Kurithi Kiti Cha Urais sio Ticket ya Kuendelea na Urais. Heshimu miaka 10 Ondoka

Kurithi Kiti Cha Urais sio Ticket ya Kuendelea na Urais. Heshimu miaka 10 Ondoka

Kwani katiba inasemaje Mkuu?, hii inamaanisha miaka aliyotumia kama Maamu basi anahesabika pia kama Rais maana office ni ile ile ya Rais siyo?

Kama ndivyo basi kuendelea ni ivunjifu mkubwa wa katiba kuwqh kutekelezwa na CCM, ikumbukwe yule Mama ni Mtaji mkubwa kwa Wapiga nchi wa hapa mjini kweli watamtemesha mkate?
 
Akiendelea hadi 2030, Tanzania inaweza kuwa kama Yemen au Somalia, makundi, udini, ukabila, tofauti kuongezeka kati ya bara na visiwani, vita kati ya matajiri na maskini, wanawake na wanaume, umaskini wa kutisha kwa wengi, ufisadi rushwa, wizi, ujambazi, utapeli wa ardhi, nyumba, mashamba, kuuza rasilimali zote za Taifa zilizobaki kushamiri zaidi.
Hii comment inatakiwa ifungiliwe uzi wake.
 
Shalom,

Ukiheshimiwa jiheshimu, sasa ukweli ni kwamba miaka 10 Ikulu ni mingi sana, ukihudimu kama Makamu wa Rais na Rais kwa nusu vipindi kiapo chako na kikanuni na kikatiba ni Cheo chako Cha umakamu, chama kimekupa ridhaa ya miaka 10 tu ya umakamu hicho kiti cha juu ni bonus kutokana na kifo cha Rais, kuondoka kwa heshima utaheshimika sana.

Kama ambavyo tunafurahia matunda ya wewe na wao kuheshimika basi ndivyo hivyo kuondoka ni lazima sio ombi.

Ipate kufahamika kwamba katiba, kanuni, taratibu na miongozo kupitia serikali na chama havina budi kuheshimika.

Asiyesikia la Mkuu huvunjika guu chukua chako ondoka imefika mwisho sasa ofisi kubwa kubwa kupewa watu wa bahati nasibu kuokota embe kwenye mikatusi .

Chama hakikumtuma huyo na ukiranja wenye Dira tuzingatie viapo ukipewa maliza ondoka.

Usiposikia la Mkuu ni kujivisha umungu Mkuu mbele ya mashetani wenye viapo vya kuzimu.

Ni hayo tu

Wadiz
Mkuu umeandika kwa ukali na kwa Mamlaka, vipi wewe ni mkubwa kuliko godfather wa ndani ya chama na Mastermind anayeshikilia rimoti mzee wa mjini?
 
Hata ningekuwa Mimi ningepumzika na kuwapisha wengine, Mana kiti ni chamoto na Kila mtu anakitolea macho.
Sijawahi kuwa na madaraka, ila inaonekana madaraka matamu, kupigiwa saluti, kuwa na escorts kila mahali, kutafuta wawekezaji, kuingia mikataba na makampuni, watu, nchi, mashirika nk nk inaonekana kutamu sana,
Kuachia ni labda kutokee nguvu kubwa kukuzidi.
Mseven, Kagame, Putin nk hawataki kuachia madaraka.
Ila mwanamke kuwa kichwa cha nyumba mtihani Sheikh,
Marekani, China, Russia, sina uhakika kama zimewahi kuongozwa na mwanamke.
 
Kwa kawaida Rais wa Nchi hii Huwa anaanza na umri wa miaka 55 na kumaliza akiwa na 65,

Muda wa kustaafu umefika.
 
Huyo Hussein Ally Hassan Mwinyi (HAHM) hafai kabisa. Anafanya miradi isiyo na ulazima, anaharibu fedha tu pasipo ulazima
1. Kulikuwa na ulazima gani wa kuifumua barabara ya Mkapa road na kuijenga upya, ilikuwa na ubovu gani?
2. Kulikuwa na ulazima gani kuvunja barabara ya ya uwanja wa ndege - Mnazi Mmoja?
3. Ujenzi wa soko la Chuini na Jumbi umeghubikiwa na tuhuma za ubadhirifu kiasi kumalizika kwake kumekawia, je kawachukulia hatua zipi watuhumiwa?
4. Vipi ile kesi aliyoshindwa kwa maamuzi ya kukurupuka dhidi ya wawekezaji wa nje mahakama ya ndani na ya kimataifa na atakayelipa fidia si yeye na walipa kodi wa Zanzibar bali walipa kodi wa Tanganyika, rejea maelezo ya Ngurumo.
......

Nami nimesema sana mama 2025 apumzike.....amuweke hata HAHM apige yake 10.....tuko radhiiii
 
Akiendelea hadi 2030, Tanzania inaweza kuwa kama Yemen au Somalia, makundi, udini, ukabila, tofauti kuongezeka kati ya bara na visiwani, vita kati ya matajiri na maskini, wanawake na wanaume, umaskini wa kutisha kwa wengi, ufisadi rushwa, wizi, ujambazi, utapeli wa ardhi, nyumba, mashamba, kuuza rasilimali zote za Taifa zilizobaki kushamiri zaidi.
.
 
IMG-20240409-WA0000.jpg
 
Mwinyi anavyoiendesha Zanzibar, aweza kuwa Rais mzuri tu.
Hamna kitu pale, tuhuma nyingi anatuhumiwa na watu,
Pia hela nyingi anapewa na Bibie,
Hivi mnadhani kwa nini bibie anapenda mikopo sana?
Bibie tangu aingie madaraka ana miaka mingapi?
Alikuta deni la taifa ni kiasi gani?
Je na kwa hivi sasa deni la taifa ni kiasi gani?
 
Back
Top Bottom