Kupunguza wafanyakazi kwa kutoa notice of termination ya siku 30 lakini hakukuwepo na consultation wala notice for intention of retrenchment

jeremiamnzava

Member
Joined
Jul 10, 2024
Posts
12
Reaction score
20
Habari wadau,

Ninafanya kazi shirika fulani tukapewa likizo ya siku 28, siku ya moja kabla ya kurudi kazini nikapewa notice of termination ya siku 30, ikieleza shirika husika linapitia financial difficult na wanafanya wanafanya collaboration na shirika lingine.

Kwa hiyo nitafanya kazi kipindi cha notice.

Ila mimi nimestukizwa na sikupewa notice of intentions of retrenchment, wala hakukuwa na consultation, sikuitwa wala hatukujadili chochote zaid ya kapewa tu notice of termination.

Naomba msaada wenu kisheria imekaaje hapo au haki yangu ni ipi?

Mifano ya case zilizofanyika zitasaidia pia.
 
Kwa anayejua Mambo ya sheria, haki yangu naipataje hapo na muda gan napaswa kwenda CMA nisubirie muda wa notice of termination uishe yan baada ya tarehe 30 July au niende kabla?
 
Kitu Cha kwanza unatakiwa uwende ukazungumze na muajiri ujue kwa sababu gani umekuwa retreached na kama mwajiri wako hajakupatia sababu za msingi za kukufanyia retrenchment for instance notice, na malipo unayostahili unaweza kuandika barua kwa mwajiri ukielezea haki unazodai after then kama mwajiri hajatoa majibu ya kuridhisha au hatoshughulika na malalamiko Yako bhas utapeleka malalamiko Yako CMA ni muhimu vitu vyote hvyo kufanyika ndani ya siku 30 hivyo usisubiri hzo cku zikaisha
 
Asante kwa ushauri wako. Niliwaandikia email nikiwataka kwanza wanilipe mshahara wa mwezi wa sita ambao nilikuwa likizo ili iweze kunisaidia kufanya kazi kwenye hicho kipindi cha notice, lkn hawajanijibu ikabidi tu nijitahidi hivyo hivyo kwenda kazin kuendelea kufanya kazi kwa huo mwezi waliosema. Boss naskia hatak kuonana na mm. Hali naona inazidi kuwa ngumu sijaitwa kujadili kuhusu hatma yangu zaid ya notice of termination inayosema my employment will end after 30 day due to financial constraint and operation requirements na kwenye huo mwezi natakiwa kumalizia report na kurudisha vifaa vya ofisi.
 
Kwanza mkataba wako unasemaje? Jifanye sasa wewe umepata kazi sehemu nyingine let's say unatakiwa uanze August 1 ungefanyaje? Je ungeanza kujadiliana nae kabla ya kuandika notice? (Haya ni maswali ya kutafakari)

Anyway, back to hoja yako, mwajiri yupo sahihi kukupa notice ya mwezi mmoja na Kwa vyovyote vile ipo indicated kwenye mkataba wako (kama hakuna hayo ni mengine tena though Bado atakuwa sahihi tu Kwa kuwa amekupa notice in advance ili ujiandae). In most cases, kwenye taasisi nyingi huwa kuna options 3 yaani kufukuza staff kama amefanya kosa kubwa, kupewa notice ya mwezi mmoja au kupewa notice ya masaa 24 lakini pia anatakiwa akulipe mshahara wa mwezi mmoja na kama hukuwahi kwenda likizo atakulipa zile siku 28 watazipigia calculation.

Na ukitaka wewe staff kuondoka, nawe unatakiwa uandike notice ya mwezi mmoja, au notice ya masaa 24 ila utamlipa mwajiri wako au kama hukuwa hujaenda likizo au kuna siku za likizo zimebaki, utaandika notice ya mwezi mmoja ila siku zako za likizo zinakuwa sehemu ya huo mwezi hivyo unaweza ukaandika Leo Ijumaa ukasepa zako Jumatatu though notice ya siku 30 itakuwa inasoma kuanzia Jumatatu mpaka hapo zitakapoishia (ndio maana nikakuuliza ingekuwa wewe ungefanyaje)

All in all, check policy za shirika lako na mkataba unasemaje alafu uongee na mwajiri wako kumwonyesha mwajiri maeneo ambayo amekiuka na usiporidhika nenda kwenye maamlaka za serikali
 
Pole Sana,ila kuna hatua za kufuata pale ambapo mwajiri anataka kupunguza wafanyakazi/retrenchment na hiyo notice uliyopewa ni suala LA mwisho kabisa baada ya mchakato wote wa kupunguza wafanyakazi.
1: Una aina gani ya Mkataba wa Kazi/Ajira
2: Je,ulipewa notisi ya retrenchment wakati uko likizo au ukiwa umesharudi kazini??
3.Je,kuna vyama vya wafanyakazi katika sehemu unayofanya kazi??
4.Je,Tangazo LA awali LA nia ya Mwajiri kupunguza wafanyakazi lilitolewa?Kama lilitolewa ulikuwa kazini au likizo??
5.Je,ni vingezo vipi vilikubaliana Kati ya Wafanyakazi/Vyama vya Wafanyakazi na Mwajiri vitatumika katika kupunguza wafanyakazi?
Kiujumla retrenchment/kupunguza wafanyakazi siyo jambo jepesi hivyo,na taratibu zake siyo kama termination za kawaida,hivyo siyo jukumu lako kuanza kuwasiliana na Mwajiri kwa ajili ya stahiki zako ni Jukumu LA Mwajiri,na Kama uliyoeleza hapo juu yalifanywa na Mwajiri wako aise kuna makosa mengi sana ambayo.
Hivyo kabla ya kusubiri kuwa retrenched sheria inakutaka Kama HUJARIDHIA/DISPUTE katika sababu zilizotolewa na Mwajiri kufungua kesi CMA kuchallenge retrenchment na taratibu zote za kupunguza wafanyakazi zitasimamishwa hadi kesi uliyifungua kufikia tamati,japo asilimia kubwa huwa tunasubiri hadi upewa retrenchment Letter.
Pia ni vyema kabla mapema umtafute Wakili/Mtaalamu wa Sheria za Kazi kwa miongozo na taratibu zaidi,na ukipenda karibu PM tufanye kazi
 
Habari wadau,

Ninafanya kazi shirika fulani tukapewa likizo ya siku 28, siku ya moja kabla ya kurudi kazini nikapewa notice of termination ya siku 30, ikieleza shirika husika linapitia financial difficult na wanafanya wanafanya collaboration na shirika lingine
. Sheria za Kazi haziruhusu notice for termination or retrenchment kutolewa kwa mfanyakazi wakati akiwa likizo

Hiyo ni redundancy, wana ground ya financial crisis. Else wise, umejiunga na chama chochote cha wafanyakazi. Go to them.
Unajua Waaajiri wengi huwa na Valid and solid substantive grounds for the retrenchment of the employees lakini Procedural issues huwa ni changamoto Sana,na mistake ndogo tu katika retrenchment inaweza kupelekea kulipa compensation ambazo ni hasara kubwa Sana kwa Mwajiri,ndio maana muda mwingi Mimi huwa nashauri Mteja wangu(Waajiri/Kampuni) turesort katika Termination of contract by Agreement.
Technically: Retrenchment imekuwa designed for Permanent contracts employees( Kama uko katika fixed contract na imekuwa retrenched aise ni kesi nzuri Sana ya kutokea)
Na other termination forms : kwa Forms zingine za contract of employment
 
Una grounds za redundancy ( termination on operational requirements au retrenchment) kwamba bosi wake hayupo sahihi?
Msaidie hapo.
Au unaniruhusu nimpe grounds kwanini imekua hivo.
Na hana compensation kwa grounds zake hadi sasa.
 
Grounds ziko sahihi,lakini procedural issues nafikiri haziko sawa ndio maana juu kabisa kuna maswali nimeuliza ili angalau wadau wawese kujua kipi cha kushauri kuliko kufanya speculations.
Compensation: ziko za kutosha hapo
Una grounds za redundancy ( termination on operational requirements au retrenchment) kwamba bosi wake hayupo sahihi?
Msaidie hapo.
Au unaniruhusu nimpe grounds kwanini imekua hivo.
Na hana compensation kwa grounds zake hadi sasa.
 
Kwanza mkataba wako unasemaje? Jifanye sasa wewe umepata kazi sehemu nyingine let's say unatakiwa uanze August 1 ungefanyaje? Je ungeanza kujadiliana nae kabla ya kuandika notice? (Haya ni maswali ya kutafakari)

Anyway, back to hoja yako, mwajiri yupo sahihi kukupa notice ya mwezi mmoja na Kwa vyovyote vile ipo indicated kwenye mkataba wako (kama hakuna hayo ni mengine tena though Bado atakuwa sahihi tu Kwa kuwa amekupa notice in advance ili ujiandae). In most cases, kwenye taasisi nyingi huwa kuna options 3 yaani kufukuza staff kama amefanya kosa kubwa, kupewa notice ya mwezi mmoja au kupewa notice ya masaa 24 lakini pia anatakiwa akulipe mshahara wa mwezi mmoja na kama hukuwahi kwenda likizo atakulipa zile siku 28 watazipigia calculation.

Na ukitaka wewe staff kuondoka, nawe unatakiwa uandike notice ya mwezi mmoja, au notice ya masaa 24 ila utamlipa mwajiri wako au kama hukuwa hujaenda likizo au kuna siku za likizo zimebaki, utaandika notice ya mwezi mmoja ila siku zako za likizo zinakuwa sehemu ya huo mwezi hivyo unaweza ukaandika Leo Ijumaa ukasepa zako Jumatatu though notice ya siku 30 itakuwa inasoma kuanzia Jumatatu mpaka hapo zitakapoishia (ndio maana nikakuuliza ingekuwa wewe ungefanyaje)

All in all, check policy za shirika lako na mkataba unasemaje alafu uongee na mwajiri wako kumwonyesha mwajiri maeneo ambayo amekiuka na usiporidhika nenda kwenye maamlaka za serikali
Naendelea kupata somo hapa JFs.
Ujuzi huu ipo siku nitamsaidia mtu mwengine.
 
Back
Top Bottom