Kurudia mtihani wa kidato cha Nne kwa udhamini wa serikali je ni suluhisho la kufeli ?

Kurudia mtihani wa kidato cha Nne kwa udhamini wa serikali je ni suluhisho la kufeli ?

nimesikia ktk Taarifa ya Habari ya Uhuru FM kuwa serikali imetangaza kuwa wale wanafunzi wote waliofeli mtihani wa kidato cha 4 mwaka 2012 watatakiwa kurudia mtihani kwa gharama ya serikali.
 
Kufeli mtihani si kufeli maisha.Na shauri wahiyimu hao wapelekwe katika vyuo vya ufundi mfano VETA.Ninaimani watakuwa na mbinu nyingi za ujasiliamali.Hii itapunguza ukali wa maisha.
 
They gone astrAy, bora wasahihishe tena ileile hvyo wanavyotaka kufanya wenye division 4 wana waregard wamefauLu..? fantasy ideA'
 
sasa na sisi tuliopata zero miaka ya nyuma watatufanyia nini mbona ina uamuzi ambao sio fair kabisa.Tunateswa na zero zetu leo hawa wanafanyiwa favor.Hiii serikali ni matatizo matupu yaani.

Si kuna programme ya ku risiti?
Ama nani kawekewa hii. Usipende kutoa toa lawama tu..
 
serikali imesema inaangalia utaratibu wa watahiniwa 240,903 wa kidato cha nne waliopata daraja sifuri katika matokeo yaliyotangazwa hivi karibuni, kurudia mtihani mwaka huu kwa gharama zake.

Source: Habari leo.

tuache unoko na uegemevu(inclination), mwaka jana watoto wengi pia walifeli akiwemo mtoto wa Kikwete aliyepata c ya biology tu hakuna aliyesema watoto warudie mitihani wala masomo. kilichotokea watu walimshambulia sana mtoto wa Kkwete bila huruma na wala hakuna aliyesema apewe nafasi ya kurudia mitihani pamoja na watoto wengine. Hapa kuna na nini safari hii kafeli mtoto wa nani anayelazimisha warudie mitihani waliofeli? RAIS ATOE TAMKO KAMA NI KWELI YUKO FAIR ASIEGEMEE SIASA KUTOKANA NA HASIRA ZA WAZAZI. mwaka huu ndo kuna binaadamu kuliko wa mwaka jana? Hii ni propaganda tu ndugu zangu. Baraza la mitihani limesema bayana mitihani ilisahihishwa KIKAMILIFU NA KWA UMAKINI MKUBWA KABISA. Sasa tatizo ni nini;
1. Mitihani ilikuwa juu ya syllabus ya form four? Tujiulize.
2. Watoto hawakufikia viwango vya kufanya mitihani hiyo- kwahiyo kurudia kutasaidiaje kupandisha viwango hivyo?
3. Mitihani hii ni special sana kwa mwaka huu?
hebu tuangalie mfumo wa shule za private wa kurecruit wanafunzi na kusimamia taaluma ya wanafunzi passmarks kutoka kidato kimoja hadi kingine. passmark kuingia shule za maana kama st. marian ni 80% . cream tupu wanaenda kuule. na mkumbuke kuwa wazazi makini wanapeleka watoto wao wazuri private schools za maana, angalia mfano Mazinde juu, st farncis, st marian grils, feza boys and girls. angalia leo the best 10 schools hakuna public schools hata moja. je shule za serkali zinachukua hatua gani kuiga mfumo huu?
Kwa kuwa suala la watu kupata zero halikuanza leo tangu enzi za mwalimu zero zilikuwepo lakini kwa proportion ndogo sana ya 0.03% hakuna sababu yoyote ya mshiko warudie mitihani. Tunataka scientific reasons and strong arguments to justify this matter especially at this particular point of time in history. Otherwise wanaotaka kuendelea na masomo basi warudie at their own arrangements. Mimi mdogo wangu alipata 0 form four kutokana na sababu za mfumo mbovu wa elimu uliopo katika shule za kata .alichukua hatua akafanya QT then he qualified kuendelea na maandalizi ya kidato cha nne akaperform vizuri akapata credits akaendelea na masomo na kufanikiwa kufanya mitihani ya kidato cha sita.
wizara ya elimu hawako fair. ukweli uko wazi hawa watoto ni wale waliokuwa wakirudishwa darasa la nne na baadae wakaruhusiwa kuendelea na darasa la tano hali uwezo wako ni mdogo. sasa leo tunaposhangaa zero form four inashangaza pia. hawa watoto walichukuliwa kuingia na alama zao 70/250 mtihani wa kiswahili, mtihani wa form two haukuwepo by then. leo wameonesha ukweli tunaanza kupiga kelele maanake nini? sambamba na hilo morali wa waalimu uko chini. na hapa wanajibu jeuri ya Kikwete alipowaita wazee wa DAR pale ikulu na kuwaambia kwamba hana haja ya kura za watumishi wa serkali majority wakiwa waalimu. kwakweli inasikitisha sana kuona FAHARI WAPIGANAPO ZIUMIAZO NYASI AMBAZO PENGINE WALA HAZIKUWAALIKA WAPIGANIE HAPO. HIVI WATOTO WALIWAALIKA WAALIMU NA KIKWETE WAPAMBANE KUPITIA VICHWA VYAO. KIKWETE NA WAALIMU WAKO MNATUANGUSHA SANA KTK NCHI HII MTAKUJA JIBU MBELE YA MUNGU MKUU.

Tuache longolongo mtihani wa kidato cha nne siyo lelemama vijana waambiwe wajibu wao, elimu sio mchezo ni mkakati na utekelezaji wa majukumu NA KWA UPANDE MWINGINE SERKALI NA WAALIMU WAANDAE MAZINGIRA YA KUWAENDELEZA WATOTO WETU. TUTAKUJA KUWA WATUMWA WA AFRICA MASHARIKI KWA HAKIKA.
 
Hivi kuna ukweli wowote juu ya hili swala la urudiaji wa mitihani ya kidato cha nne kutokana na kufeli kwa kiwango kikubwa, na kama ni kweli hawa ndugu ze2 watafanya vizuri kama inavyotakiwa au ndo watafeli kuliko hata mwanzoni?????:lying:
 
Hakuna haja ya kurudia mtihani. Kama shule zimeshindwa kutoa elimu kufuatana na kiwango hata warudie mtihani mara kumi watafeli tu.
Baraza la mitihani wanatoa mitihani kutokana na viwango vilivyowekwa kutegemea na level ya elimu. Hawawezi kuwapa form 4 mtihani wa darasa la saba ili wapasi vizuri.
Inabidi wizara ya elimu iwajibike kuwezesha na kuhakikisha kwamba kila shule inatoa elimu kulingana na viwango vilivyowekwa.
 
Jua kuna miaka ya nyuma watu walifeli pia kama vp waseme watu wote waliofeli kuanzia 2005 warudie paper
 
[table="width: 70"]
[tr]
[td]s0298/0025
[/td]
[td]f
[/td]
[td]mwanaasha jakaya kikwete
[/td]
[td]27
[/td]
[td]iv
[/td]
[td]civ-d hist-f geo-d kisw-d engl-c lit eng-d bio-c b/math-f comm-f
[/td]
[/tr]
[/table]
 
Si kuna programme ya ku risiti?
Ama nani kawekewa hii. Usipende kutoa toa lawama tu..

Dogo hujaelewa swali ndugu mi naulizia usawa upo wapi hapa? Mi nireseat alafu we upewe nafasi nyingine kivipi au we ni nani hapa tanzania.Dogo naona umepania kurudia kuzunguka kama kawa.
 
[table="width: 70"]
[tr]
[td]s0298/0025
[/td]
[td]f
[/td]
[td]mwanaasha jakaya kikwete
[/td]
[td]27
[/td]
[td]iv
[/td]
[td]civ-d hist-f geo-d kisw-d engl-c lit eng-d bio-c b/math-f comm-f
[/td]
[/tr]
[/table]

Aisee huyu ni dhahabu kwa matokea haya ya mwaka huu.
 
Daaaahhh!!!!!! ebwana inasikitisha xo wadogo ze2 ndo wanarudi kijijini kulima........kweli Tz imelala kiutendaji.....JANGA HILI!
 
Taarifa ya wazziri mkuu inasema kuwa itaundwa tume, nafikiri ikishatoa majibu ndio itajulikana kama mitihani itarudiwa au lah, ila haijatangazwa rasmi kuwa itarudiwa ama lah...

Nafikiri kurudia mitihani ni utaratibu wa kimataifa wa kuwawezesha watahiniwa kukidhia pale penye mapungufu, huko vyuoni hujulikana kama supplementary exams wengine hufanya make-up na wanafaulu sana tu....Kwa hiyo nadhani kuna tija katika hili....
 
Kama watarudia mjue kuwa ni uchakachuaji wa fedha zitakazotengwa,pia tume iliyoundwa hakuna lolote ni jinsi tu ya kutenga fungu watu wapate pesa za kufanya mambo yao.
 
nimesikia ktk Taarifa ya Habari ya Uhuru FM kuwa serikali imetangaza kuwa wale wanafunzi wote waliofeli mtihani wa kidato cha 4 mwaka 2012 watatakiwa kurudia mtihani kwa gharama ya serikali.

kama ni kweli,basi serikali imegundua kuwa imehusika na kufeli kwa watoto wa wakulima lakini inashindwa kukubali moja kwa moja kuonesha udhaifu wake,kwa kuwa imehusika basi iwajibike,sio kutupiana mpira tu kwa kumtafuta mchawi,matatizo yapo wazi sema serikali yetu kupitia viongozi wetu,wanafumbia macho haya mambo,kipindi walimu wamegoma warekebishiwe maslahi,serikali haikuwasikiliza na baadhi ya wazazi na jamii kwa ujumla wakawabeza walimu,sasa tatizo kubwa limejitokeza ambalo linamgusa mzazi moja kwa moja,mzazi huyo huyo kakaa kimya na anaendelea kudanganywa na serikali aliyoichagua,nadhani ni wakati wa wazazi kuamka na kuihoji serikali kuhusu utendaji wake na utoaji wa majibu mepesi kwa maswali magumu
 
Waongeze daraja jingine nje ya zero,kama mtihani utakuwa katika mazingira ya mtihani uliopita na usivuje mi naamini basi watu watafeli zaidi.kukaa mwaka mzima nyumbani nani atawlipia tuition.
 
Back
Top Bottom