Hili suala linaongelewa tu kama utani utani hivi ila ukijaribu kuona uhalisia unaweza kubaini kwamba kuna uwezekano pakawa na ukweli. Nimekuwa nikiangalia uchezaji Wa wapinzani Wa Simba kipindi cha pili hasa kwenye zile mechi ngumu kwa Simba Mara nyingi wapinzani huoekana wamechoka sana na wakati huo Simba wanakuwa wana nguvu sana. Tukitazma program za mazoezi za Simba hazina cha ajabu cha kuwafanya wawe ni timu ya kuongeza nguvu Na kumaliza dakika 90 kwa kishindo kuliko kipindi cha kwanza. Kuna namna!