Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
serikali moja ndio njema, Mimi nadhani huu mpango wa serikali Tatu ni janja janja ya baadhi ya viongozi kujitafutia madaraka ambayo wanadhani wanaweza kuyapata kutokana na mfumo huo.tunaheshimu utaratibu huu uliowekwa na wazee wetu (karume na nyerere) kwa sababu za msingi ambazo mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kuzipinga (tafadhali pitia malengo ya muungano)
 
Kwa muda mrefu kumekuwapo na ubishi wa aina ya serikali inayotakiwa na watanzania nawaombeni raia wa jamhuri ya muungano wa tanzania watoe maoni yao hapa kwani yaonekana ndio yatakuwa ya maana zaidi kuliko kusemewa bungeni na watu wenye masilai yao
 
Kukata mzizi wa fitina ni kuitisha referendum! Pamoja na NEC kuwa ya CCM lakini hawataki kuitisha kura ya maoni.
 
Serikali mbili za nin kwa nchi zilizoungana na kuwa nchi moja?SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA inatosha! kama imeshndkana hapo bora kuvunja muungano. NCHI NI TANZANIA ambayo imegawanyika sehemu 2 yani TANGANYIKA ambayo ina mikoa yake,na ZANZBAR yenye mikoa yake!
 
Kwa hakika kumekuwa na mvutano mkubwa sana bungeni kuhusu aina ya muungano ambao unafaa kwa watanzania,Miimi ni mtanzania ambaye nimezaliwa katika kipindi ambacho nimekuta zanzibar na Tanganyika tayari zimeungana,Nafurahia kwenda zanzibar na nashukuru Mungu nimeoa mpemba japo mie ni Mtanganyika.

Binafsi kama ningepata jambo la kushauri bungeni kwa sasa nigejaribu kuwashauri wabunge wenzangu kujikita zaidi katika kutengeneza serikali moja ya Watanzania na sio serikali mbili wala tatu kama wengi wanavyoshabikia,Wabunge wanapaswa kufahamu kwamba hakuna muungano ambao utakuwa hauna changamoto,ata mke na mume ambao walikutana na kupendana mpaka kuoana ipo siku watatofautiana lakini ufumbuzi wa mgogoro wao sio kukimbilia kuachana bali wataitwa wazee na kuyaweka mambo sawa

Inawezekana kabisa waasisi wetu kuna baadhi ya maeneo walishindwa kuyatengenezea msingi ila nina imani kama bunge la katiba litakaa chini na kutengeneza misingi mizuri ya muungano kunaweza kukaleta suluhisho la changamoto za muungano,Kwa mtazamo wangu muungano wa serikali tatu unaweza ukawa muungano wa kukidhi haja na matakwa ya kisiasa lakini nina imani muungano wa serikali moja ya Tanzania utakuwa ni muungano thabiti ambao nina imani sisi sote tunafurahia kuwa kitu kimoja.

Nasisitiza kwamba mimi ni Mtanzania ninaipenda tanzania ninaupenda muungano na daima napenda muungano wetu hudumu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRICA
 
ujue kama una 'mtindio' wa ubongo ni matatizo makubwa sana!!..sio kila ukitoka kunywa 'kibuku' lazima upost uzi hapa!!...sa hapo ndo umeongea pumba gani!
 
Maajabu anataka mbili lkn anataka Tanganyika mambo yasio ya muungano yasi valiwe na Tanzania
 
Nimesikiliza kwa umakini mjadala wa rasimu ya bunge baada ya uwasilishaji toka katika kamati. Nilichokiona ni kwamba muundo wa serikali tatu umepewa nguvu ya maelezo ya namna ya kuendesha serikali hizo. Cha kunishangaza sijasikia kabisa namna ya kuboresha serikali mbili zenye tija kwa maslahi yetu sisi wananchi. Na wao utawasikia wakitumia hoja za maelezo ya muundo wa serikali tatu in a negative way kujenga hoja zao yaani ni kama vile wanapinga tu muundo wa serikali tatu. Mfano mzuri ni suala la gharama za uendeshaji wa seriakli tatu. Wanaodai serikali tatu wanatoa maelezo ya njia ya kuziendesha lakini wafuasi wa serikali mbili wanapinga hoja hiyo (katika mtazamo hasi) kwa kutumia hoja za wafuasi wa serikali tatu.

My take: Waje na hoja ya namna gani wataboresha muundo wa serikali mbili
 
Unitary system of government is the best if we agree upon it nyumba ikiwa na Mume mmoja inaweza ongozwa vyema
 
katika title namaanisha serikali tatu ndo zenye maelezo na mbili ndo zimekuwa na ugumu katika maelezo yake.
 
Mengine ni propaganda za wanasiasa tu ambayo hayana maslahi ya moja kwa moja kwa taifa!! Kama tukiweka uzalendo na taifa kwanza basi muundo wa SERIKALI MOJA NDIO UNAO FAA!
 
serikali 3 imesimama kwa mtazamo wangu.nikiwa na maaana 1.itakua ya muungano wa tanzania na znz 2.serikali ya tanzania bar 3 .serikali ya znz hizi mbili zitakua zikifanya mabo ya husio maeneo husi na hii kuu itakua inaungalisha shunghuri
zote ambazo zitakua zimetendwa na serikal hizo zote ili kupata huwiano na usawa katika hakiki na umikikazi wa mazingira na raia wake
 
Nikiwa mmoja kati ya watanzania wanaofuatilia mchakato wa kutengeneza katiba mpya ya JMT Mpya, nina maoni kidogo kuchangia.
Elimu tunayopat mashuleni ni elimu ya kuaminishwa kutokana na tafiti mbalimbali ambazo kwa upeo wa kila mmoja mmoja anapata uelewa wa kwake. Ni pale tu mtu anaposhindwa kumpiku aidha mwalimu wake au mtafiti aliyefikia kikomo fulani ndipo kiza cha kutokuelewa nini kinaendelea. Nitoe mfano tu kidogo. Waweza ukawa mzuri wa kusoma sana vitabu au makala za aina mbalimbali za watafiti waliopita na ambao jamii inawakubali lakini huyo mtu akashidwa binafsi kuendeleza mtazamo mpya ukizingatia maisha ni mabadiliko. Mpaka sasa ni watafiti wachache sana ambao tafiti zao zimeweza na zinaweza kudumu kwa karne nyingi zijazo.
Mtafiti Galileo enzi yake ya utafiti alisema dunia ni duara na si kama meza. Watawala walimkata shingo yake kwa kuitwa mpotoshaji lakini baadaye ikaja kubalika kweli dunia ni mduara. Yapo na mengine mengi.
Nirudu kwenye mfumo wa serikali ambapo tafiti nyingi zimeishia kusema kuwa mfumo wa serikali unaweza kuwa wa Mkataba, Shirikisho, Kidini, Kifalme, au serikali moja.
Kwa mtazamo wangu nadhani mfumo wa serikali unaweza ukagunduliwa zaidi ya hizo nilizotaja kama vile mwasisi wa taifa la JMT alivyo tengeneza mfumo ambao umedumu kwa muda mrefu sasa. Kwangu mimi naona ni mfumo wa aina yake ambao ulihitaji wana zuoni kuufanyia tafiti zaidi kwa kipindi chote cha uhai wake kuliko tu kulinganisha marekani wako hivi mbona sisi tusiwe hivo. Mwl Nyerere mwasisi wa mfumo wa muungano tunaotumia anaweza kwa asilimia kubwa ametengeneza mfumo ambao wengi hatukuweza kuuelewa zaidi ya mifumo tunayosoma vitabuni na taratibu zake.
Ukifuatilia hotuba zake utagundua kuwa mfumo aliouasisi mwl wa serikali moja dola mbili ulikuwa na taratibu zake ambazo aliziweka ndani ya azimio la Arusha. Ili mfumo wa mwl uweze kwenda kama alivyoasisi basi hatuna budi kurudi ndani ya azimio la Arusha hapo mfumo huo utaweza kutufaa na kufanya kazi bila matatizo.
Hivo kwa wale wanaodai mfumo wa serikali mbili nawashauri warudi pia kwenye utaratibu uliokuwa umewekwa ndani ya Azimio la Arusha. Na wale wanodai serikali tatu inabidi kwanza izaliwe upya serikali ya Tanganyika ipate mwakilishi kwa mshirika wake ambaye ni Serikali ya watu wa Zanzibar la sivyo tuwe na Serikali moja ya Kitaifa itakayo ondoa migongano yote
 
Serikali 3
Kwa mantiki ifuatayo
1:Ili kuwe na usawa wa maamuzi kati ya Tanganyika na Zanzibar
2:Selikali kuu itashughulikia mambo machache hivyo kutakuwa na ufanisi wa kutosha
3😛ia napendekeza ardhi na mipaka yake,madini,jeshi,uchumi,pamoja na masuala yote ya ulinzi na usalama viwe ni mambo ya muungano na Selikali kuu itawajibika kuziendesha Selikali wanachama kikatiba.
 
Nikiwa mmoja kati ya watanzania wanaofuatilia mchakato wa kutengeneza katiba mpya ya JMT Mpya, nina maoni kidogo kuchangia.
Elimu tunayopat mashuleni ni elimu ya kuaminishwa kutokana na tafiti mbalimbali ambazo kwa upeo wa kila mmoja mmoja anapata uelewa wa kwake. Ni pale tu mtu anaposhindwa kumpiku aidha mwalimu wake au mtafiti aliyefikia kikomo fulani ndipo kiza cha kutokuelewa nini kinaendelea. Nitoe mfano tu kidogo. Waweza ukawa mzuri wa kusoma sana vitabu au makala za aina mbalimbali za watafiti waliopita na ambao jamii inawakubali lakini huyo mtu akashidwa binafsi kuendeleza mtazamo mpya ukizingatia maisha ni mabadiliko. Mpaka sasa ni watafiti wachache sana ambao tafiti zao zimeweza na zinaweza kudumu kwa karne nyingi zijazo.
Mtafiti Galileo enzi yake ya utafiti alisema dunia ni duara na si kama meza. Watawala walimkata shingo yake kwa kuitwa mpotoshaji lakini baadaye ikaja kubalika kweli dunia ni mduara. Yapo na mengine mengi.
Nirudu kwenye mfumo wa serikali ambapo tafiti nyingi zimeishia kusema kuwa mfumo wa serikali unaweza kuwa wa Mkataba, Shirikisho, Kidini, Kifalme, au serikali moja.
Kwa mtazamo wangu nadhani mfumo wa serikali unaweza ukagunduliwa zaidi ya hizo nilizotaja kama vile mwasisi wa taifa la JMT alivyo tengeneza mfumo ambao umedumu kwa muda mrefu sasa. Kwangu mimi naona ni mfumo wa aina yake ambao ulihitaji wana zuoni kuufanyia tafiti zaidi kwa kipindi chote cha uhai wake kuliko tu kulinganisha marekani wako hivi mbona sisi tusiwe hivo. Mwl Nyerere mwasisi wa mfumo wa muungano tunaotumia anaweza kwa asilimia kubwa ametengeneza mfumo ambao wengi hatukuweza kuuelewa zaidi ya mifumo tunayosoma vitabuni na taratibu zake.
Ukifuatilia hotuba zake utagundua kuwa mfumo aliouasisi mwl wa serikali moja dola mbili ulikuwa na taratibu zake ambazo aliziweka ndani ya azimio la Arusha. Ili mfumo wa mwl uweze kwenda kama alivyoasisi basi hatuna budi kurudi ndani ya azimio la Arusha hapo mfumo huo utaweza kutufaa na kufanya kazi bila matatizo.
Hivo kwa wale wanaodai mfumo wa serikali mbili nawashauri warudi pia kwenye utaratibu uliokuwa umewekwa ndani ya Azimio la Arusha. Na wale wanodai serikali tatu inabidi kwanza izaliwe upya serikali ya Tanganyika ipate mwakilishi kwa mshirika wake ambaye ni Serikali ya watu wa Zanzibar la sivyo tuwe na Serikali moja ya Kitaifa itakayo ondoa migongano yote

moja ndo ina faa mengine majimbo, yafaa wawekwe magavana huko au masenetor
 
Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu
Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu
Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu
Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu
Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu
Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu Tatu .....
 
Back
Top Bottom