Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
Tume ya warioba ilifanya makosa sana kupendekeza muundo wa serikali 3. Wakati wa kutoa maoni nilibahatika kupata nafasi ya kutoa mtizamo wangu ktk hili..! Nilipendekeza tume iandae maswali juu ya suala la Muungano na swali muhimu ni je! Watanzania wanautaka muungano au la. Km hawataki kwa nini na km wanautaka uwe na muundo gani!!? Wananchi wapige kura za maoni(referundum)ili waamue wenyewe. Lkn pia muda wa kupata katiba ni mfupi mno,tuna haraka gani!?
 

Mkuu inawezekana watoto kwenye familia kuitisha kura ya maoni ili kuamua kuwa wanamtaka baba yao aendelee kuwa baba au la?
 
Zanzibar wana katiba yao na wanajitegemea kama nchi. Bara tunajitegemea lakini hatuna katiba yetu. Mnapoungana huwa kila mwenza kuna kitu hana na atakipata kwa mwenzake. Hata kwenye ndoa kila mtu anapata cheti chake.
Ili kila upande uridhike serikali tatu hazikwepeki.
Kwa sasa wazenji wanashiriki katika mpango wa maendeleo wa bara je wanatuchangia sh ngapi? Kule kwao sisi hatushiriki je tunawachangia sh ngapi?
Tusiharakishe kupata katiba mpya kwani itatugharimu siku za usoni.
 
Mkuu inawezekana watoto kwenye familia kuitisha kura ya maoni ili kuamua kuwa wanamtaka baba yao aendelee kuwa baba au la?
Ha haa haaa..! Heshima kwako mkuu. Jibu langu ni NDIYO inawezekana hasa inapotokea jamii inasema na hata watoto wenyewe wanasikia juu ya malalamiko hayo kuwa,huyo baba analea watoto wasio wake. Pengine jamii inajua mwenendo wa mama yao. Watoto lazima wapige kura kuamua km waendelee na baba yao anayepigiwa kelele kila mahali kuwa si baba yao au wamuulize mama yao kisha wapime DNA.
 
Nataka serikali tatu na Tanganyika zote mbili
 
Mimi naona Serikali moja ndo suruhisho ni serikali moja tuu kama tumeamua kuungana tuungane moja kwa moja kusiwe na Tanzania hizi Tanganyika na Zanzibar zivunjwe vunjwe ziwe mikoa
 
Serikali moja,nchi moja tu,kwani hapo ndo tutamjua ni nani kati yetu washirika wa Muungano yaani TANGANYIKA na ZANZIBAR anataka Muungano wa kweli. Na kuunganisha vitu viwili maana yake ni ili upate kimoja!!
 
serikali tatu ndo chaguo la wengi na kama ikishindikana tufanye serikali moja
 
Serikali tatu.

Sababu ni kurahisisha muungano.
 
serikali tatu ili kila upande wa muungano uwe na haki na mambo yake yasiyokuwa ya muungano, mfano umiliki wa ardhi nk
 
serikali tatu..ili muungano uvunjike
 

Mkuu hapo kwenye RED ndo penyewe hasaa kama kweli tunataka muungano wa kudumu tufanye serikali moja ila kama tunataka ushirikiano wa mda flani basi tufanye serikali 2 au 3
 

Achen kutufundisha uoga. Wewe unachotaka kusema hapo ni kuwa WAISLAM NI MAGAIDI. Ndo maana unasema tukitengana alshababu na alkaida watajazana zenji coz wazenji ni waislam. Au ina maana gani ingine? Kawaambie wazenji hayo maneno yako hapo juu uone kama utavuka bahari kurudi bara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…