Kurudishiwa Viingilio vya Mechi Simba vs Yanga

Ng'wanamangilingili

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2015
Posts
5,778
Reaction score
4,859
Sisi #thecommonwananchi tunauliza sijui sijaona mtonyo ukirudishwa wa ile game iliyochakachuliwa ya Simba na Yanga, sisi watanzania ni wazuri sana wa kusahau na kuvumilia mengi.

Nawezekana uliwekwa utraratibu mwingine na wengine hatujui, tuna haki ya kujua au kukumbushwa manake juzi kati nilifanya transaction ya Ncard nikakuta patupu wakati nakumbuka kulikua na mtonyo.

Kama ni tarehe 3 tujue na tusioweza kusafiri kutokea kazulamimba village inakuaje.
 
Ndiyo maana tukasema ile tarehe 17 Machi ilikuwa siku ya huzuni sana kwa wapenda haki, maendeleo na wazalendo kwa ujumla.
 
Mkuu zile hela za viingilio sio wewe tu unayeziulizia mkuu, tupo wengi 👇
 
Ndiyo maana tukasema ile tarehe 17 Machi ilikuwa siku ya huzuni sana kwa wapenda haki, maendeleo na wazalendo kwa ujumla.
Sasa tufanyeje turudishiwe fedha zetu mkuu au tuandamane?
 
Sasa tufanyeje turudishiwe fedha zetu mkuu au tuandamane?
Hapa napendekeza tuishinikize serikali kwa sisi kukataa kula na kunywa chochote kwa siku ^tea-see-knee^ zijazo, hadi pale madai yetu yatakapozingatiwa na kupatiwa ufumbuzi wa kuridhisha. Period!!! Nothing more, nothing less. Au nasema uongo ndugu zangu!???
 
Kinachoenda kwa mganga huwa hakirudi!! Gharama tayari zilikuwa zimetumika! Jiandae kulipa tena 03/07/2021!! Maisha ni kupata na kupoteza! Hesabuni kuwa mmepoteza!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…