Uchaguzi 2020 Kura za maoni Kyela ni kitendawili na zinashtua

Uchaguzi 2020 Kura za maoni Kyela ni kitendawili na zinashtua

Katika hali ya kushtua na inayopiga butwaa ni kubwagwa kwa Mwakyembe kura za maoni

Mawaziri wa kiume woote kasoro yeye tu wamepita kwenye kura za maoni

Manaibu waziri pia woote , yaani wote hata wale waliotoka upinzani wamepita

Cha kwanza nakosa imani na kura za maoni majimbo yaliyokuwa na mawaziri , nanusa harufu fulani ya mkono wa mtu katika kura za maoni majimbo ya mawaziri na manaibu waziri

Pili ,nashindwa kuwa na jibu inakuaje Mwakyembe peke yake waziri katika mawaziri wote wa kiume yeye pekee tu apoteze kura za maoni?
Omary mgumba?
 
Karata za mtu fulani zimekataliwa majimbo 2 tu:- Kigamboni na Kyela tu. Lkn ukweli ni kwamba kuna namna. Naendelea na ukusanyaji wa data nitaleta uzi humu very soon.

Sio bure yaani kwa ile mikura tofauti na waliokuwa na spirit ya kushinda kweli
 
Wanyakyusa sio watu kama unabisha nenda kaishi nao.MWAKYEMBE ALIKUWA ANA WA FOOL KUMBE WANAMCHEKI TU LEO KAWATEGEA SHINGO WAMEPITISHA KISU.
Mwakyembe ni mzee mhuni pia muongo muongo.
Hakuna cha ziada alichofanya kyela uy baba, kyela mjini tu hakuna barabara!! na ukizingatia ni hiyo inayotumika kupita kuelekea kwao! sio kwamba ana dharau tu bali HAJITAMBUI PIA. #heri kyela ipumue kwasasa
 
Wanyakyusa sio watu kama unabisha nenda kaishi nao.MWAKYEMBE ALIKUWA ANA WA FOOL KUMBE WANAMCHEKI TU LEO KAWATEGEA SHINGO WAMEPITISHA KISU.
Mwakyembe ni mzee mhuni pia muongo muongo.
Kwani huyo mzee amekwama wapi?

Wanyakyusa ahahahhahahah nawajua hao ni majirani zangu kule home hahahahahha
 
Hakuna igizo au mpango fulani hapa? Kwa nini ni yeye tu peke yake kati ya mawaziri?
Inategemea alivyoishi na wapiga kura wake.
Jamaa ana kibuli cha kupata.
Kumbuka alivyomjibu Roma.
Alidai hawezi kusikiliza ushauri wa mtu mwenye darasa la 7 wakati yeye ana digrii 4.
Hakuwa mwanasiasa, maana viongozi wengi wa CCM ngazi matawi mpaka kata wana elimu hiyo.
Apambane na hali yake.
Asubiri viti maalumu kutoka kwa swahiba wake, ila wananchi wameshamkataa
 
Mwakyembe mzee wa Madgrii manne, wajumbe wa la saba wameonyesha umhimu wao kwenye maisha yake.
Wamegombana nini? Kwa nini mawaziri karibia wote wameshinda kwa kishindo kasoro yeye?
 
Kuna naibu Waziri pia kaangushwa na Babutale huko Morogoro
wewe kutoka mawaziri 40 wameshindwa kura za maoni watatu

Halafu mawaziri wote na wengine ambao nahisi kuna namna wameshinda kwa kuzoa mikura yaani tofautisha na wengine waliohangaika kushinda
 
Back
Top Bottom