Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
Serikali 2. Koti la muungano ndilo linalo leta utulivu zanzibar vinginevyo ni upemba na unguja.
 
Serikali 2. Koti la muungano ndilo linalo leta utulivu zanzibar vinginevyo ni upemba na unguja.

Ndivyo mnavyoambiwa makanisani ???

Kabla ya muungano huo uunguja na upemba mbona hatukuusikia ??
 
Mimi napenda Serikali Tatu, kwa sababu sisi waTanganyika tumekosa mlezi aliyepo ni wa "mama" wa kambo ambaye anachukua mali tulizoachiwa na wazazi wetu anawapa watoto wake wa kuwazaa (Zanzibar) huku tukiambiwa tumevaa koti la mama/baba yao kwa kutupumbaza tu. TUMECHOKA kutukanwa, kudharauliwa, kutengwa, kuteswa, kurubuniwa n.k kwa muda mrefu sasa YATOSHA tunataka mlezi mwema TANGANYIKA GOVT.
 
Maana halisi ya Muungano ni - "Union" itokanayo na kuweka vitu au watu pa-moja. Hivyo baada ya muungano kufanyika kitu-kimoja kinatakiwa kizaliwe chenye hadhi ya kuonyesha huo muungano (serikali ya muungano) huku walioungana wakibaki na majina yao na wasifu wao (serikali washirika)- Hii sio hesabu kusema 1 + 1 = 2! Ni lazima pale palipoungana paonekane! naa hiyo sehemu iliyoungana ndio serikali ya tatu
 
Mimi naona 3 ndio zinafaa na zitakuwa zimebalance kwa maana kwamba zanzibar watakuwa na serikali yao tanganyika hivyohivyo ma kutakuwa na serikali moja itakayowakilisha pande zote. Kukiwepo na tatu mzozo wa muungano utakufa kwasababu kila serikali utakufa na nafasi ya kuiwakilisha kwenye serikalinya muungano tofauti na sasa serikali mbili tanganyika haijulikani ipo wap ndio maana kuna mzozo wa muungano
 
Muungano = Bara + Visiwani. Kwahiyo Muungano una ardhi unahitaji elimu ya awali kuelewa. Ni sawa na kusema family haina ardhi wakati mama na baba wana ardhi. Kabla ya ccm kukazia serikali 2 wengi waliichukia sana hasa visiwani na nyuma yake serikali haikutaka katiba uwepo wa mpya. Wewe kama 'tape rewind it'. Ili tukubali serikali 2 tunaahiudiwa kuwa visiwani wataondoa kasoro za muungano. Kama ni kweli KWANZA WAAMBIE ETI WAZIOONDOE KABLA YA KUPITISHA SERIKALI 2, halafu usikie na ujionee mwenyewe kuwa hill ni ndoto. TUSIDANGANYANE kama watoto wafanyavyo. Swala kitu si 2 au 3 bali ni ipi inatekelezeka kwa urahisi kwa faida ya wengi.
 
Ulikuwepo kwa nini watu waliuana Januari 1964?


ile ilikua nipolitical isue kila chama yaani afroshirazi party.znp.zppp zilitaaka madaraka kutoka kwa muengereza chini ya ufalme wa kisultaan.
ndio machafuko yakatokea ua wenye kw wenye na kupewa nguvu na nyerere
 
Serikali 3 haziepukiki hata kama mkipitisha hiyo nya bungeni tutaendelea kudai katiba mpya hasahasa kwa mtu anaetegemea kugombea urais aweke sera ya katiba mpya kwenye ilani yake vinginevyo hatapita
 
Back
Top Bottom