Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
He! Ndiyo wamesema hivyo ccm? Kweli sasa nina shaka na upeo wao wa akili duh.
 
BUNGE Maalumu la Katiba limeelezwa kuwa si kweli kwamba muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar uliozaa Tanzania, haukuwa na ridhaa ya wananchi kama inavyodaiwa na baadhi ya watu. Badala yake, Bunge hilo limeelezwa kwamba ukweli ni kwamba viongozi wa kitaifa wa wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amaan Karume, walipata ridhaa ya wananchi kwa utaratibu uliofaa kwa wakati ule, kabla ya kufikia maridhiano wao wawili.

Hayo yalisemwa na Mjumbe wa Kamati Namba Nne ya Bunge hilo, Dk Khamis Kigwangala alipokuwa anasoma maoni ya Kamati hiyo baada ya kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu ya Katiba mpya kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Christopher ole Sendeka.

Kigwangala alisema kwa vigezo na vipimo vya leo, utaratibu uliotumika wakati ule ambapo idadi ya watu ilikuwa ni ndogo ukilinganisha na leo, idadi na viwango vya uelewa vilikuwa vidogo ukilinganisha na leo, mifumo ya mawasiliano na viwango vya kiteknolojia, ikiwemo masuala ya mawasiliano ya habari vilikuwa ni vidogo, umuhimu wa uamuzi wa kidemokrasia ni muhimu zaidi leo kuliko hata mwaka 1964.

Alisema kero za Muungano katika muundo wa serikali mbili uliopo, nyingi zimetatuliwa, lakini nyingine kadhaa kubwa na ndogo zimeorodhosheswa katika Ibara ya 269 ya Rasimu ya Katiba mpya na ambayo imeweka wazi utaratibu mahsusi wa kuzishughulikia na kuzitatua kwa kuweka Tume Maalum chini ya Ibara ya 109 ya Rasimu.

"Uwepo wa mapendekezo ya kuunda Tume ya Uhusiano na uwepo wa maandalizi ya kutatua kero za Muungano, chini ya Ibara ya 110 (d) ya rasimu ya Katiba mpya unadhihirisha kuwa hata Muundo wa Serikali Tatu unaopendekezwa na Tume kwenye Katiba mpya si muarobaini wa kero za Muungano, " alisema Kigwangala.

Source: HabariLeo
 
- Kaka JF huwa hatunadiki habari ndefu namna unless uwe umetumwa tu na SErikali ya UKAWA, hamna wa kusoma kitabu hapa kwa kawaida hapa unatoa hoja haraka na kwa ufupin sana nyie UKAWA mmefilisika kweli!!

Le Mutuz System

Jibu hoja wee mlamba hamila!
Msumari huu haukaliwi ng'o!
Mabaraza ya Katiba yaCCM hayakuwana hoja!
TUME iliita "HAKUNA ENEO" (soma Takwimu za Ukusanyaji Maoni sehemu 1.2.3.3 UK.12) na zikatupwa kapuni!
Hata mimi ningalitupilia mbaaali ukaririsho ule!
 
Tanganyika, Tanganyika, Tanganyika, Tanganyika, Tanganyika, Tanganyika, Tanganyika, Tanganyika, Tanganyika, Tanganyika, ×10 Huo ubaguzi uko wapi? Mbona siuoni.

Tanganyika, Tanganyika, Tanganyika, Tanganyika, ×100. Wee ubaguzi wee, uko wapi sasa mbona sikuoni?

Watanganyika unganeni mdai Tanganyika yenu ni haki yenu msiiogope wala kuionea haya hii haki yenu ya msingi.
 
Hio umesema wewe! Na km we ni mvivu wa kusoma basi waachie wengine wafyonze elimu.

Unless unapendelea mashairi. Ukitaka kufahamu lzm uwe na bidii kidogo ya kujifunza kwa utulivu.

Hili Li Le Mutuz liliziba nafasi bure ya watanzania wenye akili kusona nje ya nchi!
Kama limeshindwa kusoma mada inayovutia namna hii, laweza kutuambia liliwahi kusoma kitabu chochote likakimaliza?
Na je, likipewa mkataba litausoma kweli?!
Walamba hamila mfano wa Nape!
 
Sasa wakuu mnajibu hoja za mleta hoja au mnajibu aliyeshauri habari ifupishwe ?

Anyway mkuu mleta mada jaribu kuweka habari yako vizuri isomeke mpaka mwisho sio kuingia mstari mwingine kila baada ya maneno matano, vilevile kama unaweza ku-summarize itakuwa bora zaidi (kama haiwezekani poa tu wahusika watasoma)

Wataalamu wa lugha tunajua kwamba aya (paragraph)huanza na sentensi moja nk.
Kwa hiyo kama wazo moja linajitosheleza kwa sentensi moja, haina haja ya kuongeza maneno yasiyo ya lazima.
Kumbuka mleta mada ni mtaalamu wa lugha!
 
Kila kukicha utasikia wale wachache waking'ang'ana eti Serikali tatu na Utanganyika eti kupatikana kwa mambo haya ni suluhisho tosha kwa kero za Muungano. Sababu kuu eti tume zilizotangulia ziliongelea Serikali tatu, Jamani, mawazo kama haya hata wa ngumbalu au memkwa hawezi kuyaunga mkono. Hebu angalia haya mambo machache;
1: Tanganyika na Zanzibar zikiwa nchi kamili, je, Mkataba yote iliyoingiwa na Tanzania ya dhahabu, Tanzanite, Almas,gas, Uranium, Power Afrika, itakuwa chini ya nchi gani ikizingatiwa kuwa serikali ya shirikisho haitakuwa na Ardhi? Serikali ya Tanganyika raia wake watapatikanaje? Je, nani atawapa uraia wa Tanganyika? chini ya sheria uliyotungwa na bunge gani? Jamani tusipelekeshane kihivyo.

Makusudically, naona umejitoa ufahamu makusudically ili upotoshe makusudically!
Hauna hoja au haufahamu unalozungumzia.
 
Inaonyesha hujui ulisemalo kabisaaaa nakushauri acha ushabiki na rudi darasani ukasome halafu ndio uje na hoja sana, acha kupenda kuangalia sana Tbc inakudanganya sanaaaaa
 
Muungano unaofaa sasa Tanzania ni wa serikali tatu. Sababu kubwa Zanzibar kwa kutengeneza Katiba yao inayopingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya sasa hakuna njia muafaka zaidi ya serikali tatu la sivyo Zanzibar warudi wabadili maudhuii yaliyomo kwenye katiba yao. Hata kama Bunge la katiba litalazimisha muundo wa serikali mbili bado haitasaidia kama watanzania bara(Tanganyika) hawataridhika.
 
Kila kukicha utasikia wale wachache waking'ang'ana eti Serikali tatu na Utanganyika eti kupatikana kwa mambo haya ni suluhisho tosha kwa kero za Muungano. Sababu kuu eti tume zilizotangulia ziliongelea Serikali tatu, Jamani, mawazo kama haya hata wa ngumbalu au memkwa hawezi kuyaunga mkono. Hebu angalia haya mambo machache;
1: Tanganyika na Zanzibar zikiwa nchi kamili, je, Mkataba yote iliyoingiwa na Tanzania ya dhahabu, Tanzanite, Almas,gas, Uranium, Power Afrika, itakuwa chini ya nchi gani ikizingatiwa kuwa serikali ya shirikisho haitakuwa na Ardhi? Serikali ya Tanganyika raia wake watapatikanaje? Je, nani atawapa uraia wa Tanganyika? chini ya sheria uliyotungwa na bunge gani? Jamani tusipelekeshane kihivyo.

Kasome report ya Warioba acha kutupotezea muda.
 
Rasimu umeisoma lakini au umekurupuka tu?
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu, Wahenga walisema kwamba "Bila utafiti huna haki wala ruhusa ya kusema chochote".
"No Research no Right to speak" Yaani unataka kunambia kwamba wewe unaweza kujilinganisha na nguli wajumbe wa tume ya Katiba, ambao hawana tuhuma yoyote? " Kumbe ni kweli walivyosema kwamba la kuvunda halina ubani.

Ni aibu sana kuamini kila lililopendekezwa na hao unaowaita nguli wa tume ya kukusanya maoni! Wote wenye Elimu zetu tusingeingia kwenye tume hiyo, na si kila mapendekezo ya tume hiyo ni sahihi, kama ndivyo hivyo basi hata lile la kwamba kila kiongozi hususan mbunge, waziri na Rais lazima awe na shahada yaani Elimu ya juu, pia sekta ya utumishi haina umuhimu ktkt Muungano, hata mipaka ya bahari na mito haina maana kwenye Muungano. La maana ni serikali tatu tu. Ama kweli watu kama wewe ni Raia mizigo ndani ya Tz.
 
Mim serikali tatu ,ili wazanzibari wafurahi. Mfumo wa seriklali tatu kama,tume ya,warioba wa ccm mkongwe alivyopendekeza ingawa wamemkana.
 
Back
Top Bottom