Kurudi kwa kasi kwa matumizi ya Plasiki zilizokatazwa; Nani mnufaika?

Kurudi kwa kasi kwa matumizi ya Plasiki zilizokatazwa; Nani mnufaika?

maramojatu

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2012
Posts
2,372
Reaction score
3,108
WanaJF,

Naomba leo kuweka hili jambo hapa. Wizara inayohusika na mazingira wanakaa kimya kuhusu uchafuzi wa mazingira hasa mitaa ya miji.

Plastiki laini hata ambazo zilikatazwa na Waziri zimerudi kwa kasi mtaani. Mbona waziri mhusika au idara husika haichukui hatua yoyote?

Au wanasubiri mpaka mashirika ya kimataifa waanzishe miradi ya usafi?

Kama waziri wa mazingira ameshindwa, namuomba Waziri wa Afya ajitokeze sababu plastic na taka nyingine hasa za kielektroniki zinahatarisha afya ya watu.

Juzi nimeenda kula sehemu ya wazi naona wanafunikia wali na mifuko ya plastic. Hili ni hatari kwa afya sababu ingredients za plastic zinaingia kwenye chakula na zinasababisha saratani na magonjwa engine.

Tafadhali serikali chukueni hatua.

Ijumaa njema wote
 
Yaani kama huna ulazima wa kula humu sehemu wanazouza vyakula, ni heri usile, kwani baadhi yao hufunika wali kwa manailoni, aisee ambapo ni hatari, na mamlaka zipo tu.
 
itakuwa ni JIII ES EM tu - huyo ndo mnufaika wa kila kitu kwa sasa akiwa ametangulizwa mbele na Msoga Gang.
 
Yaani kama huna ulazima wa kula humu sehemu wanazouza vyakula,ni heri usile,kwani baadhi yao hufunika wali kwa manailoni,aisee ambapo ni hatari, na mamlaka zipo tu.
Ni shida tu ki2c. Kila siku naona watoto wadogo wananunua ice cream wanatafuna na vinailon vile mpaka vinakuwa unga. Wizara husika zipo zipo tu. Hata kutoa matangazo redioni na kwenye runinga kuhusu madhara ya hizo tabia hawataki. Kama vile inafika sehemu haamini kuwa establishments huwa zinapenda afya mbaya za watu
 
Hii ya kufunika chakula na karatasi za nailoni ipo sana kwa hawa mama ntilie na kiafya ni hatari sana lakini eti waziri wa mazingira yupo wale bwana afya wa kata/wilaya/mkoa wapo hawaoni kama hii ni shida.​
 
Tuombe wizara ya mazingira au ya afya wachukue hatua. Tutajaza ocean road hospital bure
 
Tuombe wizara ya mazingira au ya afya wachukue hatua. Tutajaza ocean road hospital bure
Hii hatari na matibabu pale yamekuwa ghali sana sikuhizi wengi wanashindwa kumudu ila kuna siku jamaa yangu alikiwa pale wenzetu wa upande wa visiwani wanakuja na barua tu wanapatiwa matibabu bure nilishangaa mno. Kwahiyo kuna raia wa upende mwingine wanaweza kupatiwa matibabu bure kabisa na wengine wanapaswa kulipia?​
 
Ndio utaratibu tuliouweka kuwa wale wasipate kero. labda inaweza kuathiri muungano. Kumbuka wakati ule wa KERO za muungano
 
Back
Top Bottom