Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nataka kufungua kampuni yangu ya udalali (commission agency). Directors ni mimi na rafiki yangu. Sasa pamoja na gharama zote hadi kampuni inasajiliwa, ni lazima niwe na pesa za mtaji kwenye akaunti? Au hata kama sina pesa (mtaji) kampuni yaweza kusajiliwa?
Nisaidieni kujua.
Singo nakutafuta hapa, nahitaji msaada wako tafadhali.
bestito vipi yule mtu wako aliyekuwa anahitaji kuchapishiwa kitabu chake au ndo basi mkuu
ni binti yangu,
mpe muda kidogo anahangaika na usajili huko chuoni kwao.
Ila swali lake la msingi halijajibiwa
je ni lazima awe na pesa ya mtaji kwenye account?
samahani kwa kuchelewa kuja kifaa ninachotumia mara nyingi nashindwa kuona mention ,waweza ni pm ama nipigie 0712742233
Inaanzia Elfu tatu miatano Tsh.3500/-
KUANDIKISHA BIASHARA
Kabla ya kuanza biashara, sharti isajiliwe kwa
mujibu wa sheria za nchi.
Jina la Biashara
Biashara sharti iwe na jina na inaweza
kuandikishwa kama ya mtu mmoja, kampuni,
ushirika au ubia.
Kama biashara yako itakuwa ya mtu mmoja
(sole proprietorship) itakupasa kufuata
utaratibu huu:-
(1)Chagua jina la biashara (2) Andika barua
kwa Mkurugenzi wa BRELA ukiomba
kuangaliziwa jina ulilochagua kama halijasajili
na mwingine (kwa sasa unaweza kuangalia
mwenyewe kutoka tovuti: www.brela-tz.org),
(3) Baada ya jina kupita jaza fomu nambari 2
na 3 ambazo unaweza kuzipata toka tovuti ya
BRELA (4) Lipia ada ya usajili ya Sh. 6,000/=
(5) wasilisha fomu na baada ya siku chache
utapatiwa hati ya usajili.
Kama unataka kusajili kampuni yenye ukomo
(Limited Liability) itakulazimu kuzingatia
yafuatayo:-
(1)Kampuni lazima iwe na watu si chini ya 2 na
wasizidi 50 (2) hakikisha jina la kampuni
utakalopendekeza liwe halijawahi kutumika
katika tovuti ya BRELA: www.brela-tz.org (3)
Andaa hati ya makubaliano (MEMARTs) (4)
Jaza fomu nambari 14a na 14b (5)hakikisha
MEMARTs na fomu 14b zimesainiwa na wakili
au mwanasheria (6)Lipia gharama za usajili
kulingana na mtaji unaoanza nao, (7) wasilisha
maombi yako na hati ya usajili itatolewa baada
ya muda mfupi.
JISAJILI KAMA MLIPA KODI (TIN
NUMBER)
Mfanyabiashara pia anapaswa kujisajili
mamlaka ya kodi TRA. Ili kujisajili unapaswa
kuzingatia yafuatayo: (1) uwe na hati ya usajili
(2) uthibitisho wa eneo la biashara.
LESENI YA BIASHARA
Biashara zote lazima ziwe na leseni na vibali
maalum ambazo hutolewa na ofisi za biashara
za halmashauri ya Manispaa au Wilaya ya eneo
la biashara yako. Baada ya kupata leseni na
vibali toka maamlaka husika unaweza sasa
kuanza biashara yako.
Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
Mkuu nipm namba ya singo nicheck naeKaka kuna jamaa huku JF anaitwa Singo jaribu kumtafuta ni mtu smart sana katika kazi na bei zake ni nafuu na anafanya kazi on time.
Ameshanifanyia kazi yangu ya kufungua kampuni ikiwemo name search Brela,Memorandum baada ya 1week amenikabidhi Certificate of Incorporation.Gharama zake ni ndogo sanaa compare na wengi wa humu ndani.
Ni kweli nafikiri utakapolitumia hili jina kupata leseni na Tin unaweza kutozwa kodi kubwa ukidhaniwa umeanza kufanya kazi muda wakati ulikuwa wasubiri mtaji.....ni vema kuwa na mtaji ila sio lazima huko Brela kwenye kusajili. ila kwa vile unasajili kampuni ili ufanyie shughuli zako itakuwa sio vema kufungua kampuni wakati huna hata shs 100 ya kuendesha shughuli za kampuni unayoisajili
Samahani, nataka kuuliza hii brela ni company ina deal na kitu gani hasa, nini maana ya brela?
Na mimi niko mbioni kufungua company yangu, nasubiri facilities zifike tanzania tu.