Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
Wanasiasa wanipigania hio serikar tatu hasa wa CHADEMA
Wanajua wakikosa kubamba tanzania bas wata bam.ba tanganyika bt itakuwa very costfull kwa wananch

VIONGOZ HASA CHADEMA ACHEN KUTAFUTA MAMLAKA KWA NJIA HIO ANGALIEN MTAIPELEKA NCH WAPI
 
Naunga mapendekezo ya Tume ya Warioba la sivyo kama tumeungana kikwelikweli tuwe na serikali moja, Unguja iwe mkoa na Pemba iwe mkoa.

Point...!! Asante sana kwa kutoa wazo Bora kwani Maana halisi ya Muungano ni kuwa kitu kimoja.. Mm naamini serikali moja ndio dawa Pemba mkoa na unguja mkoa pia..
 
mi naona tukiruhusu muundo wa serikali 3 vitu vitapanda bei zaidi ya hapa maana hiyo serikali ya tatu uchumi wake itakuwa inategemea Tanganyika na Zanzibar na pia tutakua 2na fanya chaguzi tatu. je, hiyo pesa za uchaguzi zitatoka wapi ya hiyo serikali ya tatu kama sio kutegemea bajeti za tanganyika na zanzibar? je vitega uchumi vya hiyo serikali ya tatu vitatoka wpi? tuwe makini ndugu zangu hawa wanasiasa wapo kimasilahi zaidi
 
Kwa kuzingatia hali ya uchumi wa nchj yetu.. serikali 3 ni mzigo.. platinum Fubu"
 
Last edited by a moderator:
HUU MUUNGANO SI HALALI,LAKINI TUMEKWENDA NAO KIMABAVU,UKWELI SASA UMEDHIRI,HATI ZA MUUNGANO FEKI,SAINI ZIMEGHUSHIWA,WARIOBA AMEONESHA NJIA YA KUPATA MUWAFAKA CCM WANAIKATAA,UNAJUWA SASA MUANGANO UNAO TUFAA NI WA MKATABA,KILA MTU NA NCHI YAKE ,KISHA TUKUBAIANE MAMBO MAALUMU KUSHIRIKIANA MFANO SOUTH AFRICA NA NAMIBIA .WAO WANSHIRIKIANA USHURU WA FORODHA,FREE WORKING PERMIT KWA RAI WAO,NA PESA ZAO ZINAINGILIANA,YAANI NAMIBIAN INATUMIA sa RAND NAPIA NAMIBIAN $ .LAKINI KILA NCHI IKO HURU .
HUU NDIO MWISHO WA MUUNGANO KAMA HAKUNA MUWAFAKA SAINI YA KARUME  KWENYE HATI FEKI YA MUUNGANO.jpg
 
Kila mfumo unategemea mazingira husika.. hivyo kama wengine walifanikiwa kwa mfumo wa S3, si lazima na sisi tufanye hivyo.. "situational analysis" ndiyo ya kuzingatia na siyo wengine walifanya nini..
 
Wacha kuleta propaganda za uongo hizo na chuki za kidini waraabu gani wenye shida na ardhi? Mbona husemi wazungu na wao ndio walokua wakoloni kila pahala duniani hata hao waarabu walikuwepo tu picha nguvu zote zilikua ktk mikono ya wazungu na sasa hivi ni nani aneniingia ktk nchi za wengine akajifa ya yy ni Mungu wa dunia? America hamna asojua mbona hamumtaji? Au hii ndo muendelezo wa chuki dhidi ya Uislam? Bcos uarabu unafungamana na uislam lkn wazungu waliodhahiri wanaofanya fisadi hawatajwi bcos dinimnalingana? Huu ni uchochezi wacheni hayo !
 
Tatu 👍mbili zimefeli kwa nn zinanganganiwa? Tugande hapohapo tu? Tunahitaji mabadiliko hio hoja ya gharama ni hoja dhaifu haina mashiko ishatolewa maelezo ya kutosha
 
Mkuu wengi tunakuunga mkono lakini kumbuka wabunge wengi ni wa CCM na wanataka serikali mbili hapa tutafanyaje wakati asilimia kubwa ya waTanzania tuko nje ya Bunge?
Mkuu, wabunge hawa sio kweli wanataka serikali mbili ila wanalazimishwa na viongozi wao wenye uchu wa kuona nchi hii inaingia kwenye machafuko.
 
Ndugu Admin naomba unisupport na hii post yangu, nataka kuangalia tu, wangapi wanapenda

A) Selikali Tatu kumaanisha Tanganyika, Zanzibar na Selikali kuu yaani Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania.
B) Selikali Mbili yaani Ya Mapinduzi ya Zanzibar na Selikali Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania.
C) Selikali Moja, yaani Selikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania.
D) Ama Selikali mbili yaani Selikali ya Tanganyika na Selikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Pia Weka na Sababu zako ziki critisize selikali zingine kwa kuonesha Faisa na hasara ya selikali hizo unazo zipinga, ili na sisi tujue faida na hasara za aina fulani ya Muungano na kwanini tuupende Muundo wa selikali hiyo utakayo ichagua.
Pia tuweze kufahamu kinacho fichika kati ya UKAWA na Wanao isupport Selikali ya sasa yaani CCM.
 
Binafsi napenda Selikali Tatu,
Kwasababu zifuatazo
Faida.
1. Itafufua nchi yetu iliyozikwa kwa miaka 50 sasa ambayo ni Tanganyika na kuibua hisia za utaifa za kukipenda chetu.
2. itaondoa ukivitimba na ufisadi kwani kutakuwa na Institution kubwa ambayo ni selikali ya Muungano ambayo itasimamia utendaji wa Selikali za nchi washirika.
3. Itasaidia Transparency katika matumizi ya selikali za nchi washirika hivyo kuongeza mapato na pia kupunguza gharama zisizo za lazima kama ifanyikavyo sasa hivi.
4. Italeta maendeleo ya haraka kwa nchi washirika kwani nchi sasa itaweza kupanua wigo wa ukusanywaji wa kodi hivyo kungeza pato la taifa, ambalo litasaidia katika kuleta maendeleo mbalimbali, katika Elimu, Afya nakadhalika
5. Tutatengeneza usawa katika kuichangia selikali kuu, maanayake Zanziba kwa Asilimia yake na Tanganyika ka Asilimia zake.
6. Tutajibu maswali ya Muungano kwani kila nchi itajua mambo yapi ya kimuungani na yapi si ya muungano hivyo kuleta ufanisi katika kuyafanyia kazi.
7. Sisi wananchi tutjua kla kinacho endelea kwani kutakuwa na uwazi na uwajibikaji,
8. Free and fair Elections.

Kuhusu Hasara ake mimi sioni kama kuna hasara yoyote tutakayo ipata.

Kuhusu Miundo mingine itatupeleka kubaya kwani Sasahivi watu wameuchoka Muungano kivuli.
 
Muungano ni marithiano kati ya mataifa au nchi mbili zenye tamaduni zinazoshabihiana.Na muungano unatakiwa uwe na haki kwa pande zote mbili kusiwe na mmoja kuchukua madaraka ya mwingine.

Sidhani kama wananchi kwa hakika wanajali serikali mbili,moja au tatu,nadhani wananchi tunahitaji maendeleo na uchumi uliokua siyo kwenye makaratasi bali uonekane kwenye jamii ya watanzania.

Wananchi wanachukizwa na viongozi walioko madarakani ambao wako very busy kujilimbikizia mali,kuuza raslimali za taifa,maliasili zetu ,matumizi mabaya ya fedha za umma,hakuna uwajibikaji,uadilifu wala uwazi.Rushwa ndiyo imekuwa haki siku hizi,hauwezi kupata haki yako kisheria,afya,elimu na hata ajira bila kutoa rushwa.

Ufisadi umefika mahala pake kiasi kwamba ufisadi umekuwa haki badala ya dhambi,madawa ya kulevya ndiyo usiseme,sasa haya ndiyo yaliyotakiwa kuundiwa tume kujadiliwa ni namna gani viongozi au wafanyabiashara au wafanyakazi kwenye sekata za umma wanaweza kuwajibishwa ili kurejesha maendeleo na hadhi ya utaifa.

Ninauhakika haya ndiyo wananchi tunayoyahitaji na si serikali mbili au tatu.
 
Muungano imara na madhubuti ni wa serikali 3. Serikali ya tanganyika, serikali ya zanzibar, na kisha serikali ya muungano! Nje ya hapo ni maigizo matupu!
 
Serikali tatu ndio suluhisho kwa sababu;
1. Serikali 2 zilizopo zimeshindwa kutatua kero za muungano kwa miaka yooote.
2. Serikali 3 zitaleta usawa kwa nchi washirika wote tofauti na sasa hakuna usawa kati ya Zanzibar na serikali ya kufikirika ambayo ipo ndani ya JMT.
3. Serikali 3 zitaleta uwajibikaji kwa viongozi wote kuanzia wa JMT na viongozi wa wa serikali washirika.
Ngoja nipige kura halafu niendelee.
 
Binafsi napenda Selikali Tatu,
Kwasababu zifuatazo
Faida.
1. Itafufua nchi yetu iliyozikwa kwa miaka 50 sasa ambayo ni Tanganyika na kuibua hisia za utaifa za kukipenda chetu.
2. itaondoa ukivitimba na ufisadi kwani kutakuwa na Institution kubwa ambayo ni selikali ya Muungano ambayo itasimamia utendaji wa Selikali za nchi washirika.
3. Itasaidia Transparency katika matumizi ya selikali za nchi washirika hivyo kuongeza mapato na pia kupunguza gharama zisizo za lazima kama ifanyikavyo sasa hivi.
4. Italeta maendeleo ya haraka kwa nchi washirika kwani nchi sasa itaweza kupanua wigo wa ukusanywaji wa kodi hivyo kungeza pato la taifa, ambalo litasaidia katika kuleta maendeleo mbalimbali, katika Elimu, Afya nakadhalika
5. Tutatengeneza usawa katika kuichangia selikali kuu, maanayake Zanziba kwa Asilimia yake na Tanganyika ka Asilimia zake.
6. Tutajibu maswali ya Muungano kwani kila nchi itajua mambo yapi ya kimuungani na yapi si ya muungano hivyo kuleta ufanisi katika kuyafanyia kazi.
7. Sisi wananchi tutjua kla kinacho endelea kwani kutakuwa na uwazi na uwajibikaji,
8. Free and fair Elections.

Kuhusu Hasara ake mimi sioni kama kuna hasara yoyote tutakayo ipata.

Kuhusu Miundo mingine itatupeleka kubaya kwani Sasahivi watu wameuchoka Muungano kivuli.

Nakubaliana 100%
 
Back
Top Bottom