Kura yako ipo kituoni sio nyumbani kwako

Wewe piga usioige Kama namna ni hiihii wao atashinda milele
 
Kwani ni lazima? Mbona mnajidai kama mnatoa masomo,kushawishi na kubembeleza?Kwani wanawakosesha kitu gani ninyi mkienda wao wakagoma/kuacha kupiga kura?
 
Hata ukipiga kura wanaiba na kuongeza kura feki kama kawaida yao miaka yote.

Bora nitulie home ninywe mbege na mupenzi wangu.
Kuliko kwenda kupigishana kelele na maccm na policcm.
 
 
Hata ukipiga kura wanaiba na kuongeza Kura feki kama kawaida yao Mika yote.
Bora nitulie home ninywe mbege na mupenzi wangu.
Kuliko kwenda kupigishana kelele na maccm na policcm.
Na ukumbuke,inaweza kutokea fujo baada ya watu kuudhiwa na jambo halafu upigwe marungu au hata risasi ufe.Sasa ufe kwa ajili ya mambo ya kijinga?
 
Kama usipopiga wanaweza kukupigia, wanashindwa nini kujaza kura za uongo? Iwapo mtu mmoja anaweza kupiga kura zaidi ya mara moja, huo ni ushahidi tosha hakuna uchaguzi hapo.
 
Mi naona hata kampeni asipige ili kuokoa hizo pesa mama ameamua awaondoe chadema ili abaki mwenyewe maana hataki reforms kwenye tume ya uchaguzi,
Asitumie nguvu nyingi kuzunguka nchi nzima maana anauhakika wa kushinda
Ila mimi sitapoteza muda maana kura haziheshimiwi
Unakuta msimamizi wa kituo ana kura feki za ccm 200 zinaingizwa kabwa ya zoeli la upigaji kura kuanza
 
Mimi nitakaa nyumbani,kama kura iko kituoni achana nayo ibaki hukohuko ila mimi nabaki nyumbani. Alishasema Nape akiwa Bukoba,akasema yule aliyekuwa DC wa Longido lkn zaidi aliyekuwa mgombea mwenza wa kiti cha Raisi mwaka 2020 upande wa CCM akesema hivi "Hata utie sukari kiasi gani ndani ya ziwa haiwezi kukoza"

Sasa mimi ni mpumbavu kiasi gani niendelee kushiriki ligi ambayo bodi ya ligi ni ileile na kiongozi wa TFF ndiye anayeteua wajumbe wa hiyo bodi?
 
Andiko kubwa poor logic. Badala ya kwenda kupoteza mda kupanga folen ntatumia huo mda kulima tuta la viaz. Ni hivi, hiyo forgery huko kafanyeji mradi mie sijashiriki kuhalalisha haramu
 
Ccm wanaandikisha wanachama wao huku wanawaomba na vitambulisho vya kupigia kura...ni lazima, ili usipoenda..wanaenda kutiki kwa niaba Yako. Wanabuni njia za wizi Kila kukicha, wametishwa kuwa hatupi kura wameanza kubuni njia mpya za wizi 🤣. Ni hatari sana watu siku nzima wanakaa kubuni kuiba, kudhulumu, kupoteza wengine...yaani kaz ya kutwa nzima
 
"Changamoto kubwa ya ulimwengu kwa sasa ni kwamba wenye akili hawataki kujihusisha na siasa,hivyo wajinga wamepewa mamlaka ya kutawala wenye akili na wasio na akili"
Donard Trump
Hii nukuu aliitoaga Plato kabla hata ya ujio wa YESU Trump aliipandia tu.
Plato — 'One of the penalties of refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors.'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…