Mwanzo wa matatizo mengine ni kujitakia tu kwa kuweka kila kitu kwenye social media;
Umepata tu mtoto huyooo ushapost, mwingine anahangaika miaka kusaka mtoto, kwanini usirogwe mtoto afe au awe wa kuugua tu hata usimfurahie!
Umefanyiwa tu engagement huyoo ushapost (she said yes), mwingine hajawahi hata kusikia neno ndoa toka kwa mpenz wake karne inakata sasa, kwanini wasikuombee mabaya muachane!
Umenunua tu ndinga huyooo ushapost, mwingine miaka ananyunda tu kwa mguu hata baiskeli hana, kwanini usiombewe mabaya upate ajali.
Umenunua tu kakiatu huyooo ushapost picha ya miguu, mwingine hakumbuki hata alinunua lini kiatu kipya, kwanini tusitamani ujikwae na kiatu kichanike!
Umekula tu vizuri huyooo ushapost, mwingine hana uhakika hata kama kesho atakula, kwanini tusikuombee tu na wewe ukose kesho!
NB:SIO KILA MTU ANAPENDA MAFANIKIO YA MTU, AU KUONA FULANI ANAFURAHA, TUNACHEKEANA TU USONI ILA MOYONI TUSHACHIMBIANA KABURI LA FUTI MIA SIO SITA TENA, MARAFIKI NAO NI KAMA UYOGA TU, LEO MBOGA KESHO SUMU.
TUWEKE VITU PRIVATE UKIMSHUKURU MUNGU INATOSHA ANASIKIA SIO MPAKA UTAFUTE MABAYA KWA LAZIMA.