Kuruhusu maandamano ya amani ya Chadema, je Rais Samia ameshawachoka wahafidhina wa CCM wasiotaka mabadiliko nchini?

Kuruhusu maandamano ya amani ya Chadema, je Rais Samia ameshawachoka wahafidhina wa CCM wasiotaka mabadiliko nchini?

Kwa kweli leo tarehe 24, inabidi iingie katika historia kwa nchi hii, kwa kuwa ni kwa mara ya kwanza, tokea tupate uhuru kwa serikali yetu kuruhusu maandamano ya amani ya chama cha upinzani!

Ingawa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 18(1) na 18(2) inaruhusu maandamano hayo ya amani, lakini wakati wote vyama vya upinzani, vilipokuwa vikiomba vibali hivyo kwa Jeshi la Polisi, jibu limekuwa kukataliwa kwa visingizio vya kuwa maandamano hayo, yataleta uvunjifu wa amani nchini!

Lakini wakati wote chama tawala cha CCM, kimekuwa kikifanya maandamano hayo, bila vikwazo vyovyote!

Wakati wao CCM wamekuwa wakilyatumia majeshi yetu, ili kutuogopesha sisi vyama vya upinzani ili tusiandamane!

Hata katika maandamano haya yaliyofanyika leo, alijitokeza Mkuu wa Mkoa wa Dar, kueleza kuwa wanajeshi wapatao 8,000 na Polisi wapatao 5,000 watashiriki kwenye yaafi, siku hiyohiyo iliyopangwa kwa maandamano hayo ya amani, yaliyotangazwa na Mwenekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Nimetafakari kwa umakini na kujiuliza, hivi inawezekanaje hawahawa CCM, ambao kwa miaka yote, wamekuwa hawataki kabisa kuruhusu maandamano yoyote ya amani ya vyama vya upinzani, leo hii wakubali ",kiulaini" kabisa maandamano ya Chadema??

Ndiyo nikapata jibu kuwa huenda hata Rais wetu Samia Suluhu Hassan, ameshawachoka hao wahafidhina wake, ndani ya CCM, wasiotaka mabadiliko yoyote ndani ya nchi na wakiamoni pia wao CCM, ndiyo wamepewa "hatimiliki" ya kutawala nchi hii, milele na milele!

Nikapata jibu kuwa, yeye Rais Samia, ambaye pia ndiye Amiri Jeshi Mkuu, ametoa baraka, maandamano hayo yafanyike, kwa kuwa ameshawachoka wahafidhina ndani ya chama chake na wale wanaojiita chawa wa Mama!

Mungu ibariki Tanzania
Ndivyo ilivyo !!
Haiwezekani ukawa unawakubalia mbumbumbu kila wakitakacho !!
Mama anajaribu kuitengeneza legacy yake ya kukumbukwa !!
Watu wanabadilika kufuatana na nyakati lakini MAJITU mengine huwa hayataki kubadilika mpaka yanaenda kuzimu !!
 
CCM ni baba wa siasa za nchi hii. Polepole mmeshaanza kumsifu mwenyekiti wa CCM.. Inapendeza. Njia nyeupe kwa mama 2025
Hivi wewe unafurahia kabisa, kuona kwenye chama chenu, anajitokeza "chief of comedians" anawakosea kabisa heshima wapiganaji wetu, kuwa eti tarehe 24, waje na "hardi brooms" zao ili waje walisafishe jiji??

Hivi kwenye "jon descriptions" za kazi zao, kweli utakuta hilo alilolitaja huyo RC kuwa zimo kwenye majukumu yao ya kazi?
 
Ni hatua moja kwenye uelekeo wa ustaarabu kifikra.
Kuzuia maandamano kwa kutoa sababu zisizokuwa na mashiko hakuna faida yoyote kisiasa.
 
Back
Top Bottom