Kura ya maoni ACT - Wazalendo kuamua Serikali ya Umoja

Kura ya maoni ACT - Wazalendo kuamua Serikali ya Umoja

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama cha ACT-Wazalendo Zanzibar, Salum Bimani, amesema viongozi wa chama hicho wanafanya vikao na Wanachama wake katika majimbo ya Unguja na Pemba kufikia uamuzi wa endapo kishiriki kwenye Serikali ya Umoja.

“Chama bado kinaendelea na vikao vyake kuhusu msimamo wake wa kuingia katika serikali au laa.” alisema.

Bimani aliyasema hayo, huku taarifa za zisizo rasmi zikieleza kwamba mchakato huo umekamilika na kazi kubwa inayofanyika hivi sasa ni kufanya uchambuzi wa maoni ya wanachama na kuangalia faida za kuingia katika serikali hiyo na hasara zake.
 
Finally baada ya sarakasi zote hizo wataunga juhudi na Wala siyo kwa interest ya wanachama wao Bali matumbo ya Viongozi Wachache.

Wewe jiulize tu kura za Maoni za Nini Kama msimamo wenu bado nikuto utambua uchaguzi uliofanyika?
Hapo tayari washaunga juhudi sema wapo kutafuta justification tu ya kuhalalisha njaa zao.

#Njaa Ni mbaya Sana

#Tanzania hakuna upinzani.
 
Dunia hadaa ulimwengu shujaa!
1456109.jpg
 
Hivi mwaka 2015 walifanya huu mchakato kabla ya kuamua kususa? Hii ni technique ya kubuy time na ni suala la muda mfupi kabla hawajiunga na Serikali ya Dr. Mwinyi

Siasa ni ajira na ajira ni pesa!
 
Ni jambo jema kupata baraka za wanachama na viongozi kabla ya kufanya uamuzi kama huo.

Amandla...
 
Finally baada ya sarakasi zote hizo wataunga juhudi na Wala siyo kwa interest ya wanachama wao Bali matumbo ya Viongozi Wachache....
Mkuu, unaona uchungu wakithamni matumbo yao
 
Wanatafuta huruma za wanachama inaitwa danganya toto
 
Hilo nalo ni jambo la kupiga ramli!!! Wanachama wa ivi vyama viwili washageuzwa misukule.
Yani viongozi wanajaribu kutengeneza mazingira "tumekubali lakini Kwa mbinde"
 
Back
Top Bottom