Uliyoyasema ni kweli, ambapo inafahamika kuna wanaotaka muundo wa serikali2 na wengine serikali3. Lakini wale wanaohisi( niki declare interest hapa mimi napendelea serikali1, ila napenda pia serikali3 ikiwa 1 inashindikana) kuwa serikali 3 ni ANGALAU suluhisho naona wanamashiko. Tume zote zilizotangulia zilikuja na muundo wa serikali3, hapa chama tawala wajiulize mara mbilimbili, ushabiki uachwe kando, tafukuri ishike nafasi, je tume zote zimeleta mapendekezo ambayo wananchi kweli hawajapendekeza? Hivi ni kweli kuwa uongo uwe tu kwenye muundo wa Muungano?! Viongoz wetu mujifunze kukubali ukweli kama munamuogopa Mungu. Yaani kabisa unajua 4+4=8, halafu ulazimishe jawabu ni 4 4, 448,844, 8=8, 9 au 44?, nafsi haziwasuti kushabikia jambo ambalo kimoyomoyo unajua siyo sahihi ila kwa maslahi yaliyojificha unasema ni sahihi? Tuwe wacha Mungu.