Wasafi Media iwe ni project ya Joe au isiwe, jamaa wanajitahidi kuwa tofauti sana kwenye hii industry.
Mfano maswali waliyomuuliza huyu boss ni yale yale ambayo yamekuwa debate mtaani.
Pia hawana noma kumpa airtime mtu yoyote hata kama anawadiss. Mfano Carry Mastory, Ney, TID (zamani) na wengine wengi. Naonaga wanapewa interview kabisa kiroho safi.
Hao Clouds sasa. Wakiwa na bifu na mtu au ukiwasema vibaya mpaka mtoto wa chekechea atajua. Mikausho mikali. Mfano hawawezi kabisa kumpa nafasi Dudubaya hata iweje kwa sababu jamaa huwa anawadiss kila siku. Angekuwa anawadiss Wasafi wangesema nae tu.
Wasafi wanajua business na kuoperate kama urban radio/tv.
Kudos!