Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
SERIKALI MBILI NDIYO MPANGO MZIMA WANZANIA TUSIKUBALI KUUVUNJA MUUNGANO WETU.
Wananchi wenzangu naomba niwaase kwamba tudumishe Serikali mbili kwani waotaka kinyume chake hawana lengo jema kwetu wameshapokea ujira Toka Kwa weupe NA wengine wanaona Kuwait serikali tatu zitawapa fursa kupata urais hivyo tuwaogopo kama ukoma maana wana pepo la madaraka hwafai kabisaaa watuondokee. Serikali mbili mpango mzima.
 
Kila kukicha utasikia wale wachache waking'ang'ana eti Serikali tatu na Utanganyika eti kupatikana kwa mambo haya ni suluhisho tosha kwa kero za Muungano. Sababu kuu eti tume zilizotangulia ziliongelea Serikali tatu, Jamani, mawazo kama haya hata wa ngumbalu au memkwa hawezi kuyaunga mkono. Hebu angalia haya mambo machache;
1: Tanganyika na Zanzibar zikiwa nchi kamili, je, Mkataba yote iliyoingiwa na Tanzania ya dhahabu, Tanzanite, Almas,gas, Uranium, Power Afrika, itakuwa chini ya nchi gani ikizingatiwa kuwa serikali ya shirikisho haitakuwa na Ardhi? Serikali ya Tanganyika raia wake watapatikanaje? Je, nani atawapa uraia wa Tanganyika? chini ya sheria uliyotungwa na bunge gani? Jamani tusipelekeshane kihivyo.
 
Ndugu yangu, Wahenga walisema kwamba "Bila utafiti huna haki wala ruhusa ya kusema chochote".
"No Research no Right to speak" Yaani unataka kunambia kwamba wewe unaweza kujilinganisha na nguli wajumbe wa tume ya Katiba, ambao hawana tuhuma yoyote? " Kumbe ni kweli walivyosema kwamba la kuvunda halina ubani.
 
Hao unaowaita "nguli" wamesemaje juu ya kuingia mikataba ya madini? Au ukimwona Tundu Lissu tu kashika mic unafikiri matatizo yoote ameyaongelea bila hata kujua kasema nini?
 
WanaJF Kwa mda mrefu sasa kuelekea utungaji wa katiba mpya kumekuwa na mjadala mkali kuhusu muungano wetu uwe wa muundo upi sasa ningependekeza tuwe na kura ya maoni hapa JF kuhusu muundo wa muungano, upi ni muundo sahihi?

1.Serikali moja.
2. Serikali mbili.
3.Serikali tatu.

N:B ukiweza kutoa sababu za muundo wa muungano unaoutaka itakuwa vizuri zaidi

serikari 3 ndio suruhisho la kila kitu
 
Hao unaowaita "nguli" wamesemaje juu ya kuingia mikataba ya madini? Au ukimwona Tundu Lissu tu kashika mic unafikiri matatizo yoote ameyaongelea bila hata kujua kasema nini?

Naona swala la muungano ndio wameweka kipaumbele kwani ndio mfumo utakaopelekeya mambo yote yataendeleya iwe ya serkali 3 au 2
 
Hii ni post niliondika kwa mmoja wa Wabunge la Katiba kutokana na reaction nilizoona akipongezwa kwa uwasilshaji
wake akiwa Mwenyekiti wa Kamati ambao ulinivutia.
Ana uwezo wa kujieleza, kupanga hoja na kuvutia wanaomsikiliza. Lakini yeye na wajumbe wengine wengi bado nina masuali kwao na kwa hivyo post hii si yake
binafsi tu ni pamoja na wajumbe wote wa Bunge la Katiba na ndio maana nikaona pia nii post hapa ili tusaidiane kukwamua nchi yetu katika mgando wa mawazo ya 2+3.

Salaam,
kama wengine unatumbukia katika shimo la kunukuu nukuu unazozipenda au zinazopendeza. Na mtindo huu umetulemaza katika bunge. Hebu stand aside and look into things from a position of a dwarf enjoying staying on the shoulders of a giant….kama alivyosema Mchungaji Msigwa kwa maana una advantage ya kuwa msomi na sio mkereketwa wa kawaida wa CCM.

Nionavyo mle ndani ni woga, mazoea, mahaba na khofu za kujitisha tu si jengine.
Sijashawishika na hoja za kubakisha mbili.
Nijibu mambo yafuatayo ili niridhike tubaki kuwa na mbili:

1. Tutakuwa na Serikali mbili ambazo hatujazifafanua kwanza na tukijua kuwa mbili tulonazo sasa zimetufikisha hapa ktk
lukuki ya migogoro.

- Tuna hakika gani Mbili Maboresho zina manufaa na pande zote mbili, maana kwa
sasa kinachochukuliwa ni kuiridhisha Tanzania Bara tu.

- Cha kushanga tunachosikia Mbili Maboresho ni kuchukua yale yale ambayo yameletwa na Tume ya Katiba katika Rasimu na kuyatumia na kisha kusema haya ni ya maboresho.

- Suali kama kungekuwa na UBORESHAJI basi CCM ilikuwa wapi?
- Kama kungekuwa na UBORESHAJI na CCM ikijua kuwa kuna haja ya uboreshaji basi CCM kwa nini isingeyafanya hayo bila ya kupoteza Blioni 70 za kuunda Tume?

2. Tatu zilizoletwa zimetolewa ufafanuzi. Kama kuna udhaifu au maeneo ya kukuziwa kwa nini isifanywe hivyo.

- Hoja gani za kiufundi za kukataa 3?
- Kwa nini tusikosoe 3 ili zibaki tatu na maslahi ya pande mbili yalindwe?
- Kwa nini CCM wanashindwa kuona kuwa kuna pande mbili za Muungano?

3. Utamshawishi vipi mtu akubal kubaki na mbili ambazo zitaboreshwa bila kujua na
kuyaona hayo maboresho kwanza Haitakuwa kuuziwa mbuzi katika gunia?

4. Hebu nijibu hizi inherent structural contradictions:
a) Tukibaki na mbili…chombo gani kitatunga sheria za Tanzania Bara? Kwa sababu kwa sasa Bunge la Muungano Art. 64 ndio lina jukumu hilo lakini hakuna uhalali huo kwa sababu hizi
- Ni makosa kulipa Bunge hilo kufanya kazi ya kutunga sheria za Tanzania bara
- Wabunge wa Zanzibar hawana uhalali wa kutunga sheria za Tanzania Bara
- Wabunge wa Znz hawabanwi na sheria za TBara na haijawahi kutokea mtu anaetunga sheria na kisha sheria hiyo isimbane.
b) Tukibakisha mbili Mahakama Kuu ya Tanzania ambayo kwa mazoea tumeiita hivyo kwa miaka 50 ina uhalali gani wa
kuendelea kuitwa hivyo?

Kiuhalisia hii ni Mahakama Kuu ya Tanzania Bara ikiwa hutaki kuiita Tanganyika. Hii inatokana na ukweli kuwa the so called Mahkama Kuu ya Tanzania ina
concurrent jurisdiction na Mahakama Kuu ya Zanzibar ( mamlaka zilizo sawa). Na ndio
maana Mzanzibari hakati rufaa Mahakama Kuu ya Tanzania bali Mahakama ya Rufaa kama Mtanzania Bara. Vipi uta reconcile hii bila ya kuwa na Tanganyika?

c) Mzanzibari anachagua Rais wa Tanzania. Lakini kwa mujibu wa Ibara 34 (3) huyu Rais wa Tanzania anakuwa pia msimamizi wa Tanzania Bara.

Jee kuna haki gani kwa Mzanzibari kumpigia kura msimamizi wa Tanzania Bara, kwa maana nyengine Rais wa
Tanzania Bara?

d) Je kwa nini tuendelea kumpa jukumu Rais wa Tanzania kusimamia mambo ya Tanzania Bara wakati ipo njia safi, salama
na isiyo dhihirisha ujuha wetu ya kuwa na Rais wa Tanganyika na kuwa na eneo la Tanganyika na wananchi wanaoishi Tanganyika kumpigia kura Rais wao

e) PM wetu, mimi kama Mzanzibari si rwangu. Kama Mtanzania sawa. Lakini
kichekesho kinakuwa PM wa Tanzania hana mamlaka yoyote yale na hana uwezo wowote wa kisheria wa kukamata hata kuku
katika eneo la Zanzibar.

- Huoni kuondosha contradiction hii ni kumu elevate huyu PM awe Rais wa Tanganyika ashughulike mambo ya Tanganyika kama anavyofanya asilimia 100 hivi sasa.

f) ni vipi tuta reconcile Waziri asiye wa mambo ya muungano kama walivyo hivi sasa kuitwa Waziri wa Muungano kama wa
Tawala za Mikoa, Afya, Kilimo? Kuna haki gani kisheria na kikatiba Waziri kama huyu kuitwa wa Muungano?

- Ni mbili gani maboresho ambazo zitaondoa contradiction hii bila ya Waziri kama huyu ama kumwita Waziri wa Tanzania Bara au Tanganyika?

g) Na tukibaki hapo hapo kwenye Uwaziri ni kwa haki gani Waziri huyu asiye wa Muungano alakini anayeitwa wa Muungano ana haki ya kuwakilish Muungano wakati mamlaka yake kiuhalisia ni sawa na Waziri wa Zanzibar.

- Yeye anashughulikia pande la nchi la Bara na huyu pande la nchi la Zanzibar ambapo tumekubali mapande haya yawepo, tena kipi kimpe yeye hadhi kubwa zaidi?

- Ubaya pia anakuwa na jeuri na kiburi kuwa yeye ni mkubwa zaidi? Hebu nipe tuta reconcile vipi hili?

h) Waziri huyu haendi nje kuisemea Zanzibar jee ana haki gani kuitwa wa Muungano? Waziri huyu kukutana na Waziri
wa Zanzibar hufanya kama ni ihsani…kuna haja gani ya kuwa na Waziri kama huyu?

- Wallahi mawaziri wa Zanzibar wamefanyiwa jeuri. Wakitoka nje Serikali ya Muungano humpa ka-mkurugenzi tu instrument za kuwakilisha nchi na Waziri wa Zanzibar akawa anabeba mkoba
wake.

- Muulize Waziri Omar Yussuf hakuwahi kulalamika hadharani kuwa wakati wa Waziri Mustapha Nkulo na yeye akiwa fedha Zanzibar kwa miaka 3 mizima Nkulo alikataa kuonana nae na kuchezesha foliti tu?

i) Katika Afrika Mashariki katika mambo 17 basi 4 tu ni ya Muungano. Zanzibar imetoa lini idhini ya kusemewa katika mambo yasio ya Muungano? Tena anaekwenda kutusemea si Waziri wa Mambo ya Nje bali ni Waziri asie wa Muungano? Haki iko wapi? Si ndio maana tuna migogoro isioisha?

j) Kwa mujibu wa Presidential Decree ya 1964 ya Nyerere civil service yote ya Bara ni ya Muungano na ni pamoja na mfanyakazi wa kijiji cha Kitanda, Tunduru ambaye hatoki kabisa katika Wizara yoyote ya Muungano.

- Mfanyakazi huyu toka mwanzo wa ajira yake analindwa na pensheni ya Muungano hata kama yeye hatoki wizara ya muungano. Lakini ikitokea mfanyakazi wa Zanzibar akihamia katika muungano miaka yake ya kazi yote ya Zanzibar inafutika na anaanz upya.

- Hata hili pia litarekebishwa vipi? Ndo maana Tume ikasema tutenganishe ajira hizi. Iwepo civil service ya Tanganyika, ya
Zanzibar na ya Muungano.

k) Tanzania Bara kwa kuwa ina sit Bunge, ina sit Urais, ina sit Makao Makuu ya Nchi inakuwa na hadhi mbili ndani ya moja.
Kukiwa na mzozo wowote Bara becomes Tanzania and Tanzania becomes Bara as against Zanzibar.

- Kwa hoja yoyote ya conflict Zanzibar haina nafasi ya kudeal na mshirika mwenzake Tanganyika bali ina deal na
Tanzania. Where is the fairness? How can Zanzibar get her rights? Na ndio tumefika hapa leo.

l) Ni namna gani tutakuwa na uwiano wa ajira za Wizara za Muungano bila ya kutenganisha Tanganyika na Zanzibar? Ni
lazima tuwe na mamlaka tatu ili katika mamlaka tunayo share na twenye jukumu la pamoja kuwepo na utaratibu unaoeleweka wa ajira.

- Leo kuwepo Mzanzibari kwenye ajira ya Muungano ni ihsani tu na kidogo kupenya penya.

- Hivi sasa kuna Mzanzibari mmoja tu Mwenyekiti wa Mamlaka, Katibu Mkuu mmoja tu na Director General mmoja tu

- Siku zote ama Zanzibar haina nafasi au ikiwepo nafasi basi ni Makamu. Hivi sisi tumekuwa relegated kuwa hivyo tu?
Hatustahiki, hatuna uwezo, hatuna elimu?

m) Tuna CAG anaitwa wa Muungano lakini pia anafanya kazi za Tanganyika. Kwa
mamlaka gani? Huyu CAG alipokuja Tume na kuulizwa kwa nini hakuwachukua Wazanzibari kujiunga na ajira za UN kwa
kuwa Tanzania ilipata nafasi 70 alisema,
“ Ni hiari yangu silazimishwi na sheria.”

n) Inasemwa kuwa kero zimekwisha zimebakia za kiganjani tu? Kero zipo 49 na
zote hazina suluhu baada ya miaka yote. Kama ni kujidanganya kusema Bandari si
Kero, Mambo ya Anga si kero, Kodi ya Mapato si kero, Mafuta na Gesi si kero, double taxation si kero, leseni za viwanda si kero, takwimu si kero na kadhalika.

- Hebu niambi ni sheria gani ya Tanzania ilotungwa kusafisha kero hiyo? Ni kifungu gani cha katiba kilichoondosha kero hizo?

- Jee kwa miaka 50 ni jambo gani la Muungano liloondolewa kwenye Katiba na kurudishwa kwa upande unaohusuka?

- Ndio maana Tume imesema sasa inaondosha kero hizo kwa kitendo cha kuyaondoa RASMI MAMBO HAYO kwenye orodha ya Mambo ya Muungano.

- Kwa maneno mengine Tume kufikia Mambo Saba mengi yamekwisha ondolewa lakini woga wa kuchukua hatua ya Kikatiba CCM walikuwa na kigugumizi au woga.

- Na kama hujui mwaka jana tu Zanzibar imeunda Baraza la Mithani huku ikielewa wazi kuwa Baraza la Mitihani kwa sasa ni
katika Mambo 22 ya Muungano Na kuna contradictions nyenginenyingi kama hizo. Pia tumeshindwa kuelewa kwa nini SMT na Zanzibar wasikae kwa miaka 50 kusuluhisha mambo kama yafuatayo:

- Kuunda mahaakama ya katiba ilotajwa kwenye katiba.

- Kuunda tume ya pamoja ya fedha ilotajwa katika katiba.

- Kutengeneza mfumo wa mchango wa muungano.

- Kutengeneza utaratibu wa migogoro ya muungano.

- Kutengeneza njia za kiila upande ku enjoy fursa za muungano.

- Kujenga misingi ya kuimarisha muungano ambayo leo inasemwa zikija 3 zitavunjika.

- Kushindwa kukubali ukweli kuwa Zanzibar ni visiwa na lazima ziishi kwa uchumi wa viiswa lakini badala yake kila siku kuikaba Zanzibar kiuchumi… unachukua mradi wa bandari huru unaopeleka Bagamoyo wakati suitable place ni Zanzibar.

- Hata akili ya kawaida kuipa Zanzibar eneo la kuwekeza Tanzania Bara haifanywi lakini mnatoa maeneo kwa ekari mamilioni kwa Wachina, Makaburu, Wakuwait halafu
mnaitusi Zanzibar kuwa haiwez kuchangia Muungano kwa uchumi wa karafuu na mwani.

- Kwa miaka 50 SMT imeshindwa kuonyesha presence yake kwenye eneo la Zanzibar. Kama nakumbuka kiji ofisi ya
Immigration, TRA na Bot na Mamlaka ya Bahari.

- Kwa miaka 50 SMT na SMZ zimeshindwa ku solve namna na mgawano mwema wa mapato ya taasisi za Muungano kama
TCRA, Posta, Simu na kama hizo. Inazungumzwa uwezo wa Zanzibar kutoweza kulipa mchango wake katika
Muungano.
Hii ni jambo la ajabu kwa sababu hilo lisemwe na Wazanzibari, lakini hata hao
Wazanzibari wanaounga mkono hoja hii ni “sell out” na hawakijui wanachokisema.

- Hakuna popote pale penye Muungano ambapo washirika hulipa 50-50 au kama ni zaidi ya wawili basi wote walipe kwa
mgao sawa.

- Principle ya Muungano huwa mbili. Ama ulipe kwa kuchaguliwa kodi maalum moja
au mbili au zaidi na kuwa za Muungano au kila upande kutakiwa kiwango maalum au
asilimia maalumu.

- Lakini principle ya pili ni ile yenye pacha mbili. Moja ni capacity to pay na pili ni
assessed contribution. Ndio maana kwa ku asses uchumi na mapato Marekani inalipa 300m dollars katika UN na Tanzania
48,000 dollars only. Lakini Denmark ambayo inaingia ndani ya Tanzania mara 20 inalipa 50m dollars.

- Principle ya tatu kwenye Muungano ni ile ya needassessment.

- Zanzibar ina watu 1,300 na Bara 44,000. Bara ina eneo la 960,000 sq miles na Zanzibar 2,600 sq miles na hatuwezi kuwa
na mahitaji mamoja.

- Kwa mfano kwa kiwango cha kimataifa cha askari kwa ratio ya 1:400 mahitaji ya Zanzibar ya Polisi ni 3,250 na Bara kwa ratio hiyo hiyo ni 107,500. Vipi hawa
watalipa sawa?

- Mahitaji ya Zanzibar na Bara ni ratio ya 1:33 kama ilivyo ratio ya watu wetu wa pande mbili za Muungano.

- Chengine ni mapato ya Zanzibar kama billion 270,000 visa vis ya Bara 1.7 trillion
ambapo humo ndani yake yamo mapato ya Tanzania. Tafadhali pata vyema ripoti ya Tume ya Fedha uone mnyumbuliko wa
mapato sekta kwa sekta ili uone jinsi ambavyo Zanzibar itaweza kujisimamia iwapo itakuwa na vyanzo vyake vya kiuchumi.

- Lakini hata kama Zanzibar isiwe na uwezo kwa sasa haina maana kuwa haitakuwa na uwezo maisha. Seychelles na Mauritius ni mifano mizuri. Mauritius per
capita yake ni 15,595 dollars (2011) na GDP ya 345 billion.

- Na Seychelles wa kwa 2012 walipata GDP ya 1 billion dollars na kwa hivyo per capita ya 11,164.

- Hebu ipeni Zanzibar haki na hadhi yake na muipe uhuru wa kiuchumi. Iwapo kwa sasa kwa kiwango cha assessed contribution ni 6 to 8 percent ya budget ya Tanzania mkiitengezea Zanzibar mazingira si hasha kwa figure kama za Mauritius na
Seychelles basi Zanzibar kuweza kuchangia hata 20 -25 budget ya
Tanzania.

- Hilo pia lishindikane basi pia katika Miungano kuna principles nyengine mbili tunapaswa kuzijua. Hizo ni ile ya SOLIDARITY na ile ya SUBSIDIARITY. Ukiingia katika Muungano hayo mawili ni
lazima.

- Kuwa na mshikamano na kusaidiana. Huwezi kukubali Muungano na mtu au huwezi kukubali kumuuoa mtu kisha
msiwe na mshikamano au msisaidine.

- Au kuoa mtu kisha ukasema
“angekuwa mrefu,” au kusema
“angekuwa na nywele za singa” Kama alivyo ndivyo umkubali. Siku moja nilimsikia Waziri Wasira akisema kuwa Serikali Tatu zingewezekana kama Zanzibar ingekuwa na saizi kama
Tanganyika. Oh, what a load of
rubbish.

- CCM inajibana kwenye takwimu za Tume na kuonyesha kile kinachoonekana ni flaw katika takwimu. Nini takwimu katika yote ambayo nimeyaaleza hapo juu, Takwimu ni tool tu lakini bado zinaelezeka vyema.

- Kwanza ni kuzisoma takwimu kama pande mbili za Muungano. Jee inakatalika idadi ya hao hao wanaoswikiliwa kuwa ni kidogo kuonyesha sampling ya nchi? CCM haiji na mfano wowote ambapo sample ilikuwa 100,000 au zaidi duniani.

- UK sampling hufanywa kwa watu 1,000 tu hata ile ya kuamua kuingia au kujitoa EU au kutumia Euro au kubakisha pound. USA sampling hata ya kujua Urais wa Marekani utaenda vipi katika uchaguzi fulani hufanyika kwa
watu 2,000 tu.

- Hata Synovet wakifanya uchaguzi kusema CCM ina nafasi ya kushinda uchaguzi sampling yao haijawahi kuvuka watu 1,000

- Lakini chengine CCM wanaji mislead kudai maoni ya Mabaraza ya Katiba
hayakuingizwa katika takwimu za
walikokataa mfumo wa Serikali Tatu.

- Kwanza wanajidanganya kwa sababu wanajua walivyo manipulate mabaraza ya katiba pili wanajipumbaza ( wanajidai
hawajui) kuwa madhumuni ya mabaraza hayakuwa kukusanya maoni.

- Maoni yalitolewa kabla na mabaraza kazi yake ilikuwa ni kutoa maoniya kuboresha
RASIMU. Kusema pale palikuwa na maoni ya mtu mmoja mmoja ni kufumba macho na
kujidanganya.

- CCM wanasema kwa nini maoni ya mabaraza yasichukuliwe. Kama ni kuchukuliwa basi ingekuwa kwa KILA BARAZA na sio idadi ya watu ndani ya
Baraza ambao walikuwa kama 19,000.

- Lakini humo ndani ya mabaraza pia walikuwamo watu walotaka Serikali 3 lakini Tume ilisema VERY VERY VERY SPECIFI kwamba haitachukua takwimu.Inashangaza leo CCM inadai tena kwa nguvu kuwa Tume imekwepa kuchukau takwimu.

- Mimi nashangaa na strategist wa CCM na pia nashangazwa na wasomi ndani ya CCM kwamba hata hili hawalioni.

- Hivi CCM hawajui kuwa mabaraza ya CHADEMA yalikuja na maoni 6,000,000. Walifika Tume na canter mzima ya maoni. Yepi maoni mengi yale ya mabaraza 19,000 ( hata tuseme yote ni ya CCM) au maoni ya
watu 6,000,000 yalokuwa yaletwe na Chadema?

- Kulikuwa na mabaraza ya taasisi kama 650 ambayo tume hoji kwamba mbona Tume inataja maoni ya mabaraza kama ya Ofisi ya Makamo wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, TRA, Baraza la Wawakilishi kuwa yalitaka Serikali Tatu.

- Pia kwa taarifa hata hiyo Bakwata, Episcopal Conference na wengine wengi walitaka Serikali Tatu lakini sasa
wanabadilisha msimamo wao.

- Hivi ungekuwa wewe katika Tume usingetaka mifano ya taasisi muhimu kama hizo kuonyesha nchi inakwenda wapi?
Tume haikufanya maamuzi yake kwa takwimu tu kama wengi wanavyotaka kuamini. Tumeshindwa kupata jawabu na
ndio tukaona njia pekee ni 3. Na kama mtu anakataa basi hoja zisiwe za emotions, hisia, mazoea na urithi wa waasisi
ambao ni wetu wote. “ We should not be held prisoners of the thinking of the
past generation."

Ahsante kwa kusoma dada Ummy, hata kama hutakuwa na nafasi ya kujibu, nimekusamehe.
Mambo mengine tumekubali kwa ujinga wetu. Na mungu amsamehe karume lakini mimi nisingekubali rais wangu aende
akajikubalishe kuwa yeye atakuwa makamo tu na mwengine awe rais maisha. Hii sijapata kuona hii. Na ndio tukafika hapa nishawishi na nitakuwa pamoja na wewe all the way.

Samahani kama kutakuwa naukakasi wa lugha

Ally Saleh
 
Hao unaowaita "nguli" wamesemaje juu ya kuingia mikataba ya madini? Au ukimwona Tundu Lissu tu kashika mic unafikiri matatizo yoote ameyaongelea bila hata kujua kasema nini?

Kwani wanaotuingiza kwenye mikataba mibovu wako chini ya Chama gani? Ama wanatuingiza kwenye Mikataba hiyo chini ya mfumo wa serikali ngapi? Mbona unaongea kama vile umeacha sehemu ya uelewa wako na akili sehemu fulani fualani kwenye zile nguo za rangi ya majani?

Wewe hushangai pale Mkulu alipoulizwa kule ufaransa kwa nini Tanzania ni nchi maskini wakati ikiwa na raslimali tele akasema hata yeye hajui kwa nini?
Hushangai tu chama kikubwa kama hicho kuamua kuingiza waganga wa kienyeji kwenye Bunge Maalum la Katiba/
Wewe hukushangaa serikali kuamia Loliondo kwa Bbabu kupata Kikombe na wakajenga miundo mbinu?
Wewe hushangai kusikia kuwa Hati ya Muungano haijulikani ilipo mara UN?
Wewe hushangai sasa kuanza mtindo wa chama tawala kurithisha madaraka kwa watoto wao baada ya Baba zao kufariki ama kustaafu?
Wewe hushangai sasa ziara za kutembelea wahanga wa mafuriko wakati wanaowajibika kujenga ,Miundo mbinu ndi tena wako mstari wa mbele kutembelea maeneo ambayo walipaswa kuwa wametengeneza miundo mbinu ya kutosha?
 
- Kaka JF huwa hatunadiki habari ndefu namna unless uwe umetumwa tu na SErikali ya UKAWA, hamna wa kusoma kitabu hapa kwa kawaida hapa unatoa hoja haraka na kwa ufupin sana nyie UKAWA mmefilisika kweli!!

Le Mutuz System

Jana nilikuuliza kama umepata fursa ya kuumuliza Waziri Mkuu wakati wa G55 kama anaeleza kwa makini sababu za kukubali hoja za kuwa na serikali tatu lakini MOD akafuta maoni yangu hukunijibu
 
- Kaka JF huwa hatunadiki habari ndefu namna unless uwe umetumwa tu na SErikali ya UKAWA, hamna wa kusoma kitabu hapa kwa kawaida hapa unatoa hoja haraka na kwa ufupin sana nyie UKAWA mmefilisika kweli!!

Le Mutuz System

Hio umesema wewe! Na km we ni mvivu wa kusoma basi waachie wengine wafyonze elimu.

Unless unapendelea mashairi. Ukitaka kufahamu lzm uwe na bidii kidogo ya kujifunza kwa utulivu.
 
- Kaka JF huwa hatunadiki habari ndefu namna unless uwe umetumwa tu na SErikali ya UKAWA, hamna wa kusoma kitabu hapa kwa kawaida hapa unatoa hoja haraka na kwa ufupin sana nyie UKAWA mmefilisika kweli!!

Le Mutuz System
Lina JF mlikaa mkapanga jinsi ya kuandika thread.

Unajua wewe una matatizo sana sijui huko Marekani unasema ulisoma chuo sijui chuo gani labda VETA ya Marekani.

Punguza uvivu jibu hoja.
 
- Kaka JF huwa hatunadiki habari ndefu namna unless uwe umetumwa tu na SErikali ya UKAWA, hamna wa kusoma kitabu hapa kwa kawaida hapa unatoa hoja haraka na kwa ufupin sana nyie UKAWA mmefilisika kweli!!

Le Mutuz System

Mi mbona nimeisoma yote na kuielewa, tena fasta tu, we unajiita system afu unashindwa kusoma, pole.

Kwa nyongeza tu, mwenzio kamwaga nondo zilizoambatana na ufafanuzi unaoeleweka, we hujaweza walau kunishawishi kuwa mleta mada ametumwa,
 
Mimi nipo Tayari kuiunga mkono CCM katika mpango wao wa serikali mbili ikiwa:-

Watataja changamoto zote za Muungano uliopo na jinsi ambavyo; mfumo wao wa serikaI mbili utajibu changamoto moja moja
 
- Kaka JF huwa hatunadiki habari ndefu namna unless uwe umetumwa tu na SErikali ya UKAWA, hamna wa kusoma kitabu hapa kwa kawaida hapa unatoa hoja haraka na kwa ufupin sana nyie UKAWA mmefilisika kweli!!

Le Mutuz System

Akili zako haziendani na mwili wako, mwili mkubwa akili ndoogo.
 
Kwani wanaotuingiza kwenye mikataba mibovu wako chini ya Chama gani? Ama wanatuingiza kwenye Mikataba hiyo chini ya mfumo wa serikali ngapi? Mbona unaongea kama vile umeacha sehemu ya uelewa wako na akili sehemu fulani fualani kwenye zile nguo za rangi ya majani?

Wewe hushangai pale Mkulu alipoulizwa kule ufaransa kwa nini Tanzania ni nchi maskini wakati ikiwa na raslimali tele akasema hata yeye hajui kwa nini?
Hushangai tu chama kikubwa kama hicho kuamua kuingiza waganga wa kienyeji kwenye Bunge Maalum la Katiba/
Wewe hukushangaa serikali kuamia Loliondo kwa Bbabu kupata Kikombe na wakajenga miundo mbinu?
Wewe hushangai kusikia kuwa Hati ya Muungano haijulikani ilipo mara UN?
Wewe hushangai sasa kuanza mtindo wa chama tawala kurithisha madaraka kwa watoto wao baada ya Baba zao kufariki ama kustaafu?
Wewe hushangai sasa ziara za kutembelea wahanga wa mafuriko wakati wanaowajibika kujenga ,Miundo mbinu ndi tena wako mstari wa mbele kutembelea maeneo ambayo walipaswa kuwa wametengeneza miundo mbinu ya kutosha?

Hao nguli ndo wamesema hayo uliyoandika?
 
Sasa wakuu mnajibu hoja za mleta hoja au mnajibu aliyeshauri habari ifupishwe ?

Anyway mkuu mleta mada jaribu kuweka habari yako vizuri isomeke mpaka mwisho sio kuingia mstari mwingine kila baada ya maneno matano, vilevile kama unaweza ku-summarize itakuwa bora zaidi (kama haiwezekani poa tu wahusika watasoma)
 
Kwani wanaotuingiza kwenye mikataba mibovu wako chini ya Chama gani? Ama wanatuingiza kwenye Mikataba hiyo chini ya mfumo wa serikali ngapi? Mbona unaongea kama vile umeacha sehemu ya uelewa wako na akili sehemu fulani fualani kwenye zile nguo za rangi ya majani?

Wewe hushangai pale Mkulu alipoulizwa kule ufaransa kwa nini Tanzania ni nchi maskini wakati ikiwa na raslimali tele akasema hata yeye hajui kwa nini?
Hushangai tu chama kikubwa kama hicho kuamua kuingiza waganga wa kienyeji kwenye Bunge Maalum la Katiba/
Wewe hukushangaa serikali kuamia Loliondo kwa Bbabu kupata Kikombe na wakajenga miundo mbinu?
Wewe hushangai kusikia kuwa Hati ya Muungano haijulikani ilipo mara UN?
Wewe hushangai sasa kuanza mtindo wa chama tawala kurithisha madaraka kwa watoto wao baada ya Baba zao kufariki ama kustaafu?
Wewe hushangai sasa ziara za kutembelea wahanga wa mafuriko wakati wanaowajibika kujenga ,Miundo mbinu ndi tena wako mstari wa mbele kutembelea maeneo ambayo walipaswa kuwa wametengeneza miundo mbinu ya kutosha?

We hushangai ulivo karirishwa jjinga? We hushangai kuona nyerere na karume wanakabshiana na kutiliana sahihi halafu huelewi?
 
Hao nguli ndo wamesema hayo uliyoandika?

Si nimekwambia shida yako haitofautiani na wajumbe wa CCM BMK kule Dodoma, Mmeambiwa na na Tume Msome Randama na Bango Kitita kila mnaposoma Rasimu na Taarifa maalum ya Tume. Wewe kaa kama ulivyo na Principle zako za Physics.
 
Nasikitika sana na wanaccm, hivi kweli kutamka tanganyika tunaleta ubaguzi lakini kusema zanzibar hatuleti ubaguzi! Kwel
 
Back
Top Bottom