Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 - Nov 22, 2024

Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 - Nov 22, 2024

Nikafikiri Niffer ni Mkuu wa mkoa ama mkurugenzi flani, nime google sijaona, mwenye kujua huyu afisa ni kitendo gani anitag!
Watu washaanza kujichomeka
Kuchangisha wabongo bana 😄
Alafu walivyokuwa watu wajibga wanatumaaa

Ova
 
50/50 wanayodai wanawake haionekani kariakoo. Mwanaume apewe heshima yake Mungu sio mwanadamu kumfanya mwanaume kichwa (ukuu) na moyo wa ubaba
Uongozi, ajira, kurithi mali uko kote midomo mirefu wanataka 50/50 anachofanya mwanaume na mwanamke anaweza. Haya jengo limeanguka tutoe kifusi tuingie basement kuokoa watu, wanahamisha goli
 
Uongozi, ajira, kurithi mali uko kote midomo mirefu wanataka 50/50 anachofanya mwanaume na mwanamke anaweza. Haya jengo limeanguka tutoe kifusi tuingie basement kuokoa watu, wanahamisha goli
APo sasa ndo wanapo feli,men atabak kua men tu na si woman
 
Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema idadi ya waliopoteza maisha katika ajali ya kuanguka kwa jengo la ghorofa eneo la kariakoo nchini imefikia 16.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wananchi kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam, alipokuwa akiongoza shughuli ya kuaga miili ya waliopoteza maisha.

Amesema athari ya kuanguka kwa ghorofa ni pamoja na kuharibika kwa mali nyingi, majeruhi wengi na mbaya zaidi ni vifo, ambapo amesema mpaka sasa waliookolewa wakiwa hai wamefikia watu 86.

Majeruhi walifikishwa kwenye hospitali mbalimbali za jijini na wengi wao wameruhusiwa huku watano wakiwa chini ya uangalizi wa karibu.

''Kutokana na athari hizi serikali imeendelea kuchukua hatua kunusuru maisha ya wenzetu ambapo shughuli za uokoaji zinaendelea''

''Kazi hiyo isisimame, usiku na mchana mpaka tuhakikishe mtu wa mwisho anaokolewa'' alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Serikali imesema inaendelea kugharamia matibabu kwa walioathirika, kwa kutoa mahitaji na gharama za mazishi kwa marehemu wote.

Waziri mkuu Majliwa amesema serikali itafanya uchunguzi maalumu kujua chanzo cha ajali na kumsaka mmiliki wa jengo ili kuisaidia polisi kwenye uchunguzi.

Imeunda tume ya watu 19 ili kuyapitia majengo yote ya maghorofa ili kujua ubora wa majengo na kuishauri serikali nini ifanye baada ya uchunguzi.
 
Daah sibezi kamati kuundwa ila naskitika kuundwa baada ya maafa.
Tuwe na desturi ya kuchukua tahadhari mapema hasa kwa Organ za kiserikali
Zilishaundwa nyingi lakini mwisho wa siku zinafungiwa kwenye makabati tu!
 
Dah hivi watu huwa Mnawaza nini lakini 🤣🤣🙌🙌🙌
Serikali imefeli pakubwa! Ghorofa 4 ndiyo mpaka leo siku ya 4?

Bora raia walivyofanya kazi wenyewe walifanya kazi kubwa kuliko hivi vitengo vya uokoaji!

Sioni chochote wanachokifanya!

Raia huwa tunapigiana sana wenyewe kwenye majanga kuliko serikali inavyotupigania.

Hii serikali yetu imejaa ufala sana!
 
Ikiwa kuna watu hawajaokolewa hadi Leo hii watakuwa bado hai kweli ?
 
Back
Top Bottom