kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,634
- 7,015
Nimeshangazwa na uongozi wa timu ya Simba kunyamazia suala la wao kushutumiwa kupulizia dawa kwenye chumba walichopangiwa Dodoma FC hapo jana.Hii ni ishara ya dharau ya wazi kwa wachezaji wa Simba,kwamba hawawezi kushinda bila kutumia "makando kando" kama msemaji wa yanga anavyopenda kusema.
Kutokana na shutuma hizo kujirudia rudia,nimeanza kuwa na wasi wasi kuwa,huu ni mpango ulioratibiwa vizuri na upande wa pili.Wamewekeza vilivyo kwenye propaganda ya soka kiasi cha kuwaaminisha wapenzi wao kuwa,wao ni bora sana kuliko timu yoyote hapa nchini.Wameweza kuwatumia mamluki wao walio kila sehemu.Kuanzia waandishi wa habari,walinzi wa uwanja,na waajiriwa kwenye timu nyingine.
Nauliza tu hawa madaktari feki wanasema kwenye vyumba kuna dawa,ni dawa aina gani?
Maana wasitudanganye kuwa wao wanajua zipo na kumbe ni utopolo tu.
Au kuna dawa za kiasili ambazo hazijulikani kisayansi?Maana dawa zinazojulikana kisayansi ukiisema tu utakosa ushahidi kwa kuwa ni rahisi kuthibitisha.
Mi nawaomba Simba,wachukue hatua kuanzia waandishi walioamua kusambaza taarifa hizi kishabiki bila ushahidi,na uongozi wa uwanja utueleze ni kwa nini wanaruhusu haya mambo kuwa sehemu ya michezo.Kwani nina uhakika hawachafui brand ya Simba tu,Bali hata kuharibu taswira ya nchi.