Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
serikali 3...
sababu: muundo uliopo hautekelezeki bila kubadili mkanganyiko uliopo kwenye katiba ya znz ki2 ambacho hakiwezi
kutokea..
pia serikali 3 inatoa dira ya kutekelezeka ya sera ya transparency ki2 ambacho hatukishuhudii kwa miaka 50.
mwisho, kuna kaudikteta kutaka kuweka kando mapendekezo ya tume na kuingiza mawazo ya watu wachache...
na kuna dishonesty iliyo dhahiri kwa ofisi kubwa za serikali kujipinga wenyewe.... all in yote wananchi wataamua mwisho wacku
 
Serikali 3 Tanganyika, Zanzibar na Jamhuri ya Muungano. Haiingii akilini kuendelea na serikali 2 ni vema ingekubalika moja maadamu hiyo haiwezekani basi ziwe 3 kama nilivyoainisha ili kudumisha muungano nayo ikishindikana basi muungano ufe kila nchi iwe na serikali yake huo ndio ukweli na tutasimamia kwa gharama yoyote
 
Serikali 3, yaani Tanganyika, Zanzibar na serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania. Hii itaongeza uwazi na uwajibikaji miongoni mwa viongozi na watendaji wa serikali hizi.
 
Serikali moja (1). Sisi ni ndugu wa muda mrefu kama sio roho ya ubinafsi na ubaguzi serikali moja inatosha kudumisha undugu wetu.
 
Serikal tatu ndio suruhishi maana itareta usawa wa kira pande ina itaondoa mtafaruku na marumbano yaliyopo kwa sababu wazanzibar wanataka nchi yao na watanganyika tunataka nchi yetu tunataka serikal tatu ni kwa ajili ya kuuenzi muungano na viongoz wetu wario tutangulia, bira hivyo ilikuwa kira nchi ibaki na chake, alafu niwashangae kidogo ndugu zangu wanao mg'ang'ania serikal mbili sijui ninani kawaroga! Hainiingii akilini kwamba mtu unaerim yako ya kutosha unashindwa kung'amua mambo madogo kama haya binafs nakuwa na wasiwawas na erim zao, zanzibar ina kila kitu chake kasoro ni fedha tu!Sasa pana muungano gani hapa?
nakuunga mkono ndg ila rekebisha kiswahili chako... SURUHISHI ni suluhisho. ITARETA ni italeta.
 
Serikali moja (1). Sisi ni ndugu wa muda mrefu kama sio roho ya ubinafsi na ubaguzi serikali moja inatosha kudumisha undugu wetu.

lazima kwanza uelewe hu ni muungano ambao duniani hakuna wa mfano wake. kiufupi ni muungano wenye mashaka tena makubwa. sasa basi! kwa mtazamo huu ni kwamba sasa ndio umefika wakati muafaka kuuchambua na uchambuzi wake ni kuirudisha serikali ya Tanganyika.
tunasifiwa duniani kwa kuwa na muungano feki
 
Muundo ma serikali unaofaa ni wa serikali tatu (3).
Serikali mbili hazifai kabisa zitatusababishia maafa makubwa siku za usoni!
 
Nadhan kila moja hapo lina faida zake na hasara zake.kwa akil zangu za kijinga me nadhan s1 n bora zaid sababu utakuwa n muungano wa kwel.kwa ukiangalia tushaingiliana kiundugu nk miaka mingi hzo serikal mbil au tatu c muungano tunaraka taifa moja bendera moja rais moja.ikishindikana bas vyovyote itakavyo kuwa sawa mrad tu utaifa uwe mbele
 
Pleae wakati unacomment hapa ni vyema ukaVote pale juu ili tuweze kuangal;ia Watanzania Wengi wanataka Muundo upi wa Selikali ambao utatatua kero za Muungano wetu

Yaani JF ndio mawazo ya "Watanzania walio wengi?" Au ndio yale yale ya Takwimu za akina Warioba?
 
Muundo ma serikali unaofaa ni wa serikali tatu (3).
Serikali mbili hazifai kabisa zitatusababishia maafa makubwa siku za usoni!

Kadri unavyoongeza idadi ya Serikali ndivyo unapoongeza idadi ya kero!
 
Eleza Faida Ya Serikali 3 Na Hasara Ya Serikali Mbili,au Eleza Faida Ya Serikali 2 Na Hasara Ya Serikali Tatu,karibuni
 
Faida ya serekali tatu ipo kwenye rasm tulishatoa maoni i kwenye tume ya warioba !
Maoni mengine ni kuchakachuwa
 
Back
Top Bottom