Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
One government alongside majimbo system
26 Regions plus the semi autonomous Zanzibar as the 'majimbos'
Plus one overall national government
 
Zibaki mbili kwani umeambiwa zikiwa tatu kutakuwa Na mabadiliko wanasiasa wanaopigia kampeni suala hili ninawasiwasi nao wengi ni majambaz waliovaa suti watanzania tuweni macho kuna shetani anataka kuvuruga hii nchi
 
nini faida ya kuvunja muungano na nini faida ya kuuacha muungano.. ikiwa tayari wanzanzibari wameshazaa na watanganyika naikiwa muungano wa inchi utavunjwa vipi kuhusu hizi familia zilizo ungana nazo zitavunjwa...



Hapo ndo unapoweza kuona madhara ya mbio za Mwenge kwenye akili za watu.Wazanzibar na Watanganyika waliooana hawakuoana kwa sababu ya Serikali.
Historia yetu ndio ilitifanya tuwe jamii moja.
Mbona kuna wapemba wengi sana wameolewa kule Uarabuni?
Tuliungana lini na Omani au Kuweit.Wahindi waliotapakaa mikoa yote ya Tanzania ni lini tuliungana na India.
Kama CCM wanapenda Muungano basi uwe wa Serikali Moja mana huo ndio imara kabisa.Hizi mbili za matatizo ambayo mvumbuzi hajulikani ni ubabaishaji mtupu.
Serikali tatu ndio zilizoko kwenye rasimu nitashangaa kuona serikali mbili zilizikataliwa na wengi zikijadiliwa kwani nazo zilipata maoni machache zaidi.
 
Nataka tanganyika yetu, wapemba waende kwao, unguja nao kwao tubaki na TANGANYIKA YETU
 
WanaJF Kwa mda mrefu sasa kuelekea utungaji wa katiba mpya kumekuwa na mjadala mkali kuhusu muungano wetu uwe wa muundo upi sasa ningependekeza tuwe na kura ya maoni hapa JF kuhusu muundo wa muungano, upi ni muundo sahihi?

1.Serikali moja.
2. Serikali mbili.
3.Serikali tatu.


N:B ukiweza kutoa sababu za muundo wa muungano unaoutaka itakuwa vizuri zaidi

serikali mbili 7bu serikali 3 itajenga Utaifa umimi kwa sasa wabongo wanaish huku wanaish kiubaguz je kukiwa 3?
 
Tangu kuanza kwa mjadala wa maoni kuhusu Rasmu ya Katiba Mpya ya Tanzania, kuhusiana na kipengele cha Muundo wa Serikali ya Muungano, watu wote wamekuwa wakitoa maoni ya kuwa na Serikali MBILI AU TATU. Sijawahi kuona hata mtu mmoja aliyewahi kutoa hoja ya kuwa na muundo wa Serikali Moja! Kama wapo waliyowahi kutoa maoni ya kuwa na muundo wa Serikali moja, naomba wanisamehe maana sijabahatika kuyaona. Nashindwa kuelewa kama mtizamo huu wa kufikiria Muundo wa Serikali ya Muungano wa Tanzania ni lazima uwe ama wa serikali mbili au tatu ni mtizamo wa bahati mbaya ama ni wa makusudi kwa lengo maalum.

Mazingira ya historia ya utendaji kiserikali katika awamu ya kwanza ya Muungano wetu huonyesha mfumo wa Serikali moja iliyokuwa na matawi makuu mawili -Tanzania Visiwani na Tanzania Bara. Hebu tuangalie kwa ufupi mazingira hayo ni yapi:

  • [*=1]Muungano ulipewa jina jipya MUUNGANO WA TANZANIA kuchukuwa nafasi ya jina la zamani MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR.

    [*=1]Baada ya kutolewa jina jipya nchi yote na sehemu zake mbili(Tanganyika na Zanzibar) ilitambulika kwa jina hilo jipya - TANZANIA; na sehemu zake kuu (tuseme nchi washirika) zilitambulishwa kwa majina ya TANZANIA BARA NA TANZANIA VISIWANI (siyo kwa majina ya Tanzania Tanganyika na Tanzania Zanzibar. Hii ilikuwa lengo la fikra za utaifa wa nchi washirika (watanganyika na wazanzibar) na kujenga utaifa wa Muungano (WATANZANIA)

    [*=1]Muundo wa Serikali ulionyesha kiutendaji kuwa SERIKALI MOJA, japo kwa maneno ilitamkwa kuwa Serikali mbili. Kwanza, Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Muungano alikuwa Rais ambaye alikuwa na mamlaka ya kusimamia mambo yote ya Muungano pamoja na mambo yote yaliyohusu Tanzania Bara. Mtendaji Mkuu huyo (Rais) alikuwa na wasaidizi wakuu wawili mmoja kwa kila upande wa Muungano, ambao walijulikana kwa jina (title) la MAKAMU WA RAIS. Upande wa Tanzania Visiwani alikuwapo Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye alikuwa pia Makamu wa kwanza wa Rais, AKIMWAKILISHA Rais kusimamia shughuli za Serikali kwa Mambo ya Muungano na AKIMSAIDIA kusimamia mambo ambayo yalikuwa yanahusu Tanzania Visiwani ambayo hayakuwa ya Muungano. Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alitenda kazi zake za kusimamia yote ambayo hayakuwa ya Muungano katika Tanzania Visiwani chini ya mwamvuli wa Serikali ya Muungano, akitumia bendera ya Muungano na Wimbo wa Taifa wa Muungano, n.k. Kwa upande wa Tanzania Bara alikuwapo Waziri Mkuu ambaye alikuwa pia Makamu wa Pili wa Rais, akimsaidia Rais kusimamia mambo yote ya Muungano na mambo yote yaliyohusu Tanzania Bara. Pili, Rais wa Muungano alikuwa na mamlaka kamili ya kikatiba kugawa Tanzania Visiwani na Tanzania Bara katika majimbo ya utawala (mikoa na wilaya) na kuwateua wakuu wa majimbo (huu ni ushahidi tosha kuthibitisha kwamba Muundo wa awali ulikuwa wa Serikali moja ya Muungano).

    [*=1]Mazingira hayo, niliyoyaelezea hapo juu, yanaonyesha wazi kwamba kiutendaji Tanzania ilikuwa na Muundo wa Serikali moja japo kwa maneo ilitamkwa kuwa Muundo wa Seikali Mbili.

Sasa tuangalie kwa ufupi kwa nini haikutamkwa wazi kwamba Tanzania iliongozwa chini ya mfumo wa Serikali moja, badala yake ikawa inatamkwa kwamba ulikuwa Muundo wa Serikali Mbili. Lengo na dhamira (kama nionavyo mimi, na nadhani kimantiki ndivyo ilivyokuwa, siyo kwamba nawasemea Waasisi wa Muungano) ilikuwa kuunda nchi moja yenye serikali moja. La kuunda nchi moja liliwezekana na kutekelezwa, lakini la kuunda Serikali moja ya wazi ilionekana haukuwa muda muafaka. Haikuwa muafaka wakati huo kutangaza muundo wa Serikali moja kwa sababu serikali za nchi washirika (Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar) zilikuwa zinatofautiana kwa vipengele vikuu viwili -moja (ya Tanzania Bara) ilikuwa imepatikana kwa njia za demokrasia na iliendeshwa kwa misingi ya kidemokrasia, na nyingine (ya Tanzania Visiwani) ilikuwa imepatikana kwa Mapinduzi (tena Mapinduzi yakiwa bado motomoto - umri wa miezi mitatu) na ilikuwa inaendeshwa kwa misingi ya kimapinduzi. Baraza la Maapinduzi lilikuwa limepiga marufuku shughuli zote za kisiasa Tanzania Visiwani kwa miaka 50 (ambayo ina maana wakati huu tunaposherehekea miaka 50 ya Muungano ndiyo Tanzania Visiwani wangekuwa wanafikiria kuanzisha shughuli za kisiasa huko). Nidhahiri kwamba katika mazingira hayo isingekuwa rahisi kuvunja Serikali ya Mapinduzi na kusimika serikali ya moja kwa moja ya kidemokrasia ya Muungano.

Kutokana na mazingira hayo, ilionekana ni busara kwa Waasisi wa Muungano kuanza na Muundo wa Serikali (kivuli) mbili kuelekea katika muundo wa serikali moja kadiri joto la vuguvugu la mapinduzi lilivyokuwa linapungua. Kwa mantiki hiyo hatua za kuongeza mambo ya Muunganoo hatua kwa hatua hazikuwa za bahati mbaya au za lengo la kuimeza Zanzibar bali zilikuwa zinalenga kutimiza lengo halisi la Muungano - kuwa na nchi moja na Serikali moja.

Kulingana na hoja hii ya kihistoria ninashauri wale wote waliojikita katika malumbano ya muundo wa serikali mbili au tatu walegeze misimamo yao ili watafakari hoja ya kuwa na Serikali moja kwa awamu hii ya pili ya miaka 50 ijayo. Kama tukiunda Serikali moja utaratibu wa zamani wa kuwa na Rais anayesaidiwa na makamu wawili utarejeshwa. Vilevile chini ya mfumo huo Wizara zote zitakuwa za Muungano zikiwa na matawi katika pande mbili za Muungano yakisimamiwa na manaibu mawaziri. Chini ya utaratibu wa Serikali moja hakuna atakayeona anapunjika katika kutawala nchi maana koti la Serikali litakuwa limevaliwa na pande zote za Muungano; na pia hakuna atakayelalamika kwamba anamezwa maana wote watakuwa na dhana ya UMOJA NI NGUVU. Muundo huo pia utakuwa unaendana na wakati maana dunia yote sasa inaimba wimbo wa MPANGO WA DUNIA MPYA (New World Order) ambao lengo lake ni kuifanya dunia kuwa kijiji cha serikali moja, uchumi mmoja na, ikiwezekana, dini moja. SISi kutaka muungano uwe wa serikali mbili au tatu tunaelekea dunia ipi?



Lt Col Makongoro I. Mongáteko (rtd)

 
Lt Col,

Kama unafahamu historia na siasa za Zanzibar, serikali moja Tanzania kamwe haitawezekana kwa sababu wenzetu huko wataona ni kama tunaimeza Zanzibar na kuifanya mkoa wakati kihistoria Zanzibar na Tanganyika zimeingia katika muungano kama nchi sawa.

Wanaweza kukuambia ukitaka serikali moja basi iwe "Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar" na Tanganyika nzima iwe mikoa ya Zanzibar kimsingi. Kama watu wa bara wasivyoweza kukubali hilo ndivyo watu wa Zanzibar wasivyoweza kukubali serikali moja itakayovunja waliyo nayo sasa.

Suala hili, from a practical point of view, ndilo lililomfanya Mwalimu Nyerere akubali kuwa na serikali mbili Tanzania.

Ndiyo maana husikii watu kuzungumzia sana serikali moja, si kitu chenye a realistic chance of happenning, even as we can debate the theoretical side of it.
 
Wazanzibar hawataki nchi moja serikali moja na ma ccm ya bara yameshindwa kuwashawishi wenzao wa visiwani juu ya hilo
 
Serikali moja ndiyo The Best Option. Kwani inatudanya kuwa wamoja kabisa.

Ila sina uhakika kama Zanzibar wanaweza kukubali option hii.
Kama hawakubaliani nayo sirikali tatu ndiyo option inayofuata.
 
Serikali moja ndiyo The Best Option. Kwani inatudanya kuwa wamoja kabisa.

Ila sina uhakika kama Zanzibar wanaweza kukubali option hii.
Kama hawakubaliani nayo sirikali tatu ndiyo option inayofuata.

#Okinawa .. Zanzibar ni nchi kutokana na katiba yao ya mwaka 2010 which means hawaezi kukubali Serikali moja wala mbili na wanachoshinikiza ni muungano wa mkataba au Serikali tatu ili nayo pia iwe na mamlaka kamili katika masuala ya utawala na umiliki wa rasilimali.
 
WanaJF Kwa mda mrefu sasa kuelekea utungaji wa katiba mpya kumekuwa na mjadala mkali kuhusu muungano wetu uwe wa muundo upi sasa ningependekeza tuwe na kura ya maoni hapa JF kuhusu muundo wa muungano, upi ni muundo sahihi?

1.Serikali moja.
2. Serikali mbili.
3.Serikali tatu.


N:B ukiweza kutoa sababu za muundo wa muungano unaoutaka itakuwa vizuri zaidi

Serikali tatu
 
serikali 1 hawezekani,maana ZNZ wanakatiba,ukitaka serikali 1 labda uufute katiba ya ZNZ ambayo inabidi utumie nguvu ambayo italeta mauji,ili kuwe na amani serikali 3,kwa kutengeneza katiba ya Tanganyika.kwa hiyo Serikali 3 ndio haki ya kulinda muungano.
 
Serikali moja hapa kamwe haitawezekana maana Zanzibar kila mmoja hapa anafaham walipofikia mpk sasa. Serikali tatu italeta utengano mkubwa zaidi maana hata Wazanzibar wenyewe wataanza kuzozana kuhusu yupi alishiriki zaidi ktk mapinduzi ama sababu nyinginezo kisha nao watatengana vilevile Pemba kivyao na Unguja kivyao.
Suluhusho ni serikali mbili ambayo inadumisha umoja na mshikamano km ilivyooneshwa ktk katiba ya sasa pia itawahakikishia Wazanzibar juu ya ardhi yao na nchi yao.
 
Back
Top Bottom