Kurudisha mabinti waliopata mimba shuleni ni kunyoosha mikono juu na kulikabidhi taifa letu kwa wakoloni mambo leo kwa ajili ya mkopo wa bil 600

Kurudisha mabinti waliopata mimba shuleni ni kunyoosha mikono juu na kulikabidhi taifa letu kwa wakoloni mambo leo kwa ajili ya mkopo wa bil 600

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Fikiria binti asiyekuwa na maadili na alipata malezi mabaya akaanza uhuni akiwa na miaka kumi na nne akapata mimba akiwa la sita. Alafu akajifungua kisha akirudi shule akawa anasoma na mabinti ambao hawajawahi kubikiriwa, hatakuwa na ushawishi mbovu kwao ili waonje utamu wa ngono? Tumejustify mapenzi kabla ya kumaliza shule

Fikiria kijana mvuta bangi ambae alikosa malezi na akaacha shule alafu ukamrudisha asome kisa tu unalazisha amalize shule. Hii sio justification kuwa kuvuta bangi na utoro sio kosa?

Mkopo wa bil 600 umetufanya tujikabidhi kwa wakoloni mambo leo. Hivi kwa rasilimali tulizonazo ndio tumelainika kwa wakoloni namna hii?
 
Miti watapigwa sana, mimba watapata sana, bangi watavuta mnoo, kubakwa watabakwa sana na pombe watakunywa mpaka walewe chakali na mwisho wa siku watarudishwa shule kuendelea na masomo. Upende usipende, tutake tusitake.

Kila mtu apambane na hali yake. Mleta mada pambana na hali yako pia.
 
Inawezekana ndiyo lengo lililo kusudiwa?

Sent from my TECNO LA6 using JamiiForums mobile app
 
Miti watapigwa sana, mimba watapata sana, bangi watavuta mnoo, kubakwa watabakwa sana na pombe watakunywa mpaka walewe chakali na mwisho wa siku watarudishwa shule kuendelea na masomo. Upende usipende, tutake tusitake.
Kila mtu apambane na hali yake. Mleta mada pambana na hali yako pia.
Sisi ni taifa moja
 
Bora kujikabidhi kwa mabeberu kuliko kwa wachina, beberu hata uzidiwe vipi na deni lake akamati mali na aachi kukukopesha. Mchina atakamata Bandari, airport, ziwa victoria, mlima kilimanjaro.

Beberu anahofu ya Mungu Mchina amjui Mungu pesa mbele utu nyuma.
 
Fikiria binti asiyekuwa na maadili na alipata malezi mabaya akaanza uhuni akiwa na miaka kumi na nne akapata mimba akiwa la sita. Alafu akajifungua...
Fikiria jamii ambayo ni halali kuoa binti mwenye miaka 13 lakini inashangaa wa miaka 14 kupata mimba.

Fikiria jamii ambayo inaamini mimba zote ni kutokana na uhuni wa mabinti zao.

Fikiria jamii ambayo inaamini kuwa mimba inaambukizwa.

Fikiria jamii ambayo haitaki kuwapa watoto wake elimu ya miili ( ambayo mabibi na mababu zao walikuwa wakiitoa) halafu wanashangaa wanapopata mimba.

Fikiria jamii yenye tatizo kubwa la mimba za utotoni ( sio kwa wanafunzi peke yao) lakini haitaki kuwapa contraceptives.
Fikiria jamii inayoamini watoto wote wanaofukuzwa shule ni wavuta bangi na wanastahili kufukuzwa.

Fikiria jamii inayoona heri kukosa mkopo utaowasaidia kujenga shule kwa ajili ya watoto kuliko kuruhusu binti aliyepata uja uzito kuendelea na masomo.

Baada ya kufikiria hivyo jiulize tena kwa nini nchi hiyo bado ina umasikini wa kutupwa miaka 60 baada ya kupata uhuru kutoka kwa mabeberu.

Amandla...
 
Back
Top Bottom