Kusajili kampuni Brela hadi niwe na sh ngapi?

Singo nakutafuta hapa, nahitaji msaada wako tafadhali.
 
Last edited by a moderator:
mkuu wewe uko mkoa upi kama uko dar nenda pale mnazi mmoja jengo la ushirika zipo ofisi za blrela kule juu horofani, wanasajilisha business name kwa sh 7000 tu kama unahitaji memorandum basi watafute consultant watakusaidia kujkuandikia memorandum au niambie nami nitakusaidia suala hilo

 
Oky aiseeee mpe hongera zake amepiga hatua nzuri sana maana waandishi wa vitabu wako wachache sana siku hizi hapa tanzania mpe hongera zake jamani
ni binti yangu,
mpe muda kidogo anahangaika na usajili huko chuoni kwao.
 
Ila swali lake la msingi halijajibiwa

je ni lazima awe na pesa ya mtaji kwenye account?
 
UFAHAMU KUHUSU KAMPUNI NA USAJILI WAKE: Kuna Kampuni za aina mbili, kampuni ambayo ni Limited by shares na zile ambazo ni limited by guarantee. Zote kati ya hizo zinaweza kuwa private company au public company. Uchaguzi wa ni kampuni ya aina gani itakufaa ufungue hutegemea sana na shughuli unayokusudia kuifanya. Consultant atakushauri vizuri.
Taratibu za kusajili kama zilivyoelezwa na mjumbe mmoja kwa kirefu hapo juu ni rahisi sana kuzitaja ila si rahisi sana kuzitekeleza. Wengi wamezoeshwa kuchakachuliwa, Unamkuta mtu hana uzoefu, elimu wala ufahamu sahihi wa kuandaa memorandum and article of association, anachofanya ni kubadilisha jina katika memorundum nyingine na kuweka jina la kampuni yako kisha kuisajili. Matokeo yake unapata memorundum and article of association ambayo kwanza haiakisi maono yako, pili inaweza ikakosa objectives mtambuka, tatu ni kwamba mambo muhimi ya umiliki wa kampuni yanaweza yakawa hayajawekwa vizuri ili kukulinda founder, ikasababisha watu watakaoingia baadae wakawa na upenyo wa kutake over kampuni yako, lakini kubwa na hatari zaidi, vitabu ambavyo utakuwa umekabidhiwa vinaweza kuwa tofauti na vile viliyobaki Brela. Mtu huyo maarufu kama (Vishoka) Anaweza kukufanyia uhuni wa kupunguza share capital ili alipe pesa kidogo pale brela. na hutaweza kujua mpaka umepata tatizo, au ukafanye rejea. Hivyo nawashauri kufanya kazi na watu competent. Ndio maana consulting company kama ANJOA COMPANY LIMITED zipo kwa ajili yako. wasiliana nasi kwa ushauri, huduma na maoni kwa namba 0759-692024 au 0688-510564 email: info@anjoa.co.tz
 
Ila swali lake la msingi halijajibiwa

je ni lazima awe na pesa ya mtaji kwenye account?

ni vema kuwa na mtaji ila sio lazima huko Brela kwenye kusajili. ila kwa vile unasajili kampuni ili ufanyie shughuli zako itakuwa sio vema kufungua kampuni wakati huna hata shs 100 ya kuendesha shughuli za kampuni unayoisajili
 
unaweza kusajiliwa kampuni yako brela ndani ya siku 3 za kazi. unaweza kuni PM kwa maelezo zaidi
 

Samahani, nataka kuuliza hii brela ni company ina deal na kitu gani hasa, nini maana ya brela?

Na mimi niko mbioni kufungua company yangu, nasubiri facilities zifike tanzania tu.
 
Mkuu nipm namba ya singo nicheck nae
 
ni vema kuwa na mtaji ila sio lazima huko Brela kwenye kusajili. ila kwa vile unasajili kampuni ili ufanyie shughuli zako itakuwa sio vema kufungua kampuni wakati huna hata shs 100 ya kuendesha shughuli za kampuni unayoisajili
Ni kweli nafikiri utakapolitumia hili jina kupata leseni na Tin unaweza kutozwa kodi kubwa ukidhaniwa umeanza kufanya kazi muda wakati ulikuwa wasubiri mtaji.....
 
Samahani, nataka kuuliza hii brela ni company ina deal na kitu gani hasa, nini maana ya brela?

Na mimi niko mbioni kufungua company yangu, nasubiri facilities zifike tanzania tu.

Brela -business registration and licensing agency,ni wakala wa serikali wa usajili na kusimamia makampuni na wapo chini ya wizara ya viwanda na biashara,ukihitaji kusajili waweza nitumia mimi,nimefanya kazi na watu kadhaa wa humu kwa mafanikio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…