Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
Ningewaomba mods baada ya sired hii kufika ukingoni kutuwekea sired nyengine itakayo toa option if raia wa hapa wengi wao wametaka serikali tatu na serikali tatu kwa mchakato unavyoendea kule bmk haziwezekani!

Jee ikishindikana serikali tatu ni bora
1 kuvunja muungano?
2 kuendelea na serikali 2?
3 Or serikali moja?
...
In short, what is your second option if serikali 3 zikishindikana?
 
Muungano wa Marekani hauna Kero za muungano wala Wizara ya muungano hata Ada za muungano hulipwa kwa wakati si Kama Zenji wamekwepa Ada ya muungano kwa miaka 47, Zile nchi ndogo ndogo hazifugi watu kwa kuzitegemea Nchi kubwa , kila Nchi inajielewa haina Utegemezi wa Makusudi Kama Zenji inavyomchuna Buzz Tanganyika , muungano wao upo kisayansi sana , Ukabila,Udini, na Uchoyo wa Ardhi na mafuta. ni mwiko , hawana wajanja wajanja wanafuja pesa za muungano ! Tujifunze kwao Rais awe mmoja tu.

Mkuu kipindi kile kilikuwa cha udekteta lakini udekteta wake siyo wa mauwaji ni wa mnyonge yaani kulia anauma na kushoto anapuliza na akitamka jambo lolote basi huwa kuun fa yakun na na ukimpinga tuu basi siku hiyo hiyo tena mida ya alfajiri unapotea sasa hapo utatia neno na matunda ya nyerere ndio haya sasa kwa kuifanya zanzibar kuwa koloni la tangayika na wakati ule unguja walikuwa kwenye usingizi wa pono sasa wameamka na hataki tena kutawaliwa na mafisadi wa tanganyika na washajua rasimu ya katiba kina kipengere cha 6 na 1 0 kinatamka hivi munguja yoyote akitaka kuwowa mke basi itamlazimu kwenda dodoma kuchukuwa shahada ya ndoa na sasa wanaona kama ni koloni la sahara ya magaharibi kutawaliwa na muroko

Which is which?
Mbona mnaongelea ushabiki wadau?
 
je wanaodai kuwa sie tushakuwa ndugu wa damu wako tayari kwa selikali moja???kama hawako tayari baada ya miaka hamsini solution ni selikali tatu....kama wazanzibari wanaithamini sana nchi yao kiasi cha kutokuwa tayari kuungana na kuwa nchi moja,basi watanganyika nao wanapaswa kuithamini nchi yao mama(tanganyika)na sisi sote tukutane kwenye muungano....ina maana wazanzibari wanauchungu na nchi yao kuliko watanganyika???lazima hapa kuna jambo ambalo viongozi wa ccm wanatuficha na sio sahihi kwa vile huu ni muungano wa wananchi na sio wa ccm...
 
!
!
aaaah mbili tu zinazingua, bora iwe moja ila kama haiwezekani basi ziwe tatu au kama zikibaki mbili basi ziwe ya tanganyka na ya muungano

Hahahahahaaa!
Sasa mkuu kama 2 zinazingua kiasi cha kupendekeza 1, jee hizo 3 hazitozingua zaidi?
Tiririka mkuu!
!
!
 
bado hoja ya serekali tatu imekaa kisiasa zaidi. haina msingi na hoja madhubutu. inaonekana kujengwa kishabiki zaidi. angalieni uhalisia wa hali ya nchi yetu alaf ndo mfikirie kuleta serekali ya 3. 2 zinatushinda io yatatu itatuzika kabisa. nasisitiza uzalendo na umakini na nchi yetu. serekali inatakiwa ipungue ibaki moja ambayo tunaweza kujitahidi kuimudu. serekali zaidi ya moja ni majanga kwa watanzania.
 
Muungano ni wa serikali moja kama wanavyo dai wajumbe wa ccm kuwa 3 zinagharama na mbili hivyo hivyo zinagharama serikali 1 itaondoa gharama zote za serikali ya SMZ Kwa ujumla kuanzia Rais wote 3 wa znz itakuwa hakuna Bara la wawakilishi itaondoa vikosi vya ulinzi vya smz kwa ujumla tutapunguza gharama kubwa za matumizi tukiwa na serikali 1.
Na hili litawezekana kirahisi kwa kuwa wzanzibari wengi wanaasili na Tanganyika kiundugu na kifamilia.pia serikali 1 itawahakikishia wazanzibari kuishi salama bila hofu ya kurejea kwa SULTANI JEMSHED/ waarabu.
Mm sioni mantiki ya wajumbe wa Bunge la katiba wa ccm kusimamia serikali mbili wakijinasibu kuwa wao ni wznz wenye kutokea Tanganyika halafu bado wanajenga hoja ya serikali 2 badala ya 1.
Nivyema sasa wana ccm znz kujenga hoja ya serikali 1 kwa sababu nilizo zianisha.
 
Huu muungano feki kati ya kata Zanzibar na nchi ya Tanganyika uvunjike tu kama wao kata hawataki serikali moja na sisi nchi kwa maana Tanganyika hatutaki mbili kwa kuwa Tanganyika haitaonekana.
NAUVUNJIKE!
 
tumechoka na unafiki wa ccm wa serikali mbili,pia tunasikitika mnadai eti tunaotaka serikali tatu tuko wachache?je wanaccm mliobungeni mnapata wapi mamlaka ya kutuamlia serikali mbili wananchi milioni 45?.hatutaki unafiki wenu.mlipouza nchi kwa vyandarua tulinyamaza,gesi mkapeleka msoga tukanyamaza,hela za EPA MKALA tukanyamaza,mkabaka na kuambukiza watoto wetu h.i.v tukanyamaza,wake zetu mkawakosovo igunga tukanyamaza,mgao wa umeme tumenyamaza,mafuta yamepanda tumenyamaza,kura mkaiba 2010 tukavumilia,Shilembi wa shinyanga mkamnyang'anya ubunge wake tukanyamaza,mkaahidi ujenzi wa hospital ya Kwangwa musoma tukanyamaza,reli ya moshi hadi mara mliahidi tukanyamaza,meli mpya ziwa victoria mliahidi tukavumilia,hospital za rufaa kila mkoa mliahidi tukanyamaza,ajira milioni moja tumenyamza,mkaenda mbali zaidi mkaahidi maisha bora toka 2005 hata bila chembe ya aibu tukanyamaza,mkawanunua madiwani wa chadema na wengine mkawafukuza madiwani wa chadema Ilemela bila kosa tukanyamaza.tumechoka hatuogopi kitu MPANGO MZIMA NI SERIKALI TATU,UTAIFA KWANZA UNAFIKI BAADAE.
 
Muungano ni marithiano kati ya mataifa au nchi mbili zenye tamaduni zinazoshabihiana.Na muungano unatakiwa uwe na haki kwa pande zote mbili kusiwe na mmoja kuchukua madaraka ya mwingine.

Sidhani kama wananchi kwa hakika wanajali serikali mbili,moja au tatu,nadhani wananchi tunahitaji maendeleo na uchumi uliokua siyo kwenye makaratasi bali uonekane kwenye jamii ya watanzania.

Wananchi wanachukizwa na viongozi walioko madarakani ambao wako very busy kujilimbikizia mali,kuuza raslimali za taifa,maliasili zetu ,matumizi mabaya ya fedha za umma,hakuna uwajibikaji,uadilifu wala uwazi.Rushwa ndiyo imekuwa haki siku hizi,hauwezi kupata haki yako kisheria,afya,elimu na hata ajira bila kutoa rushwa.

Ufisadi umefika mahala pake kiasi kwamba ufisadi umekuwa haki badala ya dhambi,madawa ya kulevya ndiyo usiseme,sasa haya ndiyo yaliyotakiwa kuundiwa tume kujadiliwa ni namna gani viongozi au wafanyabiashara au wafanyakazi kwenye sekata za umma wanaweza kuwajibishwa ili kurejesha maendeleo na hadhi ya utaifa.

Ninauhakika haya ndiyo wananchi tunayoyahitaji na si serikali mbili au tatu.

selikali mbili zimeshindwa kutuhakikishia vitu hivyo, wizi,uongo ,utapeli, ufisadi ulio kubuhu ni mazao ya selikali 2!
 
selikali mbili zimeshindwa kutuhakikishia vitu hivyo, wizi,uongo ,utapeli, ufisadi ulio kubuhu ni mazao ya selikali 2!

Je,wadhani serikali mbili ndiyo tatizo hapo? Upande wangu nadhani tatizo ni viongozi wetu wasiojielewa,wanaovunja katiba,wanajilimbikizia mali,walafi wa madaraka na wezi wa mali za umma,hawa ndiyo matatizo.Wanaoongeza matatizo ni baadhi ya Mahakimu na majudge wetu ambao wengi wao wako busy kutafuta posho kuliko kufanya kazi waliyosomea kwa uadilifu.
 
Mimi naona 3 ndio mpango mzima sina chakuongeza mengi yameshasemwa na wenzangu
 
Back
Top Bottom