Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
mkulu tuna mifumo mibovu ukiwemo na muundo wa selikali, hao ma judge/mahakimu nani kawaajiri? nani anawalipa mishahara?wanafanya kazi kwenye ofisi za nani? tunahitaji mfumo wa uongozi utakaosimamia hayo, huu mfumo tulionao umeshindwa!
 

Kwani hata huo muungano, nani aliulilia kuwa tuungane? Kwani kunamwananchi aliwahi kupendekeza serikali 2 wakati inaanzishwa?
 

Serikali3 kama ilivyopendekezwa, kwa kuwa njia pekee yenye kudumisha Muungano bila ya manung'uniko kutoka kwa nchu Washirika.
 
Hivi Moderator wa Jamii forum unaweka poll ambayo mtu hata Kiswahili kinampiga chenga? badilisheni basi hiyo "selikali" na iwe kwa Kiswahili serikali.

Hiki ni kioo cha Mtanzania na tukienzi Kiswahili tusikifanyie mizaha ya kijinga namna hii.

cc, Paw, PainKiller, Invisible
 
Kinadharia ningependelea serikali moja, ila kutokana na hali halisi iliyopo sasa hivi, serikali tatu ndio suluhusho na hiyo inawezekana kutekelezeka.

Mimi sina Shida na idadi ya Serikali Kama Kweli Serikali hizo....
1. Zitadumisha Muungano.
2. Zitapunguza mzigo wa uendeshaji na ustawi aw jamii
3. Zitaleta Umoja, Amani, utulivu na Mshikamano tuliokuwa nao

Naunga mkono Serikali mbili kwa sababu siwaamini viongozi wanaopigania Serikali tatu. Mimi niko Zanzibar Najua CUF mtazamo wao wa awali ulikuwa ni Serikali ya MKATABA.... Walipofika bungeni wakaungani na CUF kudai Serikali tatu. Ulishawahi kusikia Watoto wanauliza Cheti cha Ndoa cha wazazi wao? Halafu wana onyesha wanasema sahihinsiyo zenyewe.... Kwa nini? Hawa wote Muungano kwao ni kero... CHADEMA kwenye sera Yao wanataka MAJIMBO...Sasa MKATABA + MAJIMBO = ???????? Ndani ya CHADEMA yenyewe unaona hata kabla hawajatawala Hali ya UMAJIMBO inaonekana.... Yuko wapi ZITO KABWE? Vyama Vya Upinzani vingi tutake tusitake ni Kama taasisi za Watu binafsi.... Hakuna demokrasia ndani ya vyama Hivyo.... Bungeni wakekimbia... Mtaniambia wanatetea maoni ya wengi... Wengi wangapi? Kama mko wengi si mngoje Kura ya maoni? Kama mna uhakika mtashinda kwenye Kura ya maoni.... Mbona mmeweka Mpira kwapani?
 

Kwa kuwa wewe ni kama hao wanaojiita Tanzania kwanza na yawezekana ni mmoja wao, nisaidie hili. Mie najua vema kiswahili tena kile sanifu, pia nilifuatilia BMK kwa siku zote. Wanaojiita wengi pamoja na Kikwete alipokuwa akihutubia uvccm tarehe 25, juzi tu, analalamika kuwa kuna watu bungeni wamewatukana baba wa Taifa na Mzee Karume. Je ni matusi yapi hayo? Nijipu kwa kuwanukuu kama kweli wewe uliyasikia hayo matisi.
 

nakubaliana nawe kuwa S1 ndio suluhisho lkn hili haliwezekani kabisaaa wewe umeshawahi kumsikia kiongozi yoyote wa ccm anajaribu kuongelea hii kitu serikali moja? haiwekezani.. sory haiwezekani kabsaa ukileta S1 zanzibar haitakuwepo na hii nikitu ambacho hakiwezi kukubaliwa na wazenj. hivyo basi ili kieleweke ni muundo wa serikali 3 ndio tutapata muafaka na ndio utakuwa mwisho wa wasanii ccm
 

rekebisha hii kauli yako. wapi cuf waliungana na cuf
Najua CUF mtazamo wao wa awali ulikuwa ni Serikali ya MKATABA.... Walipofika bungeni wakaungani na CUF kudai Serikali tatu
 
Kuimarisha muungano ni kwa serikali tatu. yaani:
1. SERIKALI YA MUUNGANO. NDIO ITAKUWA NA RAIS WA NCHI
2. SERIKALI YA TANGANYIKA ITAONGOZWA NA MAKAMU/AU WAZIRI MKUU BARA NA NDIE ATAKUWA MKUU WA HIYO SERIKALI
3.SERIKALI YA ZANZIBAR ITAONGOZWA NA MAKAMU/AU WAZIRI MKUU ZANZIBAR NA NDIE ATAKUWA MKUU WA HIYO SERIKALI, HAWA WOTE WATAWAJIBIKA KWA RAIS AMBAE NDIE MKUU WA NCHI.
KAMA HUTAKI HIVI BASI KAVUNJE MUUNGANO WAKO NA HIYO SERIKALI 2.
 
Wameamua kumuenzi baba wa taifa kwa kuweka kila alichoanzisha kwenye jumba la makumbusho. Azimio la Arusha, Ujamaa na KUJITEGEMEA, huduma za afya na elimu BURE vyote vipo makumbusho sasa huu muungano upo njiani kwenda huko na njia pekee na sahihi ya kuufikisha huko ni muundo huu wa serikali mbili tu.
 

Muungano utakaodumu ni wa Serikali 2 tu, basi! Huo wa "Serikali 3/Nchi 3" utakuwa legelege, tegemezi na egemezi!
 
Muungano utakaodumu ni wa Serikali 2 tu, basi! Huo wa "Serikali 3/Nchi 3" utakuwa legelege, tegemezi na egemezi!

yaaani wewe ndo hujitambui kabisaaa... we angalia hizo kura tu hapo juu zinavosomeka zinakujulisha hiyo serikali yako ya wezi(ccm) inayotaka ibaki serikali 2 ilivyododa, acha u-mburura weyee
 

kumbe mibazazi miburula mpo wengieee!!! subirini kiama chenu chaja!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…