serikali imesema inaangalia utaratibu wa watahiniwa 240,903 wa kidato cha nne waliopata daraja sifuri katika matokeo yaliyotangazwa hivi karibuni, kurudia mtihani mwaka huu kwa gharama zake.
Source: Habari leo.
tuache unoko na uegemevu(inclination), mwaka jana watoto wengi pia walifeli akiwemo mtoto wa Kikwete aliyepata c ya biology tu hakuna aliyesema watoto warudie mitihani wala masomo. kilichotokea watu walimshambulia sana mtoto wa Kkwete bila huruma na wala hakuna aliyesema apewe nafasi ya kurudia mitihani pamoja na watoto wengine. Hapa kuna na nini safari hii kafeli mtoto wa nani anayelazimisha warudie mitihani waliofeli? RAIS ATOE TAMKO KAMA NI KWELI YUKO FAIR ASIEGEMEE SIASA KUTOKANA NA HASIRA ZA WAZAZI. mwaka huu ndo kuna binaadamu kuliko wa mwaka jana? Hii ni propaganda tu ndugu zangu. Baraza la mitihani limesema bayana mitihani ilisahihishwa KIKAMILIFU NA KWA UMAKINI MKUBWA KABISA. Sasa tatizo ni nini;
1. Mitihani ilikuwa juu ya syllabus ya form four? Tujiulize.
2. Watoto hawakufikia viwango vya kufanya mitihani hiyo- kwahiyo kurudia kutasaidiaje kupandisha viwango hivyo?
3. Mitihani hii ni special sana kwa mwaka huu?
hebu tuangalie mfumo wa shule za private wa kurecruit wanafunzi na kusimamia taaluma ya wanafunzi passmarks kutoka kidato kimoja hadi kingine. passmark kuingia shule za maana kama st. marian ni 80% . cream tupu wanaenda kuule. na mkumbuke kuwa wazazi makini wanapeleka watoto wao wazuri private schools za maana, angalia mfano Mazinde juu, st farncis, st marian grils, feza boys and girls. angalia leo the best 10 schools hakuna public schools hata moja. je shule za serkali zinachukua hatua gani kuiga mfumo huu?
Kwa kuwa suala la watu kupata zero halikuanza leo tangu enzi za mwalimu zero zilikuwepo lakini kwa proportion ndogo sana ya 0.03% hakuna sababu yoyote ya mshiko warudie mitihani. Tunataka scientific reasons and strong arguments to justify this matter especially at this particular point of time in history. Otherwise wanaotaka kuendelea na masomo basi warudie at their own arrangements. Mimi mdogo wangu alipata 0 form four kutokana na sababu za mfumo mbovu wa elimu uliopo katika shule za kata .alichukua hatua akafanya QT then he qualified kuendelea na maandalizi ya kidato cha nne akaperform vizuri akapata credits akaendelea na masomo na kufanikiwa kufanya mitihani ya kidato cha sita.
wizara ya elimu hawako fair. ukweli uko wazi hawa watoto ni wale waliokuwa wakirudishwa darasa la nne na baadae wakaruhusiwa kuendelea na darasa la tano hali uwezo wako ni mdogo. sasa leo tunaposhangaa zero form four inashangaza pia. hawa watoto walichukuliwa kuingia na alama zao 70/250 mtihani wa kiswahili, mtihani wa form two haukuwepo by then. leo wameonesha ukweli tunaanza kupiga kelele maanake nini? sambamba na hilo morali wa waalimu uko chini. na hapa wanajibu jeuri ya Kikwete alipowaita wazee wa DAR pale ikulu na kuwaambia kwamba hana haja ya kura za watumishi wa serkali majority wakiwa waalimu. kwakweli inasikitisha sana kuona FAHARI WAPIGANAPO ZIUMIAZO NYASI AMBAZO PENGINE WALA HAZIKUWAALIKA WAPIGANIE HAPO. HIVI WATOTO WALIWAALIKA WAALIMU NA KIKWETE WAPAMBANE KUPITIA VICHWA VYAO. KIKWETE NA WAALIMU WAKO MNATUANGUSHA SANA KTK NCHI HII MTAKUJA JIBU MBELE YA MUNGU MKUU.
Tuache longolongo mtihani wa kidato cha nne siyo lelemama vijana waambiwe wajibu wao, elimu sio mchezo ni mkakati na utekelezaji wa majukumu NA KWA UPANDE MWINGINE SERKALI NA WAALIMU WAANDAE MAZINGIRA YA KUWAENDELEZA WATOTO WETU. TUTAKUJA KUWA WATUMWA WA AFRICA MASHARIKI KWA HAKIKA.