Nikiwa mmoja kati ya watanzania wanaofuatilia mchakato wa kutengeneza katiba mpya ya JMT Mpya, nina maoni kidogo kuchangia.
Elimu tunayopat mashuleni ni elimu ya kuaminishwa kutokana na tafiti mbalimbali ambazo kwa upeo wa kila mmoja mmoja anapata uelewa wa kwake. Ni pale tu mtu anaposhindwa kumpiku aidha mwalimu wake au mtafiti aliyefikia kikomo fulani ndipo kiza cha kutokuelewa nini kinaendelea. Nitoe mfano tu kidogo. Waweza ukawa mzuri wa kusoma sana vitabu au makala za aina mbalimbali za watafiti waliopita na ambao jamii inawakubali lakini huyo mtu akashidwa binafsi kuendeleza mtazamo mpya ukizingatia maisha ni mabadiliko. Mpaka sasa ni watafiti wachache sana ambao tafiti zao zimeweza na zinaweza kudumu kwa karne nyingi zijazo.
Mtafiti Galileo enzi yake ya utafiti alisema dunia ni duara na si kama meza. Watawala walimkata shingo yake kwa kuitwa mpotoshaji lakini baadaye ikaja kubalika kweli dunia ni mduara. Yapo na mengine mengi.
Nirudu kwenye mfumo wa serikali ambapo tafiti nyingi zimeishia kusema kuwa mfumo wa serikali unaweza kuwa wa Mkataba, Shirikisho, Kidini, Kifalme, au serikali moja.
Kwa mtazamo wangu nadhani mfumo wa serikali unaweza ukagunduliwa zaidi ya hizo nilizotaja kama vile mwasisi wa taifa la JMT alivyo tengeneza mfumo ambao umedumu kwa muda mrefu sasa. Kwangu mimi naona ni mfumo wa aina yake ambao ulihitaji wana zuoni kuufanyia tafiti zaidi kwa kipindi chote cha uhai wake kuliko tu kulinganisha marekani wako hivi mbona sisi tusiwe hivo. Mwl Nyerere mwasisi wa mfumo wa muungano tunaotumia anaweza kwa asilimia kubwa ametengeneza mfumo ambao wengi hatukuweza kuuelewa zaidi ya mifumo tunayosoma vitabuni na taratibu zake.
Ukifuatilia hotuba zake utagundua kuwa mfumo aliouasisi mwl wa serikali moja dola mbili ulikuwa na taratibu zake ambazo aliziweka ndani ya azimio la Arusha. Ili mfumo wa mwl uweze kwenda kama alivyoasisi basi hatuna budi kurudi ndani ya azimio la Arusha hapo mfumo huo utaweza kutufaa na kufanya kazi bila matatizo.
Hivo kwa wale wanaodai mfumo wa serikali mbili nawashauri warudi pia kwenye utaratibu uliokuwa umewekwa ndani ya Azimio la Arusha. Na wale wanodai serikali tatu inabidi kwanza izaliwe upya serikali ya Tanganyika ipate mwakilishi kwa mshirika wake ambaye ni Serikali ya watu wa Zanzibar la sivyo tuwe na Serikali moja ya Kitaifa itakayo ondoa migongano yote