ghilipolla
JF-Expert Member
- Jan 6, 2014
- 280
- 53
mkuu unayosema yana ukweli kwa kiasi fulani, lakini watanzania hawana uwezo wa kukataa katiba hii ya ccm! Ccm na wapambe wao watamwaga pilau na vipesa kwa masikini wa kitanzania ambao ni wengi na watashinda tu! Tatizo la tanzania kwa sasa ni watanzania wenyewe na si kingine!Hapa tutarajie katiba ya CCM sio katiba ya Watanzania. Kikwete alipopingana na matakwa ya chama chake ya kutokuandika katiba mpya nilimuona wa maana kidogo. Lakini kwa mambo yanavyokwenda, ni usanii tu unafanyika as usual. Tujiandae kuikataa rasimu ya katiba kwenye referundum.
Tiba
Ndivyo nilivyomsikia mwenyekiti wa kamati hiyo ya Siri na Uwazi katika taarifa ya habari akisema pande zote 2 zimetoa hoja za msingi na za kidemokrasia na kushindwa kutoa maamuzi na Usiri huo na Uwazi kurejeshwa tena kwa Wajumbe kwa maamuzi.,
Source: Chanal10
Tatizo halipo kwa ccm tu,tatizo lipo kwa vyama vyote na wapambe wao,kwa sababu kila chama kimekwenda dodoma kikiwa tayari mkononi kina agenda ya katiba wanayo ihitaji na mifumo ya au serekali 2 au serekali 3,hili lilikua tayari nitatizo,na wanasiasa wanauwezo wa kuwashawishi wajumbe wawakilishi tokea kada mbali mbali na taasisi mbali mbali,kuwaunga mkono,TWAMBIENI NININI FAIDA YA SEREKALI 3 NAIPI NI FAIDA AU HASARA YA SEREKALI 2,
Uliyoyasema ni kweli, ambapo inafahamika kuna wanaotaka muundo wa serikali2 na wengine serikali3. Lakini wale wanaohisi( niki declare interest hapa mimi napendelea serikali1, ila napenda pia serikali3 ikiwa 1 inashindikana) kuwa serikali 3 ni ANGALAU suluhisho naona wanamashiko. Tume zote zilizotangulia zilikuja na muundo wa serikali3, hapa chama tawala wajiulize mara mbilimbili, ushabiki uachwe kando, tafukuri ishike nafasi, je tume zote zimeleta mapendekezo ambayo wananchi kweli hawajapendekeza? Hivi ni kweli kuwa uongo uwe tu kwenye muundo wa Muungano?! Viongoz wetu mujifunze kukubali ukweli kama munamuogopa Mungu. Yaani kabisa unajua 4+4=8, halafu ulazimishe jawabu ni 4 4, 448,844, 8=8, 9 au 44?, nafsi haziwasuti kushabikia jambo ambalo kimoyomoyo unajua siyo sahihi ila kwa maslahi yaliyojificha unasema ni sahihi? Tuwe wacha Mungu.