Kurejea kwa 'Bongo Muvi' kupitia tamthilia, waandaaji wamejifunza au watarudi kule kule?

Ray hajui kuigiza na sijawahi muelewa yeye anapayuka tu.
 
Dstv wamewapa promo kwa kuwatengea channel yao.

Na mimi si mpenzi wa hizo Bongo movie ila nilipomuona Joti nikaanza kuwa muangaliaji wa tamthilia ya Mwantumu.

Ila Wazambia ndio wanakimbiza na tamthilia yao ya MPALI iliyoingizwa sauti za kiswahili.
Yaaa,mpali noma!
Hata jua Kali,duh kwa bongo imetisha!
Huba ya kawaida
 
Hata izo tamthilia bado. Imagine umekaaa unaangalia tamthilia ya dakika 45 afu nusu saa nzima imetumika kukuonyesha ray kigosi anageuza gari au anafunguliwa geti anapita na gari. Huo ujinga huwezi ukuta kwenye muvi za mambele huko
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119]
 
Na rommy ndugu yake dai,eti nae anaigiza!!!?
 
Yaaa,mpali noma!
Hata jua Kali,duh kwa bongo imetisha!
Huba ya kawaida
Kama kina Azam watashika hatamu vizuri huenda tukaendelea kuona mazuri zaidi na hata kufikia kazi nzuri kama zinazofanyika huko nje.

Ila kama nao watataka kuwaachia Waigizaji full control yatajirudia yale yale.

Kina Ray au JB sio watu wakuzingatia sana weledi kama utawaacha huru wafanye watakavyo, wao siku zote watakimbilia wanachokifikia kwa urahisi ili yao yaende....hatimaye tutarudi kule kule na Mashabiki kuipa tena tasnia kisogo.

Huo mfano wa mdau hapo juu kwamba nusu saa nzima Mtu anageuza Gari ndio yale yale yaliyokuwa yanafanyika Bongo muvi za steps..sasa Steps yeye hakujali ila sasa kina Azam, dstv n.k.wasikubali tena.
 
 
Wazambia wako vizuri Mpali ni nzuri hakuna ma makeup na kuvaa kama wamarekani ina reflect maisha halisi ya watu.
Inanikumbusha siri ya mtungi.
Inaoneshwa chanel gani lini na saa ngapi?
 
Dstv wamewapa promo kwa kuwatengea channel yao.

Na mimi si mpenzi wa hizo Bongo movie ila nilipomuona Joti nikaanza kuwa muangaliaji wa tamthilia ya Mwantumu.

Ila Wazambia ndio wanakimbiza na tamthilia yao ya MPALI iliyoingizwa sauti za kiswahili.
Ila Nguzu ni mnyama aisee...
 
Waanze kukuza talent mpya sasa wasing'ang'anie wakongwe
 
Za Azam bado kidogo. Filamu au Tamthilia za Bongo Movie zipo viwango zipo Dstv.
Hiyo ni kwa sababu dstv wanaweka vigezo.

Nimetoa mfano hapo juu namna ambavyo Holywood tangu 1920's walikuja na sheria zao kuhakikisha kazi hazifanywi kiholela ili kulinda hadhi na soko.

Azam wawe makini na wafuatilie maoni ya Watazamaji wao kwa ukaribu ili baadae wasije kukosa Watazamaji wa hizo tamthiliya kwa kuponzwa na Wasanii...twajua wao wana content nyingi za kuonesha hata bila Tamthiliya lakini chonde chonde wasiachie njiani nia yao nzuri ya kufufua Bongo muvi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…