Kurejea kwa 'Bongo Muvi' kupitia tamthilia, waandaaji wamejifunza au watarudi kule kule?

Kurejea kwa 'Bongo Muvi' kupitia tamthilia, waandaaji wamejifunza au watarudi kule kule?

SIKU HIZI WANAJITAHIDI TAHIDI SANA

ila wengine wananyimwa nafasi kutokana na wasanii au mastaa wasio waigizaji kuhamia huko kwenye tamthilia

AZAM NA DSTV wanajitahidi kupromote local content....
 
Zamani niliwahi kuona tangazo la Ray anatafuta waigizaji, sentensi yake ya mwanzo ilikuwa, kama unajiona wewe ni mrembo na unataka kuigiza, fika ofisi zetu zilipo Sinza blah blah.
Watu wanatafuta vipaji sio warembo. Kwamtazamo wangu, Lupita Nyong'o kabla ya kutoka angeenda kwa Ray asingempa kazi kwasababu hana mikorogo
Ray ni kiazi hana elimu yeyote ya uigizaji seuze ya darasani
 
Unakuta shombe la kiarabu linaigiza scene ya huko mwitongo ndani ndani [emoji2]

Tangu lini mwarabu akaishi mwitongo nyie[emoji1787][emoji2]

Ila daaah wana mazoba yao yanapendaga sana hao makitu yao
 
Mwanzo walibugi kumpa one step entertainment hakimiliki ya kazi zao.
Hili kosa lilipelekea kufa kwa bongo movie mapema sana.

Now kosa hili lisijirudie tena.

Pia wakati huu filamu zetu zinapaswa kutumia waigizaji wasomi kutoka katika vyuo vyetu.
Hiki ndo kimeibeba HOLLYWOOD. WAIGIZAJI WENGI NI WASOMI WANA ELIMU YA WANACHOKIIGIZA.

Sababu ya kujihusisha na siasa pia iliua bongo movie.

Hili niliweke wazi kabisa Watanzania tulimkosea Mungu ili kutuadhibu akatuletea hili dubwana la kuitwa CCM. huwezi lishabikia ukawa na akili au ukafanikiwa unakuwa mtu wa hovyohovyo tu.
Angalia wanachofanya waigizaji wetu kipindi cha kampeni upuuzi upuuzi mtupu..na kinachopelekea hivyo ni njaa.

Now wasijichanganye tena uigizaji ni sanaa inayoimulika serikali kwa undani sana. Thats why HOLLYWOOD kuna movie zinazohusu CIA,FBI, white house.

Kwetu hapa watu wasiojulikana ilipaswa iandaliwe filamu, Sabaya the criminal, Makonda misifa. Haya matukio yalihitaji filamu.

Jeshi letu pia lilipaswa kutuonesha walichoko nacho kupitia movie na sio kubeba magogo sikukuu za uhuru.

Police waruhusu matumizi ya nguo na vituo vyao katika filamu kuweka uhalisia.
Sio kila movie "mimi ni afisa wa police kutoka kituo cha kati"🤣

Jambo la mwisho ni rushwa ya ngono.
Waigizaji wengi kipindi kile walipata nafasi kwa sababu walikuwa wanapigwa mbupu na ma producers.

HAwakuangalia ubora wao na vipawa.
Mimi ni afisa wa polisi kutoka kituo cha kati halafu mkononi ana kitambulusho cha mpiga kura 😂😂
 
Sijasikia mnawaongelea bongo Hood, jamaa movie zao zimejaa uhalisia sana. Kwa mfano bongo movie utakuta kwenye kupigana wanatukanana mjinga weweeee, pumbavuuuu, nk.lakini Kiuhalisia mtaani utasikia msen*, kum*** nk . Tapeli.com[emoji95][emoji95]
 
Nimefurahi kuona huu uzi una nguli wa filamu wanatoa ya moyoni. Uzuri wa JF kila mtu ana sekta yake anayoijua kiasi kwamba anaweza changia kitu ukaona mantiki kabisa
 
Bongohood wale wanajua sana wale...nikimisi filamu za bongo natazama hizo movie zao..wako katika uhalisia sana.
 
Mimi ni afisa wa polisi kutoka kituo cha kati halafu mkononi ana kitambulusho cha mpiga kura 😂😂
Leongo ni tufikie hapa
 
Dstv wamewapa promo kwa kuwatengea channel yao.

Na mimi si mpenzi wa hizo Bongo movie ila nilipomuona Joti nikaanza kuwa muangaliaji wa tamthilia ya Mwantumu.

Ila Wazambia ndio wanakimbiza na tamthilia yao ya MPALI iliyoingizwa sauti za kiswahili.
Hivi Mpali sio wanaija?
 
Back
Top Bottom