Kupunguza kero ya Watumishi kuhama, Serikali ingefanya yafuatayo kwa faida ya wote

Kupunguza kero ya Watumishi kuhama, Serikali ingefanya yafuatayo kwa faida ya wote

Pantomath

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2019
Posts
842
Reaction score
3,449
Tuliona ajira za afya mwishoni mwa 2024, Pia Tumeona ajira za walimu zimetoka kwa baadhi ya mikoa mfano Dar, Moro, Pwani n.k na utaratibu ni ule ule, wanakupanga popote, sio ulipoombea wala ulipo,

Kwa nini Kabla ya kutoa post za allocation za vituo kwa ajira mpya, mfano wanajua Dar, Shinyanga, Kigoma n.k kunahitajika manesi, madactari, wenye taaluma flani(meno, ngozi, CO, MD kadhaa) au kwa upande wa walimu wanajua kabisa mikoa hio inahitaji walimu kadhaa wa masomo mf Physics, English, Kiswahili n.k

Basi kwa idadi ile ile ya aina ya taaluma katika afya au masomo husika kwa walimu, wangeruhusu wafanyakazi waliokaa kazini muda mrefu kwenda kujaza hayo ma gap, halafu wale wapya waende mikoa wanayotoka wakongwe, nao wakiwa wanasubiri miaka miatatu ikifika wanafanya exchange kwa njia hio hio?..

Ingekua kweli wanampanga muombaji anapohitaji, hii ingekua ngumu(uonevu), lakini naye unakuta wanampanga asipotaka..

Lakini pia kitu kingine naona kinawezekana ni hiki..

Ajiara mpya post zikiwa zinatoka wangekua kwenye mkeka wanaweka namba za simu, wanatoa chance kwa mtu anayetaka kubadilishana na mwenzake haraka kwa taaluma/masomo husika na level ya elimu kabla ya kwenda kuthibitishwa wanapatana wenyewe wanamalizana,

HIi itaokoa sanaa usumbufu.

Naandika hivi maana inatokea sana, Wewe upo Tanga (MD, Nurse /Physics & Math), unapelekwa kigoma, na wa kigoma(MD, Nurse /Physics & Math) analetwa Tanga, unaona kabisa kwenye mkeka, unatamani unaishia kusema mimi si ningekua huyu.

Matokeo yake wote wanaanza tena kurupushani za kuhama zinatopunguza utendaji.
 
Nahìsi serikali inataka makabila yote yachanganyike ili kuleta utaifa zaidi. Kila mtu akifanya kazi alikozaliwa baada ya muda mrefu Italeta anguko la utaifa. Mimi nakubaliana na uhamisho wa wanandoa hawa ndio wakae pamoja lakini kama mtu ni single asiogope kufanya kazi popote. Binafsi hadi namaliza shahada ya kwanza sikuwahi kutoka nje ya DSM yaani nilikuwa sijawahi kufika hata chalinze. Siku ya kwanza kutoka DSM kwenda kuripoti kwa mwajiri mkoan nilipata stress ya kufa mtu. Nashukuru Mungu hadi sasa nimefanya kazi mikoa kumi na moja.
 
Back
Top Bottom