Kura mtandaoni kuamua muundo wa serikali

Kura mtandaoni kuamua muundo wa serikali

Serikalit 4; 1>Muungano,2>Tanganyika, 3>Unguja na 4>Serikali ya watu wa Pemba
 
serikali moja tuu ndo wananchi wakawaida tutanufaika sana huku kwenda zenji kwa passport na ukuchukua gari zenji ukifika bandarini ulipie ushuru kama kwamba umetoka nalo moja kwa moja Dubai mimi siungi mkono. nataka serikali moja tuuuu.
 
Serikali ya Tanganyika + Ya Mapinduzi ya Zanzibar + ya Shirikisho ya Tanzania =3
 
Kwa vile tulikubali kuungana na kupoteza hadhi ya mataifa yetu ya Awali tangu 1964 mf. Tanganyika kuwa kama nchi, solution ya kweli ktk hili na kuujenga zaidi muungano ni SERIKALI MOJA TU. Tatizo Wazanzibar kwa muda wote huo wamekuwa na hadhi kama nchi lakini hawaridhiki. Zaidi hapo Muungano utakufa kihoro kimnyakimnya.
 
Serikali ya Zanz wana katiba,muungano kuna katiba lakn Tanganyika ?,sasa warudishe katiba ya Tanganyika.hivyo serikali ni 3
 
Zanzibar ni serikali kamili, Tanzania ni serikali ya muungano sasa turudishiwe Tanganyika yetu. serikali tatu
 
Hivi mlikua wapi wakati wa kuchukua maoni mkawaachia waamue wenyewe sa mnalalamika nini? Acha ipite tu Serikali tatu
 
Serikali 3 ndiyo mpango mzima ingawa CCM haitapitisha katika kikao kijacho cha Bunge
 
Huwezi kukwepa serikali kali tatu kama tuna taka usawa na haki kwa kila mtanzania serikali tatu iwepo
 
Back
Top Bottom