Kurejea kwa 'Bongo Muvi' kupitia tamthilia, waandaaji wamejifunza au watarudi kule kule?

Kurejea kwa 'Bongo Muvi' kupitia tamthilia, waandaaji wamejifunza au watarudi kule kule?

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Kwa muda sasa ni kama nimegundua kuibuka upywa kwa ushabiki wa kazi za nyumbani haswa kupitia tamthiliya mbali mbali kwenye TV.

Ni Muda mrefu sana sijaona Watu wamekaa kuangalia Kazi za nyumbani kama ninavyoshuhudia sasa maeneo mbalimbali, kuanzia majumbani hadi kwenye mabaa huko mitaani.

Swali la kujiuliza ni je, hizi ni juhudi za Wana tasnia au ni kuwapongeza juhudi za stesheni za TV kutoa kipaumbele kwa kazi za nyumbani na kupelekea Jamii kuvutika kuangalia?.

Swali lingine la kujiuliza ni je, Wana tasnia wamejifunza kutoka makosa waliyoyafanya awali yaliyosababisha Jamii kuipotezea Bongo muvi, au tutarajie mazoea yale yale na baada ya muda Watanzania watachoka tena na kuipa kisogo tasnia?.

Ni nini cha kuwashauri Watayarishaji na Wasanii?.
 
Dstv wamewapa promo kwa kuwatengea channel yao.

Na mimi si mpenzi wa hizo Bongo movie ila nilipomuona Joti nikaanza kuwa muangaliaji wa tamthilia ya Mwantumu.

Ila Wazambia ndio wanakimbiza na tamthilia yao ya MPALI iliyoingizwa sauti za kiswahili.
 
Mwanzo walibugi kumpa one step entertainment hakimiliki ya kazi zao.
Hili kosa lilipelekea kufa kwa bongo movie mapema sana.

Now kosa hili lisijirudie tena.

Pia wakati huu filamu zetu zinapaswa kutumia waigizaji wasomi kutoka katika vyuo vyetu.
Hiki ndo kimeibeba HOLLYWOOD. WAIGIZAJI WENGI NI WASOMI WANA ELIMU YA WANACHOKIIGIZA.

Sababu ya kujihusisha na siasa pia iliua bongo movie.

Hili niliweke wazi kabisa Watanzania tulimkosea Mungu ili kutuadhibu akatuletea hili dubwana la kuitwa CCM. huwezi lishabikia ukawa na akili au ukafanikiwa unakuwa mtu wa hovyohovyo tu.
Angalia wanachofanya waigizaji wetu kipindi cha kampeni upuuzi upuuzi mtupu..na kinachopelekea hivyo ni njaa.

Now wasijichanganye tena uigizaji ni sanaa inayoimulika serikali kwa undani sana. Thats why HOLLYWOOD kuna movie zinazohusu CIA,FBI, white house.

Kwetu hapa watu wasiojulikana ilipaswa iandaliwe filamu, Sabaya the criminal, Makonda misifa. Haya matukio yalihitaji filamu.

Jeshi letu pia lilipaswa kutuonesha walichoko nacho kupitia movie na sio kubeba magogo sikukuu za uhuru.

Police waruhusu matumizi ya nguo na vituo vyao katika filamu kuweka uhalisia.
Sio kila movie "mimi ni afisa wa police kutoka kituo cha kati"🤣

Jambo la mwisho ni rushwa ya ngono.
Waigizaji wengi kipindi kile walipata nafasi kwa sababu walikuwa wanapigwa mbupu na ma producers.

HAwakuangalia ubora wao na vipawa.
 
Wazambia wako vizuri Mpali ni nzuri hakuna ma makeup na kuvaa kama wamarekani ina reflect maisha halisi ya watu.
Inanikumbusha siri ya mtungi.
 
Zamani niliwahi kuona tangazo la Ray anatafuta waigizaji, sentensi yake ya mwanzo ilikuwa, kama unajiona wewe ni mrembo na unataka kuigiza, fika ofisi zetu zilipo Sinza blah blah.
Watu wanatafuta vipaji sio warembo. Kwamtazamo wangu, Lupita Nyong'o kabla ya kutoka angeenda kwa Ray asingempa kazi kwasababu hana mikorogo
 
Bongo movie wanachemka kwenye waigizaji wao.Wanaangalia watu wanao trend social networks, akina dada wenye mishape na wenye sura nzuri, waigizaji wa kiume wana angalia ushombeshombe/hb ,kwao upande wa casting uzuri 90% talent 10%,vingine utajulia mbelembele matokeo yake story nzuri waigizaji wabovu.

Sasa husiombee ukutane na story mbovu waigizaji wabovu, utatamani uwaambie wenye ving'amuzi wakurudishie hela yako.

Wee Pierre Likuid na Nicolejoyberry nk nao waigizaji siku hizi, wadangaji wa mjini wote wamekimbilia bongo movie.
 
Mwanzo walibugi kumpa one step entertainment hakimiliki ya kazi zao.
Hili kosa lilipelekea kufa kwa bongo movie mapema sana.

Now kosa hili lisijirudie tena.

Pia wakati huu filamu zetu zinapaswa kutumia waigizaji wasomi kutoka katika vyuo vyetu.
Hiki ndo kimeibeba HOLLYWOOD. WAIGIZAJI WENGI NI WASOMI WANA ELIMU YA WANACHOKIIGIZA.

Sababu ya kujihusisha na siasa pia iliua bongo movie.

Hili niliweke wazi kabisa Watanzania tulimkosea Mungu ili kutuadhibu akatuletea hili dubwana la kuitwa CCM. huwezi lishabikia ukawa na akili au ukafanikiwa unakuwa mtu wa hovyohovyo tu.
Angalia wanachofanya waigizaji wetu kipindi cha kampeni upuuzi upuuzi mtupu..na kinachopelekea hivyo ni njaa.

Now wasijichanganye tena uigizaji ni sanaa inayoimulika serikali kwa undani sana. Thats why HOLLYWOOD kuna movie zinazohusu CIA,FBI, white house.

Kwetu hapa watu wasiojulikana ilipaswa iandaliwe filamu, Sabaya the criminal, Makonda misifa. Haya matukio yalihitaji filamu.

Jeshi letu pia lilipaswa kutuonesha walichoko nacho kupitia movie na sio kubeba magogo sikukuu za uhuru.

Police waruhusu matumizi ya nguo na vituo vyao katika filamu kuweka uhalisia.
Sio kila movie "mimi ni afisa wa police kutoka kituo cha kati"🤣

Jambo la mwisho ni rushwa ya ngono.
Waigizaji wengi kipindi kile walipata nafasi kwa sababu walikuwa wanapigwa mbupu na ma producers.

HAwakuangalia ubora wao na vipawa.
Hapa nime note point kubwa ya tasnia kudidimizwa na Wadau wasiojali kingine zaidi ya kipato.

Ni kweli kwa Kampuni iliyokuwa imeshika Bongo Muvi ilikuwa na nafasi ya kufanya makubwa na kuifikisha tasnia mbali...lakini kinyume chake ndiye alikuwa muuwaji wa Bongo muvi.

Nadhani kuna matumaini kwa Kampuni kama AZAM maana kwa kuanzisha tu kitengo cha 'Sinema zetu' ilikuwa ni hatua moja kubwa sana bila kujali watapata nini kutoka Bongo muvi/tamthiliya za nyumbani.

Tupongeze pia na channel nyingine zilizoingia humo na kutanua wigo.
 
Hata izo tamthilia bado. Imagine umekaaa unaangalia tamthilia ya dakika 45 afu nusu saa nzima imetumika kukuonyesha ray kigosi anageuza gari au anafunguliwa geti anapita na gari. Huo ujinga huwezi ukuta kwenye muvi za mambele huko
Nimewahi kuwataja kina Ray, JB n.k kama Watuhumiwa namba moja ya walioiua Bongo muvi.

Hawa na Wenzao walishika Tasnia wakishirikiana na Wasambazaji walikuwa wametanguliza pesa mbele.

Ipo haja Kampuni kama Azam na wengine kujifunza vizuri ujinga uliofanywa na kina Ray na steps wao wakauwa tasnia ili wasije wakarudia makosa.

Hawa Wasanii kuwapa full control ni hatari maana wao kipaumbele ni pesa na umaarufu, kama alivyokuwa steps alishika mpini...kwa sasa nao kina Azam, dstv na wengine wasiruhusu ule ujinga ujirudie.
 
Haswa DSTV wanawa shape sana Bongo movies wanaaza ku improve...
Kabisa, wasiruhusu ujinga wa bora liende.

Ikiwezekana Azam, dstv, Star times n.k waanzishe sheria zao za kuendesha hizi kazi.

Hata Hollywood miaka ya 1920's walianzisha sheria za Holywood za Uandaaji Filamu...lengo lilikuwa kuondoa ujinga na kuleta heshima kwa tasnia.

Holywood wana sheria mpaka ya kiwango cha mwisho cha chini 'low budget' kwa kuandaa kazi ya filamu.
 
Bongo movie wanachemka kwenye waigizaji wao.Wanaangalia watu wanao trend social networks, akina dada wenye mishape na wenye sura nzuri, waigizaji wa kiume wana angalia ushombeshombe/hb ,kwao upande wa casting uzuri 90% talent 10%,vingine utajulia mbelembele matokeo yake story nzuri waigizaji wabovu.

Sasa husiombee ukutane na story mbovu waigizaji wabovu, utatamani uwaambie wenye ving'amuzi wakurudishie hela yako.

Wee Pierre Likuid na Nicolejoyberry nk nao waigizaji siku hizi, wadangaji wa mjini wote wamekimbilia bongo movie.
Paragraph yako ya mwisho ina point kubwa Sana nadhani ni kitu ambavyo wanatasnia waifanyie kazi hata mimi binafsi sipendi Huu utaratibu wa kuwapa nafasi watu wanaotrending na watu maarufu kwenye movie zao na most of them nimewaona hawana talent kabisa ya uigizaji mtu kama gigy money,Pierre, nicole hawaoneshi kabisa uhalisia kwenye uigizaji mpaka unashangaa huyo director wao anafanya upuuzi gani? Ingawa kuna baadhi yao wapo vizuri kama mimi mars, nandy
 
Kidogo naweza kukupinga kuhusu Gigy.

Nimemuona kidogo na amenishawishi ana kitu, ila ni kama tu atapata script zinazomfiti.

Watu kama Gigi ni character zilizo tayari ni namna tu ya kuwatumia...na hili huanzia kwa Muandishi ambapo naye anapaswa kuwa tayari anamfahamu vizuri Gigi.

Kuhusu kina Pierre sijabahatika kuwaona wakiigiza lakini sio mbaya kuwatumia, sanaa haina mipaka.

Watu kama hao huwa wanatumika kwenye roles ndogo na haswa kwa kile walicho na umahiri nacho, tatizo tasnia yetu bado sio ya kibunifu sana kuwezesha hayo...nafahamu mapungufu ya tasnia yetu huwa wanalazimisha tu mambo.

Ila hata wao wana nafasi ya kujipima wana uwezo wa nini na kama wanaona role wanazopewa haziwafiti wakatae badala ya kujichoresha.
 
Back
Top Bottom