Yaani nina maswali mengi na muhimu, nikitulia ntaanzisha uzi wangu na kukutag ili tusichafue uzi wa mleta mada. Swali la mleta mada ni zuri sana,
Poa, wewe andaa tu, siku yoyote.
Ila pia mimi ndie mwanzilishi wa (thread)uzi huu.
Pia nikuache na jambo moja la msingi.
Ni heri uwe Tajiri mpumbavu, kuliko kuwa masikini mpumbavu (au mjinga)
Mungu alipomuumba mwanadamu (roho ya mwadamu)
alimpulizia pumzi yake akawa nafsi iliyo hai. Na katika nafsi ndipo zinakaa akili..
Si tu kuishi vizuri kunahitaji akili hata kumjua Mungu na mbinu zake kunahitaji akili.
Ishugulishe akili yako sanaaa tena sanaaaaaa.
Akili mtu wangu.
Mwalimu darasani au jamii ikikwambia Bangi ni mbaya vijana hamfai kuvuta bangi, je ni kweli ni mbaya ???
Chunguza kweli bangi ni mbaya je ina madhara gani ??
Tusikubali kuwa na mawazo ama fikra za kubebeshwa na mtu fulani, bila sisi wenyewe kuchunguza pande zote na kucompare data.
Mungu humuongezea mwanadamu akili (hekima na maarifa) je umewahi kuwa na juhudi za kumuomba Mungu jambo hilo ama umepuuza na kujiona akili yako iko sawa na inajitosheleza..?
Ni hivo tu mkuu, Mungu kanisii niishi kwa Matumaini, natumainia mazuri mengi mbeleni, so tumaini nililonalo ndilo linanipa furaha siku zote na kunifanya nisikate tamaa kwa lolote, na nikisahau najua Mungu lazima anikumbushe.