Unapo ungana/kuunganisha kitu maana yake ni kwamba unazalisha kitu ama unakiunganisha kwa kuwa kimoja ama kukizalishia kingine kilicho imara zaidi.
Tunajua kabla ya muungano nchi hizi zilikuwa mbili zenye madaraka kamili kwa kila upande. Baada ya kuungana zililenga kujenga nguvu ya pamoja iliyo thabiti na kuifanya isikike kikamilifu bila kupoteza uhuru/mamlaka ya kila moja wapo. Na kama hili ndilo ni vigumu kuunganisha sehemu ndogo ambayo ni sawa na 1/8 na sehemu ya pili yake yenye ukubwa 7/8 ili kupata kitu kimoja kwa kutegemea usawa. Hapa lazima mmoja ambaye ni mdogo {kieneo}atakuwa amemezwa na mkubwa{kieneo}.
Na huwezi kusema kwamba uendeleze serikali mbili ktk kuungana huko ukauita kuwa ni muungano ulio sahihi. Kwa kuwa mtakuwa mmeungana kuna mambo mengi yaliyokuwa yakisimamiwa na serikali washirika yatapaswa kuendeshwa na serikali ya muungano ambayo hiyo iwe isiwe lazima isimamiye upande mwingine wa muungano{nchi} kwa asilimia mia moja. Hili linapo tokea linainyima sifa ya kuwa serikali ya muungano kwa kujigeuza mtawala kamili wa upande mmoja wa muungano na wakati huohuo ikijipenyeza kusimamia upande wa pili wenye serikali yake na kuyasimamia bahadhi ya mambo kwa kivuli cha muungano.
Hili linapotokea ni sawa na nchi {ndogo}mwanachama wa muungano kujiweka ktk madaraka ya nchi nyingine{mwanachama wa pili wa muungano} kiutawala.Ambapo itahitaji idhini yake ktk mambo yake mhimu ili iweze kuyatenda na ikikataliwa na serikali hiyo inayo jiita ya muungano ndiyo basi tena. Hapa kwa kifupi tunaweza kusema inatawaliwa na sehemu yenye kuiongoza serikali ya muungano. Bila kificho hapa mhanga ni Zanzibar kwa kuwa hata siku moja kwa katiba tuliyo nayo serikali ya mapinduzi ya zanzibar haitakaa iwe serikali ya Jamhuri ya muungano. Labda Watanganyika watawaliwe na mzanzibar kama ilivyo wahi kutokea chini ya mwamvuri wa serikali ya jamhuri ya muungano.
Ili kuondoa makandokando hayo ni vyema zikaundwa serikali tatu ambazo kila pande zitakuwa na serikali yake kwa kusimamia mambo yatakayo kuwa yameainishwa kikatiba na kusimamiwa na serikali moja ambayo itakuwa juu ya hizi serikali mbili,ikibeba na kuratibu majukumu yote mazito ya kitaifa na kimataifa kwa mjibu wa katiba itakavyo kuwa ikielekeza. Na hii ndiyo itakayo kuwa ikiongozwa na rais na hizo mbili viongozi wake si lazima wawe marais ili kuondoa mkanganyiko wa idadi ya marais ndani ya nchi moja. Hawa tunaweza kuwaita mawaziri wa kuu.
''kwa mtizamo huu nilionao,ningependelea kuona tunakuwa na serikali tatu kwa ajili ya ustawi wa taifa letu''.