Binafsi napenda Selikali Tatu,
Kwasababu zifuatazo
Faida.
1. Itafufua nchi yetu iliyozikwa kwa miaka 50 sasa ambayo ni Tanganyika na kuibua hisia za utaifa za kukipenda chetu.
2. itaondoa ukivitimba na ufisadi kwani kutakuwa na Institution kubwa ambayo ni selikali ya Muungano ambayo itasimamia utendaji wa Selikali za nchi washirika.
3. Itasaidia Transparency katika matumizi ya selikali za nchi washirika hivyo kuongeza mapato na pia kupunguza gharama zisizo za lazima kama ifanyikavyo sasa hivi.
4. Italeta maendeleo ya haraka kwa nchi washirika kwani nchi sasa itaweza kupanua wigo wa ukusanywaji wa kodi hivyo kungeza pato la taifa, ambalo litasaidia katika kuleta maendeleo mbalimbali, katika Elimu, Afya nakadhalika
5. Tutatengeneza usawa katika kuichangia selikali kuu, maanayake Zanziba kwa Asilimia yake na Tanganyika ka Asilimia zake.
6. Tutajibu maswali ya Muungano kwani kila nchi itajua mambo yapi ya kimuungani na yapi si ya muungano hivyo kuleta ufanisi katika kuyafanyia kazi.
7. Sisi wananchi tutjua kla kinacho endelea kwani kutakuwa na uwazi na uwajibikaji,
8. Free and fair Elections.
Kuhusu Hasara ake mimi sioni kama kuna hasara yoyote tutakayo ipata.
Kuhusu Miundo mingine itatupeleka kubaya kwani Sasahivi watu wameuchoka Muungano kivuli.