba 16, 2024 asubuhi.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewatoa hofu na kuwahakikishia Watanzania na Wanajamii ya Kariakoo kwamba kazi kubwa ya uokoaji inaendelea ili kuwaokoa Watu waliofukiwa baada ya jengo kuporomoka Kariakoo ambapo amesema juhudi za kupeleka oksijeni chini zinafanyika ili wapate hewa safi.
Akiongea na Wananchi baada ya kukagua zoezi la uokoaji leo PM Majaliwa amesema ““Mh. Rais anatoa pole sana kwa Ndugu wa Familia ambazo ni Waathirika wa tukio hili, Wafanyabiashara wengi ambao biashara zenu zipo kwenye jengo na zimeangukiwa na jengo hili pamoja Jumuiya yote ya Kariakoo, pokeeni salamu hizi za pole kutoka kwa Rais na Serikali kwa ujumla, tunajua wakati kazi inaendelea na nimeenda kuona Makamanda wetu wa uokoaji wanaendelea tumeona tuwaache waendelee”
“Lugha nzuri ya sasa ni kuwahakikishia Watanzania na Wanajamii ya Kariakoo kwamba kazi kubwa ya uokoaji inaendelea, Vyombo vya Ulinzi vyote vipo hapa, Wizara mbalimbali zipo hapa, tuombe Mungu wanaookolewa wawe hai, nimeona Mtu ametoka anasema wenzangu wapo chini kwahiyo tuhakikishe hatutumii nguvu bali tunatumia akili ili kuwaokoa kule chini, jitihada za kuwapelekea oksjeni kule chini zinaendelea ili watoe wakiwa hai”
=====
Nimesikitika kupokea taarifa ya ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika Kata ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.
Saa 6:44 Mchana: Rais Samia atoa pole kwa waathirika Kariakoo
Nimeuagiza Uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, na Idara ya Menejimenti ya Maafa kufanya kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi.
Wakati hilo likiendelea na tukimuomba Mwenyezi Mungu awape pona ya haraka majeruhi, tuwaombee pia utulivu na subra ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wenzetu wanaotafuta riziki zao katika eneo hili muhimu kibiashara nchini ambao kwa namna mbalimbali wameathiriwa na ajali hii."
=====
Saa Muda huu mtaa wa Congo Kariakoo uokoaji unaendelea.
Tuwaombee wenzetu wapone
Ghorofa moja katika Mtaa wa Congo na Mchikichi limeporomoka , hadi sasa hali ya majeruhi au vifo haifahamika lakini kwa mujibu wa mashuhuda kulikuwa na watu katika ghorofa hilo
View attachment 3153537
View attachment 3153536
View attachment 3153546
View attachment 3153816
UPDATES
PIA SOMA
- Rais Samia atoa pole kwa waathirika Kariakoo. Aagiza kufanywa kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi
- ZIMAMOTO: Watano wamefariki, zaidi ya watu 40 wameokolewa ajali ya ghorofa Kariakoo
- Waziri Mkuu Majaliwa awasili lilipoporomoka jengo Kariakoo, uokoaji waendelea
- Ghorofa laendelea kushuka, zoezi la uokoaji lasimama, mwananchi watawanywa
- Sauti za waliofukiwa na Ghorofa Kariakoo: "Tuko hai lakini tunateseka, tusaidieni tutakufa"
Kwahiyo bata ni muhimu kuliko walipa kodi?Majanga na kula bata kimeanza kipi mkuu ...
Pale Zenji, zile ghorofa za mji mkongwe kila siku zinarekebishwa ndani kwa ndani, mbaya zaidi nyingine zinafanywa kuwekwa partition kwa ndani... So kama ilikuwa na kuta za kutenganisha vyumba.. kuta zinabomolewa na kujengwa style nyingine kwa ndani ili tu wapate vyumba vingi na kufanya apartment... sasa sijui kama haina madhara hii😂😂😂 Kweli sijaona kila kitu kwenye hii dunia
Daaah hapo nimekuelewa mkuuKwahiyo bata ni muhimu kuliko walipa kodi?
Kuwafikia na kuwatoa ni jambo jingine. Kufukiwa na kifusi kama hiko si rahis kumtoa mtuHiyo ni kauli ambayo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ameitoa asubuhi hii kupitia vyombo vya habari akiwa Kariakoo.
My take: Kwanini uwadanganye watu? Kama mmewafikia wahanga mkaweza kuwapa hivyo vitu sasa mnafanya tena jitihada zipi kuwafikia ili kuwaokoa? Si mngewachukua muondoke nao kama mmeweza kuwafikia?
Hii serikali ya Samia sijui kwanini hawataki kujisahihisha na kurudi kwenye mstari!
Sehemu ambayo mtungi wa gesi unapenya? Acheni siasa rahisi na uongo uongoMkuu sio imepatikana nafasi ya kupitisha hayo mahitaji na sio watu?
Simkubali Chalamila ila hoja yako haina mashiko.