Serikali moja ndo mpango. Huwezi kuunganisha vitu viwili ukapata vitatu.
Ukiunganisha viwili lazima upate kimoja.
Wanaotaka serikali 2 ni waroho wj madaraka wanataka waendelee kuhodhi mfumo mzima wa utawala.
Na wanaotaka serikali 3 ni zaidi ya waroho kwan wana tamaa ya fisi, wanaamini njia hiyo ndo itakayowanusulu kupata nafasi za kutawala ilihali wakiwa njiani kuelekea kuuvunja muungano.
MUUNGANO NI KITU CHA KHERI, LAKINI SIO KITU CHA LAZIMA.
Kosa kubwa walilolifanya waasi ni kuwapeleka watu kwenye muungano pasipo kuwauliza kama wanautaka muungano ama hawautaki.
Na kosa hilohilo wameendelea kulifanya watawala wa sasa kwa kutaka kutengeneza katiba mpya pasipo kuanza kuwauliza wananchi kama wanataka muungano ama hawautaki.
Jibu lingekua ndiyo, hapo moja kwa moja ungeundwa muundo wa serikali moja,taifa moja na nchi moja.
Wala tusingeulizana tunataka serikali ngapi tena. Zaidi hata ubabe ungetumika kuunda muundo serikali moja kwa sababu tiyari wananchi wameshahiyari wanataka MUUNGANO.
Jibu lingekua hapana, tungeachana kila mtu akashka hamsini zake na wale wazanzibar waishio bara na kufanya biashara tungewapa uraia kwa anayetaka na asiyetaka akarudi nchi yake ya asili na akawa anakuja tanganyika kama mwekezaji ama mtalii.
Mwishowe tukabaki kushirikiana na kuishi kama majirani mema huku tukishuhudia wanavyokatana mapanga waunguja na wapemba kama tulivyoshuhudia wauwaji ya kimbari ya 1994 kule kwa majirani zetu ambao ilikua ni sehemu ya tanganyika kabla ya mwaka 1920 Rwanda na Burundi.
Tungepokea wakimbizi na tukaendelea kuzifaidi ajira za UN kupitia UNHCR na kutafuna madolariiiiiii.
Narudia kusema ndg zangu watanyania MUUNGANO NI JAMBO LA KHERI LAKINI SIO LA LAZIMA.