Kupoteza Ubinafsi Halisi: Persona na Wazazi

Kupoteza Ubinafsi Halisi: Persona na Wazazi

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
Tunazaliwa tukiwa ‘sisi.’ Orijino. Hatuogopi kukosea. Hatuogopi kupenda. Hatudanganyi. Hatuumizi. Tunadadisi. Tunafikiri. Tunauliza. Tunatafuta majibu.

Hata hivyo, imani kuwa ni salama kuwa ‘sisi’ halisi iko mikononi mwa watu wazima tunaoishi nao. Hawa, kwa wengi wetu, ni wazazi tunaowategemea.

Utegemezi huu kwa wazazi unajenga matarajio fulani ambayo wakati mwingine ni tofauti na uhalisia wetu. Taratibu tunaanza kujifunza tabia tusizomaanisha. Tunaanza kujitetea. Tunaanza kuridhisha. Tunaanza kudanganya. Tunadanganya kupata upendo. Tunaigiza kukubaliwa. Tunapoteza ‘usisi’. Tunatengeneza persona —sura inayokubalika na watu.

Persona, kwa nadharia ya Carl Jung, ni ule mkusanyiko wa matarajio ya nje, makatazo, maonyo, maelekezo, yanayotulazimisha kuachana na ile sura halisi tuliyonayo lakini tunayojua haipokelewi. Unaanza kudanganya kwa nia nzuri —kukidhi matarajio.
‘Nani kavunja kikombe?’ anauliza mama kwa hasira. Unajua ni wewe.
‘Sio mimi mama!’ Persona imekuchochea kudanganya. Ndani unatamani umridhishe mama. Lakini huwezi kumridhisha kwa kuwa ‘wewe’.
‘Nifanye nini kueleweka na mama ninayehitaji upendo wake, ukaribu naye na tabasamu lake?’
‘Nikisema ninachotaka atakasirika. Nikisema ninavyojisikia atanielekeza namna ya kujisikia!’

Najifunza kuigiza. Ndani naumia. Nje natabasamu. Tabia inaanza kuongozwa na msukumo wa nje. Namtengeneza ‘Mimi’ wa mama halafu nabaki na ‘Mimi’ mwingine ninayemjua mwenyewe.
 
Back
Top Bottom